Tatizo sio kuongea English, Je, Lugha ya Kiswahili tunajua vema kuiongea na kuiandika? Majibu tunayo, suluhisho sio kusomesha shule za kimataifa. Bali ni kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wetu wa elimu. Tuachane na lugha za kigeni, tujikite kwenye lugha yetu. Ila tuwe wakweli tu, waliosoma hizo international schools kwa hapa Tanzania, sio msaada kwa taifa. Maana hawajabadili lolote katika maendeleo yetu. Ila imekuwa ni ufahari kwenye familia zao, nimekutana nao chuoni, waliisoma namba, nimekutana nao kazini, wamenikera, kwa uvivu maana wanajijua walivyokuzwa.