Hongera, maana umekuwa mzalendo. Jamii yetu imezungukwa na watu (wakulima, wafugaji, wavuvi) wanaoishi katika umasikini mkubwa. Je hizi elimu za IST zimewasaidia hawa watu wetu kuondoka kwenye umasikini? Kujieleza na confidence ni vitu vizuri sana, lakini elimu bora inatakiwa ijikite kwenye kuleta maendeleo ya watu katika jamii yetu na siyo mtu mmoja tu binafsi.
Natamani wanaosifia sana hizo international schools na wao kusoma Universities za nje ya nchi na kuishi huko watuletee mifano ya watu waliotoka hizo shule na kwa jinsi gani wamekuwa msaada/ role models kwa watu wetu wa Tanzania.
Je tunahitaji skills gani kuwasaidia wakulima na wafugaji wetu ambao ndio majority. Tunahitaji watu wa kwenda majukwaani na kwenye makongamano na kuongea kingereza/ kiswahili kizuri? Je ili vijana wetu waweze kujiajiri hapa Tanzania wanahitaji skills gani?
Hebu tuache haya mambo ya kurithiswa/ kuaminishwa na wakoloni tuwaze nje ya Box. Tunahitaji skills zipi za kuwatoa watu wetu kweye umasikini, wazalishe kwa ubora na ufanisi na kupata masoko ya bidhaa zao? Skills gani za kuwawezesha vijana kujiajiri?
Andiko lingekuwa zuri sana kama wangesema muasisi wa kampuni kama ASAS, Tanga milk, Shambani milk, alisoma IST kwa sasa anamiliki kiwanda cha bidhaa za maziwa. Ananunua maziwa kiwa wafugaji pia kaajiri waTanzania kadhaa kwenye processing, distribution na marketing. Hizo habari za exposure za kuishi na kufanya kazi nje ya nchi ni fursa zilizopo kwa vijana wachache sana na hazina trickle down effects kwa waTanzania walio wengi.