Mtu yoyote aliyewahi kuishi na mwanamke/mwanaume na kuunda familia Hawezi kuwekwa katika Kundi la Kataa Ndoa

Kwani utaratibu wa cheti umeanza lini?

Inamaana babu zetu walioweza endelea hii generation walikuwa hawajui walifanyalo?
Bila cheti hauwezi kua mke na mume kisheria labda muitane tu ila siku ikifika ya kuthibitisha kama nyie ni mke na mume na hamna cheti ndio utaelewa ninacho kwambia.
 
Huwezi ongoza taifa ambalo robo tatu ya Watu ni wakataa Ndoa, hiyo haiwezekaniki.

Ni kama kuongoza taifa la mashetani ambalo mara kwa mara mapinduzi, tamaa mbaya, uchafu utakuwa ndio mila na desturi.
 

Unazungumzia watoto wa miaka 15
Hapa anazungumziwa Mwanamke na mwanaume aliyekamilika
 
Wapo sana maana wamekataa kuhalalishwa na jamii. Na kanisa au msikiti , .... na serikali pia . Ukiwa na ndoa unadhaminika hata kukitokea mgogoro unasaidika kwa haraka
 
Hakuna kitu kama icho ndugu yani bila cheti cha ndoa hawawezi kua mke na mume bali watakua ni mahawala walio ishi kwa muda mrefu

Kwa jicho la kisheria sivyo.
Lakini kwa nature hizo sheria hazitambuliwi.
Ndio maana hata kwenu ukoo mzima sio ajabu wenye vyeti vya ndoa hawafiki Kumi.

Ni sawa useme kama huna cheti cha kuzaliwa hujazaliwa, utakuwa na matatizo ya Akili.

Cheti ni kithibitisho tuu na sio Ndoa. Ni kama Pete n.k.
Cheti kinaweza kupotea au kuungua na moto na bado ndoa ikawepo.

Cheti unaweza ukafoji lakini ndoa huwezi ukafoji.

Kisheria upo sahihi lakini kiuhalisia hauna usahihi wowote
 
Yani ata kama umetoa mahari kama hujafunga ndoa upate cheti uyo sio mke wako ni hawala tu
Wewe mke wako kapewe cheti mimi wangu nalala naye, nazaa naye na anapika na kupakua.

1. Cheti kinakusaidia nini?
2. Nikiwa na cheti napata nini na nikikosa cheti ntakosa nini kwa mwanamke?
 
Wanaume kataa ndoa ni wale wanaokimbia majukumu. Mru anatamba eto ronaldo kataa ndoa wakati mwenzao ana mchumba na watoto kibao wanalea pamoja.

Ronado yupo ndoani miaka na miaka sema kwa jicho la kisheria ndio wanasema hakuna ndoa pale. Ila kiuhalisia wale ni mume na mke
 
Wewe mke wako kapewe cheti mimi wangu nalala naye, nazaa naye na anapika na kupakua.

1. Cheti kinakusaidia nini?
2. Nikiwa na cheti napata nini na nikikosa cheti ntakosa nini kwa mwanamke?
Wewe kaa nae hivyo lakini uyo sio mkeo kisheria
 
wote walio zaa walikua na ndoa....?!
 
Kataa ndoa ni wanaume wasiojiamini, wabinafsi si ajabu hata familia zao zina walakini.

Sio ajabu wala haikatazwi kua muoga na mbinafsi wana haki yako pia ila sasa tatizo ni kuwa wanatumia mbinu ya kuwachafua wanawake ili hoja zao zisikilizwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…