Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
una mpangia Mungu cha kufanya? ww unayo yafanya anakupangia nan?
 
Hujajibu swali.

Kama unafikiri umejibu, weka numuu hapa.

Vinginevyo unakubali unakimbia swali kwa sababu huwezi kulijibu.

Kwa sababu huyo Mungu hayupo
 
Thibitisha hiyo logical consistency ndio njia bora ya kuthibitisha dai lako la uwepo wa mungu? na huo mfano wako alieua ndio anajua njia bora na ukitaka atakuthibitishia wacha kurukaruka thibitisha
 
Tufute aya kwa uelewaka mbovu unashindikwa kufasiri aya unatuletea habari za kuokota
 
una mpangia Mungu cha kufanya? ww unayo yafanya anakupangia nan?
Hapana. Simpangii. Naonesha kwamba hana logical consistency.

Mnasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Mnasema Mungu kaumba mbingu na dunia na watu.

Hivyo mfumo mzima wa DNA unavyohifadhi habari na ubongo unavyofanya kazi aliujua.

Angeweza kuweka habari zake zote kwenye DNA na ubongo.

Kwa sababu.

1. Uwezo wa kufanya hivyo alikuwa nao. Mnasema ana uwezo wote.
2. Ujuzi wa kufanya hivyo alikuwa nao. Mnasema ana ujuzi wote.
3. Upendo wa kufanya hivyo anao. Mnasema ana upendo wote.

Kufanya hivyo kungeturahisishia kazi kwa kutuwezesha kumjua Mungu moja kwa moja bila kutegemea msahafu, tafsiri na fasiri zenye utata mwingi sana.

Mungu mwenye upendo angetusaidia sana sisi tunaobisha uwepo wake kama angeweka habari zake wazi hivyo katika namna ambayo haibishiki.

Kwa nini hakufanya hivyo?

Kutokufanya hivyo kuna contradict habari za kwamba ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Simpangii cha kufanaya. Nauliza tu kwa nini hakufanya jambo linaloonekana bora, la heri, jema, ambalo lingetuepusha watu wake na migogoro mingi sana ya tafsiri.

Kwa nini hakufanya hivyo?
 
Unajua utume wa Mud ulianzia wapi?

Kaka mtu hata kama humpendi jaribu kumfanyia uadilifu na kumuheshimu pia.

Kitendo cha kumuita mtume wetu "Mud" ni utovu wa adabu na si kitendo kizuri.

Sisi huyu ni mtume wetu tunampenda kweli kweli,tunamfata yeye na kumuadhimisha pia amani ya Allah iwe juu yake.

Huwa sipendi sana kujadiliana mijadala ya dini kwa kuchelea watu kama nyinyi huenda ukamtukaan kipenzi chetu na kumkosea adabu kama ufanyavyo wewe.

Mtume wetu aliudhiwa tangu alipokuwa hai na aliudhiwa pia baada ya kufa kwake,bali mpaka leo anaudhiwa.

Hala hala kaka ! Tuchunge heshima za watu.

Utume wa Muhammad amani ya Allah iwe juu yake ulianza alipotimiza miaka 40.
 
Mkuu tulia mm nitakwenda nae sawa nijue akili yake inaishia wap
 
Niwie radhi mkuu.
 
Wapi? Weka nukuu yako ulipoimaliza hapa.


Hiyo si kazi yangu. Inaonyesha unafuta sana kumbukumbu,wewe katika ile Elimu ya Rijali habari zako zisingekuwa zinachukuliwa.
 
Toa utaratibu wa kupewa utume unaoeleweka mbona tena unakimbiakimbia
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea, akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena; “soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia; “soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake. Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.

Mara, yule mtu (Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia” Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
 
Hiyo si kazi yangu. Inaonyesha unafuta sana kumbukumbu,wewe katika ile Elimu ya Rijali habari zako zisingekuwa zinachukuliwa.
Hapana. Inaonesha unalazimisha kumbukumbu ambazo hazipo ziwepo.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Acha kulazimisha mambo.

Kamanunabusha weka post hapa tuone.

Huwezi kuweka. Kwa sababu hiyo post haipo. Kama ambavyo huyo Mungu hayupo.

Acha kuishi kwa maruweruwe.
 


Vizuri.
 
Tatizo lako lipo wap hapo kwenye hayo maelezo uliyocopy?eleza tukusaidie
 
Sasa kama ni beyond our tiny capabilities kuelewa, hii Quran imeandikwa ili nani aielewe? Au ameandikiwa nani?
Historia ya Kanisa yaonyesha zamani biblia haikusomwa na kila mtu wadhani kwa nini?
Kwa nini mtu anasoma mpaka PhD ili kuwa Padre na kuweza kuhubiri 'injili' kwa usahihi na sio wewe tiny brain?
Hii sio riwaya ndio maana kuna Maulamaa na Maamuma ,Walimu naWanafunzi
Fanya mazoezi ya ubongo utaelewa tuu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…