Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Kwa nini Mungu wako ajitekenye na kucheka mwenyewe?

Kwa nini awezeshe ugonjwa uwepo na dawa badala ya kukataza ugonjwa usiwezekane kabisa?

Na vipi kuhusu magonjwa ambayo hayana dawa?
Nimekuuliza wewe unieleze reasoning kwa upeo wako ya kuwepo magonjwa na tiba duality hyo imetoka wapi,je unamaelezo ya kisayansi yanayoexplain jambo hilo.

kuhusu magonjwa ya siyokuwa na dawa ni suala la ugunduzi/uvumbuzi tu,kuna magonjwa yanayotibika hivi sasa ambayo miaka 10-100-1000 iliyopita yalikuwa hayatibiki wala kujulikana dawa lakini hivi sasa yanatibika,so usiseme gonjwa halina dawa sema gonjwa halijagundulika dawa yake.kisicho na dawa ni ulemavu tu,lakini hakuna gonjwa lisilokuwa na dawa.
 
Wengine huwa ni mashabiki tu. Maada ikishawekwa hata kama haijui ataingangania ndio maana hawezi leta mfano mwingine tofauti ili kusuport wazo lake

Usifikirie nimekuja kufurahisha genge au kwamba nina kahoja kamoja nimekaolkota huko na kisha kukimbia nako hapa.Kwa taarifa yako unajadiliana na mtu anayemfahamu Muhammad, Kurani na Uislamu kwa kina.Kung'an'gania hoja moja ya Jua kuzama ni kuonyesha uweledi wangu katika mijadala.Siwezi kujadili hili na hapo hapo nikawa nimerukia suala jingine.Mpaka hoja hii ionekane kwamba imejadiliwa exhaustively ndio nitahamia hoja nyingine.
 
Kwa nini Mungu ahitaji kutujaribu kama tutafuata haki, ikiwa aliweza kutuumba tufuate haki tu bila kufanya kisicho haki?

Umeongea kwamba dunia ni mtihani/challenge.

Mwalimu ambaye hana ujuzi wote, uwezo wote na upeno wote akitoa mtihani ili ajue mwanafunzi anajua nini, nitaona sawa.

Mtihani una kazi ya kumfahamisha mwalimu, mwanafunzi wake kaelewa nini.

Huyo Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, anayepanga kila kitu na kujua majibu ya maswali yote, kwa nini aweke mtihani?
 
Unahoji wee Mungu[emoji4] [emoji12]
 
Kwa nini Mungu karuhusu magonjwa ya bacteria yaue watu kwa miaka mingi kabla dawa haijagundulika?

Pia, huko Africa kwa mfano, kuna magonjwa mengi sana ambayo dawa zimeshagunduliwa lakini hatuna huko, hatuna vifaa vya hospitali, hatuna ujuzi, hatuna umeme hatuna maji.

Mungu huyo kwa nini anatufanyia uchoyo hivyo kwa mambo ambayo yeye hata hayamgharimu shilingi moja?
 
Unahoji wee Mungu[emoji4] [emoji12]
Dhana ya kuwepo huyu Mungu inajipinga. Ina contradiction.

Contradiction inaonesha huyu Mungu hayupo.

Ni habari imetungwa na watu tu.
 
Tuwekee Ushahidi Mungu anaongea na Muhammad!

Pangoni Hira, Muhammad alikuwa peke yake, unafikiria kutakuwa na shahidi gani tena mkuu? Ukilazimisha sana jambo hilo utaletewa Mijusi,Buibui,kenge na Nge tu.
 
mkuu kuuliza maswali wewe peke yako bila kujibu unayoulizwa sio fea.wewe unuelezee logic ya magonjwa kuwapo na tiba zake zikawapo kisayansi hii ikoje?.
 
Mambo ya iman ukiyadiscuss sana utaomekana kituko
 
Nimesema mtihani as in challenge sio mtihani wa darasani.
Unaposema kwanini amefanya hivi na asifanye vile unazungumzia choices zake yeye sio mimi na yeye ndio anajua kwanini kafanya hivyo,kama wewe ulivyochagua kuwa na huyo uliyenaye na sio mwengine.
 
Mkuu taratibu! Fanya hakuna Mungu, nakama hakuna Mungu hao watoto kwanini wafe kwanini duniani kuwe na kilio? Na sisi binadamu tumetoka wapi nani ni lazima tufe kwanini tufe..sasa! wakati hakuna Mungu?
 
Mkuu taratibu! Fanya hakuna Mungu, nakama hakuna Mungu hao watoto kwanini wafe kwanini duniani kuwe na kilio? Na sisi binadamu tumetoka wapi nani ni lazima tufe kwanini tufe..! sasa wakati hakuna Mungu?
Kama hakuna Mungu, hao watoto kufa si kitu cha ajabu.

Wanakufa kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye angeweza kuzuia wasife hayupo.

Hili jambo halina contradiction, halikosi logical consistency.

Ukisema Mungu huyo yupo, halafu kaumba ulimwengu huo unaoachia watoto wafe hivyo, hapo ndipo contradiction inapokuja.

Watu popote tulipotokea (na sijifanyi kwamba najua jibu) naweza kusema hatujatoka kwa Mungu huyo.

Tungetoka kwa Mungu huyo, dunia isingekuwa na mabaya kama ilivyo nayo sasa.

Ni lazima tufe kwa sababu Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote ambaye angetunusuru na kifo hayupo.

Kifo kinaonesha Mungu hayupo, hakioneshi Mungu yupo.

Mungu angekuwepo, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, angetunusuru na kifo.

Hayupo.

Ndiyo maana hatunusuriki na kifo.
 

Mimi na-maintain hoja kwamba hoja iliyoko mezani ni juu ya Jua kuzama katika matope.Hoja za Mungu hayupo, nitazikabili siku nyingine.Hizi hoja kabla ya wewe kuzikopi somewhere, kuna watu wengi wenye akili waliwahi kujiuliza hata ya unavyojiuliza wewe lakini walipatiwa majibu.Mimi nitakujibu, tena na kwa kuongezea na maswali mengine ambayo wewe hata huyajui na wala hujawahi kuyauliza katika kuhoji Metafikizikia ya Mungu.
 
Sawa hakuna Mungu tuambie kuna nini!!??
 
Kuna walimu watakufundisha humo. Kwani humu jamiiforums imekuja yenyewe bila coding?

Walimu ambao wamekuwa attested na Mungu au nani? Mimi namkubali mwalimu mmoja tu naye ni Muhammad kwa sababu yeye alipokea ufunuo tena kwa nguvu sana kiasi cha kuachwa na maumivu mwilini kwa ajili ya hilo.Hao wengine kwangu sio authentic.Na hao wa Youtube, Muhammad alisha sema hakuna mtu mwingine mwenye ukweli zaidi yake.Yeye ndiye alikuwa wa mwisho katika kuwa na ukweli.Sasa hao wa Youtube wana ukweli gani tena? Bila shaka ni wapiga pesa tu.Hawezi kuja mtu mwingine zaidi ya Muhammad kufafanua jambo ambalo Muhammad alishindwa kueleweka.Kama Muhammad alishindwa kueleweka basi ndio tusubirie Kiama hakuna namna tena.
 
Sijawahi kusema kwamba hoja nimeianzisha mimi, nilishawahi kusisitiza hapa kwamba hizi ni classic arguments watu wamejadili tangu enzi za Anselm na Aquinas na kabla yao, sasa sielewi unaposema hoja hizi nimekopi unataka ku prove nini?

Suala si hoja nimekopi au sijakopi, there is nothing new under the sun.

Erasto Mpemba kagundua "The Mpemba Effect" miaka ya sitini, watu wakajua uvumbuzi mpya, kumbe kina Francis Bacon na Aristotle walishaandika hayo mambo miaka maelfu iliyopitahuko.

Soma hapa Mpemba effect - Wikipedia

Hoja ya msingi ni kwamba, wewe unaji contradict.

Unasema unasimamia logical consistency, unapinga Quran kwa sababu haina logical consistency.

Ukiambiwa hata Mungu wa Biblia naye hana logical consistency, unakataa kujibu.

Kwa sababu nia yako si kusimamia logical consistency.

Nia yako ni kushambulia Quran (sistetei Quran, haina logical consistency).

Ungekuwa unasimamia logical consistency kweli, ungejibu tuhuma kwamba hata Biblia haina logical consistency.
 
Duuh inaelekea umejipanga ..ngoja nichukue mirinda nyeusi kwanz [emoji16]
 
Sawa hakuna Mungu tuambie kuna nini!!??
Hilo ni swali ambalo watu wote tunatakiwa tulichunguze, tulipatie jibu.

Kwa sasa, watu wana tabia ya kutoa jibu la "Mungu" kwa maswali yote wasiyojua majibu yake.

Ni aina fulani ya "coping mechanism" kwa watu wasiotaka maswali magumu.

Ndiyo maana mtu akifariki, jibu jepesi sana la kufukia mjadala ni "kazi ya Mungu haina makosa". Tunakimbia uchunguzi zaidi. Inawezekana kifo kimetokana na ajali, uzembe, na hakuna kazi ya Mungu kwa sababu Mungu hayupo.

Maswali ambayo hatuna majibu yake, tuychunguze tujue majibu yake, tuhakiki majibu.

Tusilazimishe jibu la "Mungu" wakati inaonekana wazi kabisa jibu la "Mungu" halina logical consistency na lina contradiction, kwa sababu Mungu hayupo.

Isiwe tabu sana kusema "hapa hatujui jibu, tuchunguze zaidi tujue, ila katika kuchunguza, jibu la Mungu linaonekana si sahihi hapa, kwa sababu halina logical consistency na linaleta contradiction".

Tatizo tunalazimisha jibu la Mungu hata pale inapoonekana wazi kabisa jibu hilo halina logical consistency na lina contradiction na Mungu huyo hayupo.
 
Duuh inaelekea umejipanga ..ngoja nichukue mirinda nyeusi kwanz [emoji16]
Ameshindwa kujibu swali la kwa nini anashambulia uongo wa Quran, halafu anakubali uongo wa Biblia.

Nimemwambia yuko sawa kusema Quran ina uongo (kwa sababu ina uongo kweli) lakini, kama kweli hataki uongo, akubali kwamba hata Biblia nayo ina uongo.

Anakimbia swali hilo.

Kwa sababu nia yake si kukataa uongo.

Nia yake ni kushambulia Quran.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…