nimekuelewa Sana unachokieleza ni kutafuta maendeleo kwa kuvutia wawekezaji si ndio . Sasa kwenye hili swala serikali ndio zinawajibu wakufanya haya China imeendelea kwa serikali za Mao zhedong naimetumia hii kusomesha wanafunzi huku ikiandaa mazingira mazuri ya uwekezaji. Sasa mpendwa serikali za Africa zimeshindwa kufanya hilii kabisa kwakua zinakumbwa na Mambo mengi a figisu za hao wanaojiita mabeberu kwa kuwa resources zinawindwa vibaya mno. Rushwa nyingi zinaanzishwa na hao mabeberu kwa mfano kina tshombe na Mobutu wa congo wote hao ni mipango ya mabeberu. Hata hapa bongo in 1980's kulikua na mfumo bomba waelimu lakini yule waziri "x" waelimu inasemekana alipewa rushwa akanza kuleta Mambo ya physics with chemistry sijui kutoa michezo mashuleni. Ndio maana Magufuli amemuweka mmama kwa kuona anamsimamo flani.
Sasa mapendekezo yangu ni kutafuta maendeleo kwa kuanzia na vijana. Unajua hata U.S.A ilikua haijaendelea kuliko ulaya lakini ilipo anzisha high school iliwafanya vijana kuweza kuwa creative mno bila ya hata kuwa na vyuo vingi watu Kama kina Edison, Ford, wright brothers waliweza kufanya Mambo ambayo hata dunia ya leo haijayabadilisha. So kwa tz mm naona vijana tuanze kwa mfumo waelimu uliopo maana uko poa Sana sema hatujalenga katika objectives Bali ni kufaulu tu. Tz ni kati ya nchi chache zenye A level system ambao mm ninauona kuwa ni mzuri kwa sababu mtu unasoma misingi ya dunia.
Vijana tukiendelea kusema kila siku serikali hatutatoboa
Mkuu Bruno, nimekuelewa sana ila napingana na mawazo yako kidogo.
Kwanza, "architect of development" wa China ni Deng Xiaoping na sio Mao Zedung. Mao alichukia matajiri na mfumo wa kibepari.
Pili, hamna nchi ambayo haijawahi kuibiwa na "mabeberu". China iligawanywa na wazungu lakini sasa imeweza kuikomboa HK na Macau. Taiwan itakuwa vigumu bila ya kuiharibu uchumi wa China. Marekani anatafuta njia ya kumrudisha nyuma kimaendeleo kama alivyofanya Iran, Iraq na nchi nyingine. China haitaingia kwenye mtego wa kuikomboa Tauwan kwa sababu itakuwa vita vya dunia vya tatu.
Anyway, sikubaliani kuwa vijana wana nafasi ya kutoboa bila elimu ya juu. Sababu ndogo ni kuwa hamna nchi inayojitoboa kirahisi hivyo. Njia kuu ya kujitajirisha ni kuuza bidhaa kwa wingi nje. Na huwezi kufanya hivi bila ya kutumia elimu ya juu yenye mfumo unaokwenda na wakati (MBA imeanza juzi tu UDSM) na kuwa na serikali inayoheshimu demokrasia na yenye sera nzuri za biashara.
Mabeberu wako na wataendelea kuwepo. Ukiwa na serikali bora, italinda maslahi ya nchi na pia itafanya biashara inayoheshimu sheria za biashara za kimataifa.
Nchi nyingi zina asilimalu lakini rasilimali ni mali iwapo umeshazalisha na kuuza. Vijana hawana uwezo wa kufanya biashara hizi bila ya mkopo na elimu.
Wakati wa kutoa sababu nyingi kwa nini Tanzania bado haina uwezo wa kuwapa maji safi na umeme wananchi wake wote hamna zaidi ya mfumo mbaya wa elimu na siasa. Tuna miaka karibu 60 ya uhuru. Nchi nyingine pia zilikuwa vitani na mabeberu lakini zimetoboa haraka sana (Singapore, Malaysia, Vietnam, Indonesia, Brazil)
This excuse hold no water. Hasa ukitegemea kuwa tukiwa na shida tunawatumia mabeberu hawa hawa kuomba msaada kwa zaidi ya miaka 50 mfululizo.
Mwalimu Nyerere mwenyewe, pamoja na kufuata siasa ya kijamaa za akina Mao na Karl Marx, alikwenda Scotland sio Beijing kusoma na aliamua kupata matibabu na kufariki nchi ya mabeberu ya Uiingereza sio China wala Urusi.
Whatever happened to live by example?
Elimu inayokwenda na wakati na yenye mfumo bora kutoka nursery mpaka chuo kikuu ndio njia pekee ya kupata maendeleo haraka. Singapore ni kisiwa chenye watu milioni 5, nusu wakiwa wageni. Rasilimali yake si dhahabu wala mbuga za wanyama bali elimu bora tu. Sasa ni matajiri kuliko beberu wa Uiingereza, mkoloni wake.