Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Kwa nini Mungu wako ajitekenye na kucheka mwenyewe?

Kwa nini awezeshe ugonjwa uwepo na dawa badala ya kukataza ugonjwa usiwezekane kabisa?

Na vipi kuhusu magonjwa ambayo hayana dawa?
Nimekuuliza wewe unieleze reasoning kwa upeo wako ya kuwepo magonjwa na tiba duality hyo imetoka wapi,je unamaelezo ya kisayansi yanayoexplain jambo hilo.

kuhusu magonjwa ya siyokuwa na dawa ni suala la ugunduzi/uvumbuzi tu,kuna magonjwa yanayotibika hivi sasa ambayo miaka 10-100-1000 iliyopita yalikuwa hayatibiki wala kujulikana dawa lakini hivi sasa yanatibika,so usiseme gonjwa halina dawa sema gonjwa halijagundulika dawa yake.kisicho na dawa ni ulemavu tu,lakini hakuna gonjwa lisilokuwa na dawa.
 
Wengine huwa ni mashabiki tu. Maada ikishawekwa hata kama haijui ataingangania ndio maana hawezi leta mfano mwingine tofauti ili kusuport wazo lake

Usifikirie nimekuja kufurahisha genge au kwamba nina kahoja kamoja nimekaolkota huko na kisha kukimbia nako hapa.Kwa taarifa yako unajadiliana na mtu anayemfahamu Muhammad, Kurani na Uislamu kwa kina.Kung'an'gania hoja moja ya Jua kuzama ni kuonyesha uweledi wangu katika mijadala.Siwezi kujadili hili na hapo hapo nikawa nimerukia suala jingine.Mpaka hoja hii ionekane kwamba imejadiliwa exhaustively ndio nitahamia hoja nyingine.
 
Hakushindwa kama aliweza kuumba wa dizaini hii tulionao na complixity/sophistication zake,sasa kwanini kauumba wa dizaini hii Uislamu ndio unakupa jibu wewe mdadisi kuwa kaumba mfumo ukiwa hivi ili awajaribu nyinyi aliewaumba kama mutafuata haki na kutenda wema ama mutakengeuka na kufanya mabaya,then wote mtakufa na kufufuka tena kwakuwa roho ambayo ni energy huwa haifi kwa mujibu wa wanasayansi bali hubadilika au kuhama kutoka kwenye medium moja kwenda nyengine,kwahyo ili kumake sense ya haya yanayoendelea lazima uamini kwanza kuwa kuna kufufuliwa ambapo wema watakuwa rewarded na wabaya wataadhibiwa na kisha wale waliodhulumiwa watalipwa kile walichozulumiwa.
Na ukiniambia huamini kuwa kutakuwa na kufufuliwa nitakujibu kuwa kama ardhi inaweza kuwekwa mbegu ikatoa mti wenye matundo na huoni ajabu kwanini uone ajabu binaadamu kufa,then akafufuka tena.

Kuhusu kwanini watoto wadogo wanakufa bila hatia na watu kuumwa nakuteseka duniani nitakueleza kuwa dunia na mfumo wake mzima ni challenge/mtihani ndio maana hata kutokea kwake kulianza na big bang.ndo maaana ukiwa siberia ama sehemu nyengine yoyote yenye sub zero temperature usipovaa mavazi ya kuzuia baridi utakufa kwa baridi na ukivaa hutakufa kwa baridi,ndio maana hata porini wanyama wanawindwa haijalishi kama aliyewindwa alikuwa mkorofi au la.ndio maaana hata ukilima kuna baadhi ya mazao yatamea na mengine yatakufa.Mungu kaicha dunia ijiendeshe kwa mfumo huo.
Kwa nini Mungu ahitaji kutujaribu kama tutafuata haki, ikiwa aliweza kutuumba tufuate haki tu bila kufanya kisicho haki?

Umeongea kwamba dunia ni mtihani/challenge.

Mwalimu ambaye hana ujuzi wote, uwezo wote na upeno wote akitoa mtihani ili ajue mwanafunzi anajua nini, nitaona sawa.

Mtihani una kazi ya kumfahamisha mwalimu, mwanafunzi wake kaelewa nini.

Huyo Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, anayepanga kila kitu na kujua majibu ya maswali yote, kwa nini aweke mtihani?
 
Unahoji wee Mungu[emoji4] [emoji12]
 
Nimekuuliza wewe unieleze reasoning kwa upeo wako ya kuwepo magonjwa na tiba duality hyo imetoka wapi,je unamaelezo ya kisayansi yanayoexplain jambo hilo.

kuhusu magonjwa ya siyokuwa na dawa ni suala la ugunduzi/uvumbuzi tu,kuna magonjwa yanayotibika hivi sasa ambayo miaka 10-100-1000 iliyopita yalikuwa hayatibiki wala kujulikana dawa lakini hivi sasa yanatibika,so usiseme gonjwa halina dawa sema gonjwa halijagundulika dawa yake.kisicho na dawa ni ulemavu tu,lakini hakuna gonjwa lisilokuwa na dawa.
Kwa nini Mungu karuhusu magonjwa ya bacteria yaue watu kwa miaka mingi kabla dawa haijagundulika?

Pia, huko Africa kwa mfano, kuna magonjwa mengi sana ambayo dawa zimeshagunduliwa lakini hatuna huko, hatuna vifaa vya hospitali, hatuna ujuzi, hatuna umeme hatuna maji.

Mungu huyo kwa nini anatufanyia uchoyo hivyo kwa mambo ambayo yeye hata hayamgharimu shilingi moja?
 
Unahoji wee Mungu[emoji4] [emoji12]
Dhana ya kuwepo huyu Mungu inajipinga. Ina contradiction.

Contradiction inaonesha huyu Mungu hayupo.

Ni habari imetungwa na watu tu.
 
Tuwekee Ushahidi Mungu anaongea na Muhammad!

Pangoni Hira, Muhammad alikuwa peke yake, unafikiria kutakuwa na shahidi gani tena mkuu? Ukilazimisha sana jambo hilo utaletewa Mijusi,Buibui,kenge na Nge tu.
 
Kwa nini Mungu karuhusu magonjwa ya bacteria yaue watu kwa miaka mingi kabla dawa haijagundulika?

Pia, huko Africa kwa mfano, kuna magonjwa mengi sana ambayo dawa zimeshagunduliwa lakini hatuna huko, hatuna vifaa vya hospitali, hatuna ujuzi, hatuna umeme hatuna maji.

Mungu huyo kwa nini anatufanyia uchoyo hivyo kwa mambo ambayo yeye hata hayamgharimu shilingi moja?
mkuu kuuliza maswali wewe peke yako bila kujibu unayoulizwa sio fea.wewe unuelezee logic ya magonjwa kuwapo na tiba zake zikawapo kisayansi hii ikoje?.
 
Mambo ya iman ukiyadiscuss sana utaomekana kituko
 
Kwa nini Mungu ahitaji kutujaribu kama tutafuata haki, ikiwa aliweza kutuumba tufuate haki tu bila kufanya kisicho haki?

Umeongea kwamba dunia ni mtihani/challenge.

Mwalimu ambaye hana ujuzi wote, uwezo wote na upeno wote akitoa mtihani ili ajue mwanafunzi anajua nini, nitaona sawa.

Mtihani una kazi ya kumfahamisha mwalimu, mwanafunzi wake kaelewa nini.

Huyo Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, anayepanga kila kitu na kujua majibu ya maswali yote, kwa nini aweke mtihani?
Nimesema mtihani as in challenge sio mtihani wa darasani.
Unaposema kwanini amefanya hivi na asifanye vile unazungumzia choices zake yeye sio mimi na yeye ndio anajua kwanini kafanya hivyo,kama wewe ulivyochagua kuwa na huyo uliyenaye na sio mwengine.
 
Kokote watakakwenda au kama hakuna wanapokwenda, kumtenganisha mtoto mchanga na mama yake aliyemzaa na anayependa kuwa naye mpaka anakua mtu mzima, kama una uwezo wa kuzuia utenganishi huu, ni ukatili.

Ndiyo maana watu wanasikitika na kulia kwenye misiba.

Swali la msingi hujajibu.

Mungu alishindwa kuumba dunia hi ikiwa haina na haiwezekani kuwa na utenganishwaji huu?
Mkuu taratibu! Fanya hakuna Mungu, nakama hakuna Mungu hao watoto kwanini wafe kwanini duniani kuwe na kilio? Na sisi binadamu tumetoka wapi nani ni lazima tufe kwanini tufe..sasa! wakati hakuna Mungu?
 
Mkuu taratibu! Fanya hakuna Mungu, nakama hakuna Mungu hao watoto kwanini wafe kwanini duniani kuwe na kilio? Na sisi binadamu tumetoka wapi nani ni lazima tufe kwanini tufe..! sasa wakati hakuna Mungu?
Kama hakuna Mungu, hao watoto kufa si kitu cha ajabu.

Wanakufa kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye angeweza kuzuia wasife hayupo.

Hili jambo halina contradiction, halikosi logical consistency.

Ukisema Mungu huyo yupo, halafu kaumba ulimwengu huo unaoachia watoto wafe hivyo, hapo ndipo contradiction inapokuja.

Watu popote tulipotokea (na sijifanyi kwamba najua jibu) naweza kusema hatujatoka kwa Mungu huyo.

Tungetoka kwa Mungu huyo, dunia isingekuwa na mabaya kama ilivyo nayo sasa.

Ni lazima tufe kwa sababu Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote ambaye angetunusuru na kifo hayupo.

Kifo kinaonesha Mungu hayupo, hakioneshi Mungu yupo.

Mungu angekuwepo, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, angetunusuru na kifo.

Hayupo.

Ndiyo maana hatunusuriki na kifo.
 
Hija ya msingi unaikwepa halafu unasema nataka kukutoa katika hoja ya msingi?

Unaelewa kwamba ukishakubali kwamba unatafuta logical consistency, Mungu wa Biblia kashindwa mtihani wa logical consistency na hivyo hutakiwi kumuandama Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency, halafu hapo hapo ukamkubali Mungu wa Biblia ambaye naye hana logical consistency?

Unaelewa hiyo ni contradiction?

Unakataa kula mavi ya muarabu kwa sababu unasema hutaki kula mavi.

Halafu unakula mavi ya Myahudi bila tatizo.

Halafu bado unadai hutaki habari za kula mavi?

Mimi na-maintain hoja kwamba hoja iliyoko mezani ni juu ya Jua kuzama katika matope.Hoja za Mungu hayupo, nitazikabili siku nyingine.Hizi hoja kabla ya wewe kuzikopi somewhere, kuna watu wengi wenye akili waliwahi kujiuliza hata ya unavyojiuliza wewe lakini walipatiwa majibu.Mimi nitakujibu, tena na kwa kuongezea na maswali mengine ambayo wewe hata huyajui na wala hujawahi kuyauliza katika kuhoji Metafikizikia ya Mungu.
 
Kama hakuna Mungu, hao watoto kufa si kitu cha ajabu.

Wanakufa kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye angeweza kuzuia wasife hayupo.

Hili jambo halina contradiction, halikosi logical consistency.

Ukisema Mungu huyo yupo, halafu kaumba ulimwengu huo unaoachia watoto wafe hivyo, hapo ndipo contradiction inapokuja.

Watu popote tulipotokea (na sijifanyi kwamba najua jibu) naweza kusema hatujatoka kwa Mungu huyo.

Tungetoka kwa Mungu huyo, dunia isingekuwa na mabaya kama ilivyo nayo sasa.

Ni lazima tufe kwa sababu Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote ambaye angetunusuru na kifo hayupo.

Kifo kinaonesha Mungu hayupo, hakioneshi Mungu yupo.

Mungu angekuwepo, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, angetunusuru na kifo.

Hayupo.

Ndiyo maana hatunusuriki na kifo.
Sawa hakuna Mungu tuambie kuna nini!!??
 
Kuna walimu watakufundisha humo. Kwani humu jamiiforums imekuja yenyewe bila coding?

Walimu ambao wamekuwa attested na Mungu au nani? Mimi namkubali mwalimu mmoja tu naye ni Muhammad kwa sababu yeye alipokea ufunuo tena kwa nguvu sana kiasi cha kuachwa na maumivu mwilini kwa ajili ya hilo.Hao wengine kwangu sio authentic.Na hao wa Youtube, Muhammad alisha sema hakuna mtu mwingine mwenye ukweli zaidi yake.Yeye ndiye alikuwa wa mwisho katika kuwa na ukweli.Sasa hao wa Youtube wana ukweli gani tena? Bila shaka ni wapiga pesa tu.Hawezi kuja mtu mwingine zaidi ya Muhammad kufafanua jambo ambalo Muhammad alishindwa kueleweka.Kama Muhammad alishindwa kueleweka basi ndio tusubirie Kiama hakuna namna tena.
 
Mmi na-maintain hoja kwamba hoja iliyoko mezani ni juu ya Jua kuzama katika matope.Hoja za Mungu hayupo, nitazikabili siku nyingine.Hizi hoja kabla ya wewe kuzikopi somewhere, kuna watu wengi wenye akili waliwahi kujiuliza hata ya unavyojiuliza wewe lakini walipatiwa majibu.Mimi nitakujibu, tena na kwa kuongezea na maswali mengine ambayo wewe hata huyajui na wala hujawahi kuyauliza katika kuhoji Metafikizikia ya Mungu.
Sijawahi kusema kwamba hoja nimeianzisha mimi, nilishawahi kusisitiza hapa kwamba hizi ni classic arguments watu wamejadili tangu enzi za Anselm na Aquinas na kabla yao, sasa sielewi unaposema hoja hizi nimekopi unataka ku prove nini?

Suala si hoja nimekopi au sijakopi, there is nothing new under the sun.

Erasto Mpemba kagundua "The Mpemba Effect" miaka ya sitini, watu wakajua uvumbuzi mpya, kumbe kina Francis Bacon na Aristotle walishaandika hayo mambo miaka maelfu iliyopitahuko.

Soma hapa Mpemba effect - Wikipedia

Hoja ya msingi ni kwamba, wewe unaji contradict.

Unasema unasimamia logical consistency, unapinga Quran kwa sababu haina logical consistency.

Ukiambiwa hata Mungu wa Biblia naye hana logical consistency, unakataa kujibu.

Kwa sababu nia yako si kusimamia logical consistency.

Nia yako ni kushambulia Quran (sistetei Quran, haina logical consistency).

Ungekuwa unasimamia logical consistency kweli, ungejibu tuhuma kwamba hata Biblia haina logical consistency.
 
Mkuu kaa vizuri sana katika uzi huu kwa maana ukija pupa utakosa mlango wa kutokea! Hapo Mungu anaongeleaje habari za Alexander the Great? Alexander, aongelewe hapo kwa faida ya nani hasa? Mungu alikuwa anamueleza Muhammad habari za Alexander kwa ili Muhammad apate picha gani hasa?

Hivi unafahamu kuwa Alexander the Great aliishi miaka mingi sana kabla ya hata Yesu Kristu kuzaliwa au hata Muhammad?

Mtawala aliyeitwa Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) alikuwa ni mtawala(Mfalme) wa Makedonia (336-323 KK).Makedonia ni eneo la kijiografia na kihistoria katika Peninsula ya Balkani, kusini-mashariki mwa bara la Ulaya.Je,ni lini Muhammad aliwahi kufika Makedonia kabla hajazaliwa hadi akaweza kuona jinsi Alexander alivyoliona Jua likizama katika matope?
Duuh inaelekea umejipanga ..ngoja nichukue mirinda nyeusi kwanz [emoji16]
 
Sawa hakuna Mungu tuambie kuna nini!!??
Hilo ni swali ambalo watu wote tunatakiwa tulichunguze, tulipatie jibu.

Kwa sasa, watu wana tabia ya kutoa jibu la "Mungu" kwa maswali yote wasiyojua majibu yake.

Ni aina fulani ya "coping mechanism" kwa watu wasiotaka maswali magumu.

Ndiyo maana mtu akifariki, jibu jepesi sana la kufukia mjadala ni "kazi ya Mungu haina makosa". Tunakimbia uchunguzi zaidi. Inawezekana kifo kimetokana na ajali, uzembe, na hakuna kazi ya Mungu kwa sababu Mungu hayupo.

Maswali ambayo hatuna majibu yake, tuychunguze tujue majibu yake, tuhakiki majibu.

Tusilazimishe jibu la "Mungu" wakati inaonekana wazi kabisa jibu la "Mungu" halina logical consistency na lina contradiction, kwa sababu Mungu hayupo.

Isiwe tabu sana kusema "hapa hatujui jibu, tuchunguze zaidi tujue, ila katika kuchunguza, jibu la Mungu linaonekana si sahihi hapa, kwa sababu halina logical consistency na linaleta contradiction".

Tatizo tunalazimisha jibu la Mungu hata pale inapoonekana wazi kabisa jibu hilo halina logical consistency na lina contradiction na Mungu huyo hayupo.
 
Duuh inaelekea umejipanga ..ngoja nichukue mirinda nyeusi kwanz [emoji16]
Ameshindwa kujibu swali la kwa nini anashambulia uongo wa Quran, halafu anakubali uongo wa Biblia.

Nimemwambia yuko sawa kusema Quran ina uongo (kwa sababu ina uongo kweli) lakini, kama kweli hataki uongo, akubali kwamba hata Biblia nayo ina uongo.

Anakimbia swali hilo.

Kwa sababu nia yake si kukataa uongo.

Nia yake ni kushambulia Quran.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom