una mpangia Mungu cha kufanya? ww unayo yafanya anakupangia nan?
Hapana. Simpangii. Naonesha kwamba hana logical consistency.
Mnasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Mnasema Mungu kaumba mbingu na dunia na watu.
Hivyo mfumo mzima wa DNA unavyohifadhi habari na ubongo unavyofanya kazi aliujua.
Angeweza kuweka habari zake zote kwenye DNA na ubongo.
Kwa sababu.
1. Uwezo wa kufanya hivyo alikuwa nao. Mnasema ana uwezo wote.
2. Ujuzi wa kufanya hivyo alikuwa nao. Mnasema ana ujuzi wote.
3. Upendo wa kufanya hivyo anao. Mnasema ana upendo wote.
Kufanya hivyo kungeturahisishia kazi kwa kutuwezesha kumjua Mungu moja kwa moja bila kutegemea msahafu, tafsiri na fasiri zenye utata mwingi sana.
Mungu mwenye upendo angetusaidia sana sisi tunaobisha uwepo wake kama angeweka habari zake wazi hivyo katika namna ambayo haibishiki.
Kwa nini hakufanya hivyo?
Kutokufanya hivyo kuna contradict habari za kwamba ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Simpangii cha kufanaya. Nauliza tu kwa nini hakufanya jambo linaloonekana bora, la heri, jema, ambalo lingetuepusha watu wake na migogoro mingi sana ya tafsiri.
Kwa nini hakufanya hivyo?