Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
THIS IS VIVID EXAMPLE
 
inawezakana ikawa sio yeye anayehitaji kitabu kuelezewa bali sisi ndio tunavihitaji kumuelewa,kama tunavyohitaji vitabu kuelewa elimu nyengine kama biolojia fizikia etc.
Mungu huyo angekuwepo, asingetupa gharama isiyo na lazima ya kuhitaji kitabu kumuelewa.

Angetuumba ubongo tayari umesha download habari zote za kitabu kumuelewa.

Ukiona unaambiwa kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote, halafu habari zake zimeandikwa katika kitabu, jua huyo aliyeandikwa kwenye kitabu si huyo Mungu anayesemwa.

Kwa sababu Mungu mjuzi hivyo, mwenye uwezo hivyo na upendo hivyo angetupa yote yaliyo katika kitabu katika vichwa vyetu tusingehitaji kuhangaika kujifunza lugha nyingine, kutafsiri, kubishana kuhusu tafsiri na uhjinga mwingine mwingi.

Kwa nini atupe kazi ya ziada viumbe wake anaotupenda wakati ana uwezo wa kurahisisha mambo hayo kwa kutupa kila kitu kichwani?
 
Unaamin hizo story za wagiriki wa kale?
 
Dini yoyote inayofundisha Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uuwezo wote na kaumba kila kitu mwanzo inafundisha predestination.

Hii inajumlisha Ukristo wote, si hayo madhehebu uliyoyataja tu.
 
Wengine huwa ni mashabiki tu. Maada ikishawekwa hata kama haijui ataingangania ndio maana hawezi leta mfano mwingine tofauti ili kusuport wazo lake
 
Unapenda mambo mteremko kiasi hiko
 
Unaamin hizo story za wagiriki wa kale?
Siamini.

Najua kwamba muandishi anayeshindwa kumaliza story logically anaweza kutumia "deus ex machina" kumaliza hadithi.

Hii hapa hadithi fupi inayotumia "deus ex machina".

Willy Janja alikuwa jasusi wa Tanzania aliyefika Pretoria kukusanya nyaraka za makaburu ili kujua mipango yao ya ulinzi dhidi ya ANC.

Tatizo, nyaraka zilikuwa zinalindwa na ulinzi mkali, katika jengo lenye kuta tatu na walinzi mia tatu.

Willy Janja akawa anakuna kichwa, ataingiaje humo ndani.

Pale pale radi kubwa ikapiga, ikavunja kuta zote tatu na kuua walinzi mia tatu, ikafungua vitasa vya jengo, ila haikuunguza nyaraka.

Wwily Janja akachukua nyaraka zote na kutokomea nazo kurudi nazo Tanzania.

Mwisho

Katika utunzi wa hadithi, hadithi hii ina mapungufu makubwa sana.

Imetumia "deus ex machina" ya radi iliyopiga, ambayo imevunja kuta tatu, imeua walinzi mia tatu, imefungua vitasa, haijamuua Willy Janja, haijaunguza nyaraka, na imempa ushindi kiubwete Willy Janja.

Hadithi hii haina "believability".

Habari ya kuwapo kwa Mungu wako ni sawa na hiyo "deus ex machina" ya Willy Janja.

Haina believability.
 
Sasa mkuu wewe unataka kumpangia namna gani aendeshe vile alivyoviunda na system nzima ya universe,yeye ndo kaamua iwe hivyo,hayo unayoleta ni mawazo yako ya jinsi mambo yangetakiwa yawe, sasa na yeye anamaono yake.Hujawahi kujiuliza kwanini kuna baadhi ya viumbe wanaweza kuogelewa bila kufundishwa,na sie binaadamu hatuzaliwi na uwezo huo mpaka kujifunza.?

Tuachane na hayo naomba nkuulize swali,hivi ukiuangalia mwili wa binaaadamu na system nzima ya binaadamu ,uchakataji chakula,mfumo wa fahamu,ubongo na mifumo mingine ilivyo sofistiketedi,unaamini ni vitu vilivyotokea tu kwa bahati mbaya au kuna dizaina?
 
Unapenda mambo mteremko kiasi hiko
Siyo mimi ninayependa mambo mteremko.

Mungu wako ndiye hana logical consistency.

Ameandikwa kama Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Hana sababu ya kutowapa viumbe wake mteremko. Asiwape mteremko kwa nini?

Uwezo anao, upendo anao, ujuzi anao.

Sasa kama tunaona maisha hayana mteremko, tukiuliza kwa nini Mungu hajatupa mteremko si kwa sababu tunapenda mteremko.

Ni kwa sababu tunahoji kama huyo Mungu yupo, kama yupo, mbona anajipinga mwenyewe?

Inakuwaje baba mwenye uwezo, ujuzi na upendo anawafanyia uchoyo wanawe anaowapenda?

Hujajibu swali hili.
 
Nimejibu aya inanasema 'dhul qarnaini aliliona' sasa ww uelewi nn muonaji ni dhul qarnaini kwa upeo wa macho yake

Ni sawa ngoja tuelewe hivyo kwamba ni Dhul-Qarnaini (Alexander the Great) ndiye aliyeliona Jua likizama katika matope.Sasa tunajiuliza hivi Dhul-Qarnaini alizaliwa mwaka 356 na kufariki mwaka 323 kabla ya Kristu kuzaliwa na kabla ya Muhammad kuzaliwa.Je,yeye Muhammad kwa nini hakumuuliza Mungu ni kwa nini Dhul-Qarnaini aliweza kuliona Jua likizama katika matope wakati sio kweli? Mbona kwa mjibu wa aya hiyo inaonekana Muhammad alikuwa ameenda kuwashitakia kwa Mungu baadhi ya watu waliokuwa wanamuuliza Muhammad habari za Dhul-Qarnaini? Ilishindikanaje, Muhammad kumhoji Mungu juu ya ukweli wa hicho alichokuwa Mungu anamueleza kumuhusu Dhul-Qarnaini?
 
Hapana, si kwamba nataka kumpangia.

Naonesha kwamba yeye mwenyewe hana logical consistency, anajipangia, halafu anavuruga alivyojipangia.

Anaumba, anaruhusu dhambi, halafu anajua dhambi itatokea, halafu ikitokea anakasirika na analeta mafuriko.

Tena mafuriko yanaumba mpaka viumbe wasio na hatia.

Kwa nini? Huyu ndiye Mungu wa haki kweli?

Huyu Mungu yupo kweli au ni uongo tu?
 
Katika ulivyo vitaja hapo nikipi kinacho kutesa?
 

Lipi limekufikirisha hivyo, mkuu?
 
Mungu sio mjinga kumwandikia.mtu aseyejua kusoma na kumwandikia uongo

Unamaanisha kwamba kwa kuwa Muhammad hakujua kusoma wala kuandika, basi Mungu asingaliweza kumfanyia roho mbaya ya hivyo ya kumuingiza chaka? Kama ndivyo,sasa umegundua nini katika aya hii ya Jua kuzama katika matope? Huoni kwamba tayari Muhammad aliingizwa chaka kwa kupewa hadithi ya jambo ambalo halipo?Na huoni tayari kwa kutojua kusoma kwa Muhammad kumemharibia CV yake?
 
hivi unaelewa mantiki ya msamiati" muweza wa yote",na mwenyewe upendo kwa wote",.. utajisikiaje baba yako atakapo kwambia kuwa anauwezo wa yote na upendo kwa wote" kisha akapeleka nyama na mchele kwa bimkubwa "(mkewe WA Kwanzaa) halafu kwa bimdogo (mkewe wa pili ) ambaye ndiye mama yako akawalaza na njaa", tokana na ukosefu wa kuwepo kwa chakula nyumbani ""??

tunaposema muweza wa yote na upendo kwa wote huwa tunataka muelewe kwanza mantiki ya misamiati hiyo miwili""
 
heheee heeehee
 
Mleta mada inaonyesha una kichwa kigumu kama nazi ya kilwa. Sasa hapo haujaelewa nini kwamba Dhul-Qarnain aliliona jua likizama kwenye tope kwa upeo wa macho yake?
 
Dini yoyote inayofundisha Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uuwezo wote na kaumba kila kitu mwanzo inafundisha predestination.

Hii inajumlisha Ukristo wote, si hayo madhehebu uliyoyataja tu.

Mkuu mimi ni mtu ninayejadili mambo kwa Logical Consistency.Leo niko na hoja ya Jua kuzama katika matope.Hili la kwako juu ya kwamba hakuna Omniscience,Omnipresence, Omnipotence, God with all Loving and with devine Mercy, nitayaletea uzi wake, siku yake pekee.Kwa hiyo usifikirie hizo hoja zako hazina hazina majibu.
 
Sasa unapomkataza mtoto asiangalie tv usiku si lazima uihamishe kutoka sebuleni uifiche chumbani,utategemea mtoto mwenyewe atafuata maelekezo yako ya kutoangalia tv muda huo uliomkataza,sasa utakapotoka ghafla usiku kwenda sebuleni ukamkuta amekaidi amri uliyompa ukamuadhibu hatakuuliza kwanini umenikataza halafu TV umeiacha mpaka nkashawishika kuingalia ilhali umenkataza,hivyo ndivyo navyoilewa falsa ya dhambi,kwamba kwanini kitimoto kimekatazwa,alafu nguruwe wapo,au kwanini umekatazwa usile mke wa mtu alafu mwenzio alafu huyi mke akawa mzuri na anayetamanisha balaa.

unadhani kuna logic gani ya kuwepo magonjwa alafu kukawa na dawa na mitishamba yanayotibu magonjwa hayo,logical consistency iko wapi hapo.iweje napata mafua,alafu nkinywa tangawizi na asali au salimia,kinapona.hii system imetokea wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…