Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mchawi hela mkuu, shule nyingi ambazo mitaala wamebase kwenye GCSE Ada zao sio za nchi hii. Niliona mwanang mmoja alikua abasoma Haven of Peace (HOPAC) maburungutu aliyokua analipiwa ada aisee Acha tu

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Wazazi/ walezi wengi wanapenda watoto wao wasome shule bora. Lakini changamoto inakuja kwenye gharama kubwa za kusoma kwenye hizo shule.
 
Hahaaa.mkuu wabongo tunaakili zetu za kuzaliwa nazo.hivi unaweza amaini kuna masela wanashika vitengo mhiumu sana huko nchi za wenzetu lakini walimaliza hapa hapa bongo shule hizi hizi za serikali.Yaana nazungumzia kwamba walijifunza kingereza kwa kiswahili"leo tutajifunza kuhusu nauni......,nani anaweza kunitajia mifano miwili ya nauni?...anaandika ubaoni NOUN".Yaani walianza kingereza kama somo moja darasa la 4,na masomo yote ya kingereza fomu one.
Tusikate sana taamaa .hizo IST,ukiwa na mihela tuu,unakuwa tayari umeshaijua kwamba iko.Ila ukikosa huo uwezo mpeleke mtoto shule yoyote ile na mkazanie atatoboa tuu.
 

Ww unapenda tu kubishana lakini mkuu hapo juu yupo sahihi.
 
Umenipa mambo mengi Sanaa.
 
Mkuu umemaliza kila kitu hapa.
Na mada imeishia hapa atakayeendelea kukubishia hapa huyo ana matatizo.
Angalia maisha anayoishi msanii TID yale ndio mfano wa watoto waliosoma kwenye shule hizo.
TID hajasoma international school , amesema shabaan Robert ni English medium ya kawaida
 
Sasa bila mtihani tutajuaje kama ameelewa?

Shule za internationali ni ujinga mwingine tu wa kuendelea kuamini hao wenye mitaala yao.
Binafsi natamani kuona watoto wafundishwe vitu vilivyo katika mazingira yetu,na vitu ambavyo vinaendesha ulimwengu.
Mf watoto wajifunze
Kilimo kwa vitendo
Uvuvi
Ufugaji
Stadi za kazi
Tehama nk
Hivi viwe kwa vitendo zaidi na sio kukalilishana.

Shule zitengwe kama ilivyokuwa awali,yani shule za
Kilimo
Biashara
Tech nk.
Mtoto ajifunze kitu kimoja tangu kidato cha kwanza,sio anzie kidato cha tano kama tufanyavyo.hii itawafanya wabobee kwenye fani husika tangu awali,hili litawafanya wawe wabunifu zaidi,

Mambo ya shule za kimataifa nao ni aina ta ujinga
 
Nyongeza:

Kusoma na kushindwa kuelewa ulichokisoma.

Hili tatizo huna hata haja ya kwenda mbali. Humu humu tu JF kila siku watu wanasoma vitu lakini hawaelewi walichokisoma.

Sijui huko shuleni walikuwa wanajibu vipi maswali ya insha; ile unasoma insha halafu ukimaliza kusoma unajibu maswali yahusianayo na insha uliyoisoma.

Ni kipimo kizuri sana kupimia uwezo wa mtu wa kusoma na kukielewa alichokisoma.

Imani potofu.

Imagine mtu ana PhD yake tena katika mambo ya sayansi halafu papo hapo anaamini katika uchawi.

Like, seriously?

Unakutana na mdada mtanashati kabisa. Kasoma ana Master’s yake [chagua fani] halafu anaamini katika habari za kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya mapenzi.

Akienda kwa mganga huko, mganga anampeleka baharini huko. Anamwambia avue nguo halafu aoge maji ya bahari.

Wakimaliza huko baharini, anamrudisha nyumbani na makorokoro ya ajabu ajabu akimwambia ndo sijui dawa ya kumtuliza mume or whatever other nonsense.
 
Hayo NI mawazo yako
Na mtoa mada nae ametoa mawazo yake
Raha ya kuishi hapa duniani NI kutofautiana kimawazo na ndio maana kunakuwa na maendeleo

Hatuwezi watu wore kuwa na mtazamo mmoja

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 

Mkuu hawa watu hawana bei za 23 to 25 bei zao ni balaa
 

Attachments

  • CE7E49BA-640E-4E44-B174-240515740993.jpeg
    128.7 KB · Views: 6
Watu wengine wabishi tu. hata kama TID angesoma IST akaharibikiwa, hawezi kutumika kusema kuwa international schools hazifai.
TID hajasoma international school , amesema shabaan Robert ni English medium ya kawaida
 
Nilivyokuelewa ni km vile wanakuwa tayari ni watu kutoka Royal families kwa hiyo mambo ya connection za masomo ya nje ya nchi zipo nje nje,Maana kwa mtu km mimi Kapuku eti nimejichanga changa tuhela twangu twa kahawa au korosho nikajipinda nikampeleka shule hizo za kiinternational bila connection sidhani km mwanangu anaweza kufika ktk vyuo hivyo vya Mamtoni,kwangu ni km naota .
 
Tofauti huwezi kuiona chuo. Utaiona mnapomaliza chuo. Ndo utajua nani wa kimataifa nani wa Mtakatifu Kayumba.
Unataka kusema kwenye competition ya ajira,wale wa International watapa ajira kiurahisi kuliko wa Kayumba hata km GPA za wale wa St.Kayumba ni nzuri kuliko za wale wa International??
 
Tajiri namba moja wa Tanzania bwana Mo kasoma shule gani?? Mo amesoma International School of Tanganyika (IST)

Watu wote tunahangaika kutafuta hela/utajiri. Sasa kama tajiri namba moja kasoma IST unataka kutulinganishia na nani mwingine??
Nimemjibu mdau humu kwamba wanaosoma shule hizo wengi huwenda kusimamia miradi ya familia au kupewa nafasi kwenye mashirika ya serikali kama wazazi au ndugu ni watu wa serikali
Mfano Ni huo uliotoa lakini suala la kukuza vipaji siliafiki sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sio vizuri kwenye mada nzuri kama hii kuweka siasa ila utanisamehe.....Tundu Lissu na Cahadema ndio vinara wa ujinga huu wa kuwa wanajua kiingereza ndio wasomi sana!
Aliongea hivyo wapi na lini?,Au ni chuki tu?
 
Kwa hiyo Sisi akina Uchebe wa St.Kayumba hatuna creativity, reasoning na logic?.
 
Haijaishi umesoma Mpaka level gani foundation ndio kila kitu Nina uhakika reasoning yako and analytical skills zako ni tofauti kabisa na wale watoto wa Breibum na IST
Tatizo wengi mko brainwashed na hicho mnachoita reasoning na analytical skills ambacho kimsingi ni kutekwa kifikra, namaanisha huyo anayekufundisha huko IST sijui na international school gani huko hataki uwe huru kifikra ndo maana anakuingizia ideology za ushoga na unaona ni kitu kizuri kabisa, simply because ameshakuteka kifikra. Wengi mmekwama hapo kwenye ndoto kwamba mtoto wangu akisoma IST atakuwa katibu mkuu wa UN kwa sababu ana analytical na reasoning skills, then what! hivi kuna binadamu hata kama hajakanyaga darasani ambaye hawezi kufanya reasoning na analyisis? labda kama ubongo wake umekufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…