Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
scrolls ni kurasa chache tu mfano labda zile amri kumi za mungu kama mussa angepewa zile tu tungesema pale kapewa kitabu?ila pale ingekua kapewa scrolls
Weka tofauti ya kitabu na Scroll nione
 
Adam ndie nabii wa Kwanza?
Alipewa kitabu gani?


Kuwa mtume au nabii si lazima upewe kitabu.

Na tofauti ya mtume na nabii ni kubwa sana. Kwa ufupi "Kila mtume ni nabii lakini si kila nabii ni mtume".

Kumepita mitume wengi hali kadhalika manabii wengi. Lakini waliopewa vitabu ni :

1.Muhammad
2.Issa
3. Musa
4.Daudi

Pia kulikwa na misahafu yaani nakala za Ibrahim na Mussa.

Allaha ndio anajua zaidi.
 
Mkuu, mitume na manabii Mungu aliwapa utume au unabii kwa mpangilio uliwazi na unao eleweka, lakini kwa Mud nitofauti! Why kwa mud kuwe tofauti?
 
Kuna tofauti gani ya kitabu na Scrolls?
Kitabu ni collection of sheet wakat scroll ni huwa ni kama bandiko ambalo halija-contain mambo mengi, kusoma lazima ulikunjue na ukimaliza unalikunja kama atlas
 
Upo sahihi kabisa hujakosea hata nukta.... hiyo surat Kahf imejaa code sana ni hadithi ya matukio matatu tofauti... mwenzetu badala ya kuuliza maana anakuja na shutma.... inashangaza sana.
Mkuu inaposema imejaa code unakua unamaanisha nini?
 
Kama hakupewa kitabu Watu wake walimjua vipi Mungu na miongozo.?
Nayeye aliutoa wap unabii
 
Weka tofauti ya kitabu na Scroll nione
hi hivi nikichomoa kurasa nne za kitabu fulani halafu nikaziweka upande wa kushoto na na kitabu chenyewe nikakiweka upande wa kulia

hapo sasa upande wa kulia nitakua nina kitabu na upande wa kushoto nitakua na kurasa(scrolls) tu na sio kitabu,unaweza ukajaribu hata hapo kwako chana kurasa chache weka pembeni na kitabu chenyewe weka pembeni hapo utaona utofauti wake mubashara kabisa

uisahau kuleta picha ukifanya hivyo
 
Mkuu, mitume na manabii Mungu aliwapa utume au unabii kwa mpangilio uliwazi na unao eleweka, lakini kwa Mud nitofauti! Why kwa mud kuwe tofauti?
utofauti upo wapi unao uona wewe?

na ukumbuke mungu anafanya atakavyo yeye na haojiwi kwa matendo yake
 
Fact niliyo prove ni kwamba dhana ambayo inajipinga yenyewe haiwezi kusimama kama ukweli.

Mfano. Kama pembetatu na duara ni maumbo tofauti katika Euclidean geometry planes, duara lina nyuzi 360 na pembetatu ina nyuzi 180, hakuwezi kuwepo pembetatu ambayo hapohapo ni duara katika Euclidean geometry.

Hiyo ni contradiction. Hilo umbo la kufikirika la "pembetatu duara" halipo. Halina logical consistency.

Vivyo hivyo, huyo Mungu wenu ambaye upande mmoja mnasema ana uwezo wote, ujuzi wote, ujuzi wote na upendo wote na upande mwingine kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, ilhali aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kutokea, ni contradiction.

Mungu huyo hana logical consistency.

Kusema Mungu huyo yupo ni sawa na kusema kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidean geometry planes.

Haya ni mambo ambayo nayaelewa na kuyakubali ma sisemi kwa sababu mtu mwingine kaandika.
 


Qur'an imesema hivyo ndio kwamba kuna watu wapigwa mihuri na vizibo kwenye masikio,mionyo. Sasa swali la msingi nakuuliza wewe. Je unawajuwa hao watu ? Na je unaweza kuniletea ushahidi kwamba huyu amepigwa muhuri na kuwekewa vizibo masikioni ?

Kama hujaelewa usilize swali kwanza.

Cha msingi kila mtu atimize wajibu wake,na kutii sheria.
 
kwanza mimi siamini hiyo sijui " nini Quran" so muda WA kuchnguza hao watu sina " kinachoshangaza ni mungu kwenda kuwachoma moto watu ambao yeye mwenyew ndiye aliyewafunga masikio na mioyo yao",una muadhibu mtu ambaye wewe mwenyewe ndiye uliyechangia asiweze kukufuata " sasa huo siuonevu mkuu..??
 
Sipingi wewe kukubaliana nayo nacho kuuliza je unahakika nayo? Na unahakika nayo kwa uhakika upi wa kujiridhisha au your still follower
 
Kuna mtu kashathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote yupo?
 
utofauti upo wapi unao uona wewe?

na ukumbuke mungu anafanya atakavyo yeye na haojiwi kwa matendo yake
Wahyi (ufunuo) uliokuja kwa Muhammad alisikia makengele,uso kuwa mwekundu,jasho kumtoka. Katika Bukhar, Hadithi na 2, Juzuu na 1,Al-Lu’lu Kitabu cha 3.Uk. Na.874 Hadithi na 1505 “Hadithi ya Aisha r.a mama wa waumini amesema, kuwa Al Harith ibn Hisham r.a alimuuliza mtume wa Allah s.a.w ‘ Ewe mtume wa Allah hivi wahyi (ufunuo) hukujia vipi?’ mtume wa Allah s.a.w akajibu, “ Wakati mwingine hunijia kama mlio wa kengele, na aina hiyo ndiyo ngumu zaidi kwangu, inaondolewa hali hiyo kwangu wakati tayari nimeshapata wahyi. Na nyakati nyengine malaika anakuja kwangu akiwa katika mfano wa mtu, kwa hiyo ananieleza na ninayazingatia aliyoyasema.” Aisha r.a alisema , Na hakika nilimwona unamshukia wahyi siku ya baridi kali na ilipomuondoka hali hiyo, paji lake la uso lilichuruzika jasho.”
 
Sipingi wewe kukubaliana nayo nacho kuuliza je unahakika nayo? Na unahakika nayo kwa uhakika upi wa kujiridhisha au your still follower
Nina uhakika kama wewe ulivyokuwa na uhakika kwamba swali lako linatakiwa kujibiwa na jibu ukaniuliza swali hili.

It is a matter of simple logic.

Wewe una uhakika Mungu yupo na unaweza kuthibitisha hilo kwa namna ambayo haipingiki kimantiki?
 
siamini hadithi mkuu labda iwe imeendana sawa sawa na quran,vinginevyo sitaiamini kabisa maana hadithi nyingi zimechakachuliwa
 
Nina uhakika kama wewe ulivyokuwa na uhakika kwamba swali lako linatakiwa kujibiwa na jibu ukaniuliza swali hili.

It is a matter of simple logic.

Wewe una uhakika Mungu yupo na unaweza kuthibitisha hilo kwa namna ambayo haipingiki kimantiki?
JIBU LANGU: Kudhibitisha kitu ni kwa kuona, kugusa, kusikia, kuonja na kunusa.
SWALI LANGU: Je kuna njia ingine ya kudhibitisha kitu tofauti na hizo tajwa hapo juu?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…