bob_fundi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2025
- 457
- 705
Yan huo mtazamo wako uko vizuri sana naunga mkono hoja kwa asilimia 💯.Kila mtoto huja na sahani yake, watoto ni baraka, tajiri na mali zake maskini na watoto wake. Zote hizi ni kauli uchwara zinazoendelea kuongeza idadi ya maskini duniani hasa barani Afrika.
Watu maskini wanazaliana kama mapanya na kuongeza idadi ya maskini na umaskini duniani.
Mtu maskini hapaswi kuzaa mtoto kabisa kwenye hii dunia. Mtu maskini akizaa mtoto anaongeza maskini mwingine duniani.
Unapata wapi ujasiri na nguvu za kuzalisha watoto wengi, wakati unajua hali yako ya kiuchumi ni pangu pakavu tia mchuzi?
Unategemea hao watoto waje kula mawe? Unategemea hao watoto waje wavae majani? Unategemea hao watoto waje kusoma vipi? Unategemea hao watoto waje kutibiwa vipi?
Wakati serikali nyingi duniani zikipambana kupunguza umaskini duniani, Kuna mafukara kutwa kucha kungonoka na kutelekeza watoto mitaani. Halafu yanakuja kuonea wivu matajiri walioji "discipline" kuzaa watoto wachache.
Mateso, shida na matatizo mengi ya watu duniani chanzo ni mafukara mawili yaliyoleta kiumbe duniani bila kuwa na uwezo wa kuhudumia na bila kuwajibika kwenye malezi.
Watoto ni gharama. Watoto wanahitaji pesa. Watoto ni pesa. Huna pesa funga zipu usizalishe. Pambana na umaskini wako kwanza. Sio kuzaa kiumbe kije kiteseke duniani.
Solve your poverty first, before bringing kids to this world. Usilete kiumbe duniani kije kiteseke.
Tena changamoto nyingine ni kwamba unakuta mtu anasaidiwa alafu anazaa kilasiku unakuja kutesa watoto tu kwenye hii dunia