Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.


Umekuja kwa sura yako kamili 😛😛😛
 


Je Mungu Aweza Kufa?


Tukiendelea na dhana yenye kutatanisha kwamba Mungu wa Wakristo anaweza tu kusamehe dhambi ndogo kwa kusababisha dhambi kubwa - dhambi ya kumtoa Yesu ili auliwe - dhambi ya kuua, tunalazimika kujadili mada ya uungu ili tuweze kuijadili mada hii. Mungu ni wa milele, alikuwepo tangu na tangu na atakuwepo milele na milele: Hakuumbwa; Hawezikufa; n.k.


Kama Yesu ni mtoto wa Mungu, kama wakristo wanavyodai, hii ingemfanya na yeye kuwa Mungu pia, ingewezekanaje yeye, kama Mungu, afe msalabani kama wanavyodai?


Ikiwa "mwili wake wa ubinadamu" ndio ulikufa, hii italeta maana kwamba alikufa kama mtu mwingine yeyote.

Na kama ni hivi - imani yote ya kuwa Yesu aliteswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanaadamu, itakuwa haina msingi wowote - kwani damu ya mtu wa kawaida haiwezi kuwa fidia ya dhambi za mtu mwingine.
 
Allah hajui jua hahaha my gosh allah wa wakoreshi kama idol tu hajui lolote

Anajua hili

Athari za Upagani Katika Imani Ambazo
Paulo Aliziingiza Katika Ukristo


Paulo hakuielewa maana halisi ya kafara zilizokuwa zikitekelezwa na Wayahudi katika Agano la Kale; waliteketeza kafara hizi kama shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutokana na rehema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu aliwajaalia - na sio kwa ajili ya kuhakikishiwa msamaha wa Mwenyezi Mungu kutokana na madhambi yao.


Karibu dini zote za kipagani zinaamini kwamba kafara wanazozitoa kwa miungu yao ni kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi yao. Mimea, wanyama na hata watu waliuawa ili kuwa na uhakika ya "rehema ya Mwenyezi Mungu".


Sio hivyo tu bali karibu wafuasi wa dini zote za kipagani huchukua vyakula hasa mikate na pombe, vinavyokuwa vimetengwa kwa ajili ya sadaka kwa miungu. Wapagani waliamini kwamba kwa kula vyakula hivi vilivyotengwa kwa ajili ya miungu, wao pia (wapagani) walikuwa wanapata baadhi ya sifa na nguvu za kimungu - roho za miungu hao ziliingia na kuishi ndani yao (hao wapagani).


Paulo alichukua imani hii akaiingiza katika Ukristo, akaiita kuwa ni "Sakramenti ya chakula cha Bwana au Ekaristi". Kwa sababu inachukuliwa kuwa ni sehemu kubwa ya imani ya kuteswa na kufa kwa Yesu. Mfumo na tendo hili la Ekaristi umekuwa ni moja wa Sakramenti muhimu kabisa katika Ukristo kwa sababu ni alama na ukumbusho wa tendo la Yesu kutoa mwili na damu yake kama kafara na fidia ya dhambi za mwanadamu.


Imani hii ambayo Paulo aliingiza katika Ukristo kutoka kwenye upagani ilimrahisishia sana kazi.

Kwa hadhira yake - watu wa mataifa hawakuona taabu yeyote kuingia katika ukristo kwani imani ya Mungu kufa akiwa kijana na baadaye kuwa hai kuwaokoa watu wake ili kuwepo katika imani zao za kipagani.

Ikiwa miungu wao akina Adonis au Mithran waliwahi kufanya kitu cha aina hii kwa ajili yao kwanini Yesu ashindwe kulifanya hilo sasa hivi?
 
Allah hajui jua hahaha my gosh allah wa wakoreshi kama idol tu hajui lolote

Paulo Alifanikiwa Kitu Gani?


Watu wa mataifa kwa mara nyingine tena walifarijiwa: walikuwa na waokozi katika dini zao za zamani za kipagani, na mara hii tena, Paulo aliwapa mwokozi mmoja katika imani yao mpya ya Ukristo.

Aliwaambia kwamba walichokuwa wanatakiwa kukifanya ili kuwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao ni kuamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao, hilo tu ndilo walilotakiwa kulifanya.


Katika sheria ya Kiyahudi, mambo muhimu katika kafara au fidia kwa ajili ya madhambi ni Rehema ya Mwenyezi Mungu, toba na jitihada za dhati katika kufanya mambo ya kheri; kafara ya damu haikuhitajika.

Katika jitihada zake za kuwapata watu wa mataifa, Paulo alilitafsiri upya Agano la kale na akawapa Wakristo wapya mwokozi wao - mtu ambaye huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine.

Imani yake ya kuteswa na kufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za wanadamu - aliyoiingiza katika ukristo, imekuwa ni tatizo kubwa kwa Wakristo kuielezea ikaeleweka, baada ya kuona jambo zima linatatanisha wakati nguvu za hoja na akili zinapojaribu kufurukuta na kutaka kutumika.
 
Allah hajui jua hahaha my gosh allah wa wakoreshi kama idol tu hajui lolote
Ahahahahahaahahahahahahaha kama Bwana asivyojua kuwa Nyoka ali vumbi
MWANZO 3:14
"Bwana Mungu akamwambia nyoka, kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote, na MAVUMBI utakula siku zote za maisha yako"
Ahahahhahahahahhahhahahajjajahajajaja toka lini nyoka akala vumbi ahahahhaahahahahqhqqhqqhah ndio maana mnasema alivuliwa nguo huyo watu wakamuacha na kakaptula amejikunyata baridi
 
Kama mpaka sasa bado kuna mtu anaamini yesu alisulubiwa ili yeye apate uokovu bila shaka atakuwa na tatizo la akili " Haki yake mwenye haki, uovu wake mwenye uovu"
Ahahahhahaahahahaha nyie endeleeni kumfanya yesu mpira wa kona mnamgombania
 
TUMFAHAMU AL LAH.

Here’s a quick and easy study in Qur'an 4:125:

In Qur’an 4:125,
there are two words for Allah, but they do not have the same meaning.

Kwa WANAOJUA KIARABU TU.

Allah and Lil away from Lillah, that leaves us with lah (god), a word that is common to both names.

LAH ni Jina la.Mungu Mwezi(moongod)
Wa kimisri na aliyeabudiwa na Waarabu.

Kwa kingereza, 'Lillah' linatafsiriwa TO THE GOD.

Kama Uonavyo Lillah and Allah yote ni majina ya Kiarabu yanaandikwa kama.Neno Moja. Lakini ni vipande vya maneno mawili tofauti.

Lil and Al si sehemu ya Neno 'LAH'.

— Lillah na Allah yameundwa na maneno mawili.
Lillah ikimaanisha "to god"
Allah ikimaanisha "the god".


In Arabic, Al = “the”
Na inaunganishwa na majina yale yanayoelekezwa kwa Mungu tu.

Ndio maana majina yote 99 ya Allah yanaanza na "Al"or "the".




Take note however, that “the” is not part of the name. It is just a language tool used to indicate that the name is unique to god; only god can be given this.

Kwa mfano. Kwa Kiarabu huwezi tamka "The Muhammad,” [emoji777]
Kwasababu Muhammad ni Jina la Mtu.

Zingatia hata miungu ya kike ya Mecca ni
Al-Lat and Al-'Uza ina.fanana sana na Allah kwakua yote huanza na Al..kwakua ni miungu.

AJABU NI KUA MESSIAH ANAITWA
Al-MESSIAH ndani ya Quran.[emoji23] [emoji123] .
Kwasababu ndio Messiah peke yake ulimwenguni.
Na ndio binadamu pekee ndani ya Quran mwenye Al au "the" imeunganishwa kwenye jina lake.
 
Hayo ni mambo ya kuzusha kutoka kwa mzushi Paulo
 



Dhana ya Dhambi ya Asili


Imani ya ukristo juu ya dhambi ya asili haina nafasi yoyote katika Uislamu, kwani Waislamu wanaamini kwamba mwanadamu huzaliwa akiwa hana dhambi yoyote. Ndani ya Quran, Mwenyezi Mungu anasema:


"Uelekeze uso wako katika dini iliyokuwa sawa ambayo Allah amemuumbia mwanadamu, ambayo inawiana na maumbile ya mwanaadamu". (Quran 30.30)


Aya hii inatueleza kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu katika umbile zuri kabisa, na akiwa ni twahiir, asiyekuwa na dhambi lolote; na kwamba umbile lake lilikuwa linamwongoza kutii na kuinyenyekea sheria ya Mwenyezi Mungu.

Dhambi hairithiwi: ni kitu ambacho mwanaadamu hujiletea mwenyewe anapofanya jambo ambalo hakutakiwa kulifanya au anapoacha kufanya jambo ambalo alitakiwa kulifanya.

Kusema kwamba kila mmoja wetu huja duniani anapozaliwa akiwa na mzigo wa dhambi iliyofanywa na babu yake wa nyuma kabisa huko itakuwa si chochote isipokuwa ni kukana sifa ya Mwenyezi Mungu ya uadilifu na rehema yake.


Ingawa Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu uhuru wa kuchagua na kufanya mambo anayoyapata hapa duniani, mwanaadamu ni kiumbe mwenye mfumo maalumu na mwenye asili na uwezo maalum.

Mwanadamu atalipwa au kuadhibiwa kwa lile alilofanya yeye mwenyewe, si kwa lile lililofanywa na ndugu yake wa zamani huko.

Matendo yetu wenyewe ndiyo yatakayoangaliwa siku ya hukumu na katika muda wa uhai wetu, Mwenyezi Mungu hutupatia kila nafasi inayowezekana ili tuweze kufanikiwa na Mwenyezi Mungu si mwenye kutudhulumu, mwenye kututwisha mzigo wa dhambi ambazo hatukuzifanya.

Kwa hiyo ni sisi wenyewe ndio tutakaoitengeneza au kuiharibu hatima yetu hapa duniani na kesho huko akhera.


Hii ni kwa sababu Waislamu wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam, kosa lake la kutotii amri ya Mwenyezi Mungu.


"Kisha Iblis aliwatekelezesha (wakala tunda katika ule mti) katika Bustani, na akawatoa katika ile hali waliyokuwa nayo -- kisha Adam akafunuliwa kuwa anatakiwa atubu, alipotubu Mwenyezi Mungu alimsamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwingi kusamehe, Mwingi wa Rehema". (Quran 2:36-37)


Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam, na vilevile alimuondolea aibu na alamu ya kutorehemewa ambayo wakristo wanadai kuwa inarithiwa na wanadamu wote tokea wakati huo wa Adamu mpaka leo na watakaondelea kuzaliwa.
 


Kifo Cha Yesu


Kuhusiana na suala la kifo cha Yesu msalabani - ingawa ni wazi kwamba Yesu, kama alivyokuwa kwa mitume wengine kabla yake, walipatwa na masaibu makubwa kwa sababu ya kujaribu kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu ambao hawakuonyesha nia na ari ya kuupokea.

Na alikuwa anajua vizuri kwamba hili lingemtokea, hata hivyo hakufikia kiwango cha kuuliwa na hususan kuuliwa kulikopangwa na Mungu - kama ilivyodai Paulo baadaye, yaani kuuliwa ili kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.


Katika Bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa unyenyekevu na shauku kwa Mwenyezi Mungu kuwa "kikombe kinipite" (Mathayo 26:39), ambapo kikombe hiki kinamaanisha kukamatwa na kufa kwake. Hivi kweli tunaamini kwamba mja mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu anaweza kuomba rehema akanyimwa?


Wazo zima la kuteswa na kufa kwa Yesu msalabani ili awe kafara ya dhambi za wanadamu halikubaliani na hoja za kiakili na mantiki linapohusishwa na Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu.

Je inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mwadilifu kwa kiwango cha juu kabisa akakataa kumsamehe Adam - na kizazi chake baada yake kwa ajili ya dhambi lake tu (Adam) - mpaka Yesu aje?

Je inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake akataka na kuruhusu kudhalilishwa na kuuwawa kwa mmoja wa mitume wake aliyekuwa mnyenyekevu na mtii sana kwake?

Je inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake afe kwa ajili ya dhambi za watu wengine? Katika Uislam, hatudhani kuwa hili linawezekana.


Tukiliangalia hili kutokana na mtazamo wa upendo Mwenyezi Mungu, hoja zile zile zinatajitokeza kuhusiana na uadilifuwa Mwenyezi Mungu: Je Mungu mwenye upendo mkubwa kwa waja wake angewaadhibu wanaadam wote bila kuja Yesu?

Je Mwenyezi Mungu mwendo upendo mkubwa kwa waja wake angehitaji kuwa ni lazima mmoja wa waja wake wema na waaminifu (Yesu) adhalilishwe na kuuawa ili awasamehe wanadamu madhambi yao? Yeyote na kila mtu anaweza kushangaa na kujiuliza hii ni AINA gani ya upendo wa Mungu unaoweza kudai kiasi cha gharama kikubwa kiasi hicho na cha kutisha namna hii.


Uislam unashikilia kwa nguvu msimamo kwamba kila mtu anawajibika kwa vitendo vyake: kila mtu ataadhibiwa kwa maovu yake. Haiingii akilini kwamba Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu anaweza kumuadhibu mtu kwa dhambi alizofanya mtu mwingine.


"Kila nafsi italipwa kutokana na matendo yake na nafsi haitaulizwa juu ya matendo ya nafsi nyingine". (Quran 6:164)


Hakuna mtu anayeweza au atakaye adhibiwa kwa dhambi za mtu mwingine.

Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba kila mmoja wetu atalipwa au kuadhibiwa kutokana na aliyoyafanya yeye mwenyewe katika maisha yake.


"Na Mwenyezi Mungu hamtwishi yeyote mzigo mkubwa kuliko ule anaoweza kuubeba. Kila jema nafsi inalolifanya ni kwa faida yake, kila uovu inaoufanya ni kwa hasara yake." (Quran 2:286)
 
Ndio nini unatufundisha kiarabu? au unajadili Muundo wa lugha ahahahahahahhhajajaja hapa tunajadili maandiko sio muundo wa lugha , leta nukuu ya sura 4 :125 kama kuna jambo ujalielewa tukufundishe, kuhusu masiha QURAN ilishaweka wazi kabisa ni mtu tena alikua akienda chooni ana hata harufu ya Uungu
 
Vijana unawapa dozi nzito wanaanza kutufundisha kiarabu ahahahaa
 
Musa alikuwa nabii na alishiriki katika kufanikisha mambo ya kivita huyo ni muongo, hata samweli alikuwa nabii ndio alimpaka mafuta sauli kuwa mfalme wa Israel kwa amri ya Bwana na yeye ndio alimletea sauli amri kutoka kwa Mungu aende AKAWAANGAMIZE waamaleki, na sauli alipomwacha hai mfalme Agagi Samweli aliingia kumkata kata mapanga mfalme Agagi kama Bwana alivyoamuru, yaani mkitaka kukataa vita labda mchome vitabu vitabu , hata Israel Mungu wenu alikosa alternative ya kuwapa waisrael mpaka kwa vita ndio iliwezekana
 
Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda sio kumbebesha yesu zigo la misumari ahahhaahahahaahaaaahahua starehe upate wewe mimba abebe jirani
 

Mtumishi hawa makafir [emoji117] wamesha ivaa laana [emoji117] wanacho kifanya ni wazimu wa maswali[emoji117] na sababu kubwa hawana Elimu ya Roho [emoji117] na Hawajui kusoma [emoji117] na mwalimu wao kafa anasikitika [emoji117] ndio sababu wanaokota okota okota mizizi pori wakiona dawa kumbe sumu [emoji12]
 

Attachments

  • IMG_20180916_191007_774.jpg
    14.6 KB · Views: 21
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…