umeuaje kama kadi ya klinikia bila kuisoma?
Usipotoshe maana halisi ya Aya hizo za Quraan ambayo ni maelezo kuhusu kisa cha vijana wawili walio lala ndani ya cave na kuamka baada ya generation mpya kuzaliwa mahali hapo.
Unajaribu kupotosha maneno ya Allah ili kujipa tamaa kuwa uko sahihi na ukafiri wako.
Jua kuzama , kutua au kuchomoza hotokea magharibi na mashariki ya dunia. Hili limewekwa wazi na Quraan tukufu.
Kama hujui maana ya lugha jifundishe lakini usipotoshe kwa kujifurahisha kupotoka.
Mimi hapa ninapokaa jua huzama nyuma ya nyumba yangu na linainhia baharini ! Na huchomoza Alfajiri upande wa mashariki kutoka kwenye magorofa! Jee maana yake hilo jua linatoka kwenye magorofa na kutokomea baharini !
Kusema hivo ni kujaribu kuonesha upande gani jua lina zama na kutua
Elimu haina kikwazo jaribu kujifunza upate kuelimika . Ujinga ni wa kujitakia hasa unapokubali za kuambiwa tu bila na kuchanganya na za kwako
Tafsiri kwa kiswahili kinacholekea ya aya hizo uliozitaja
85. Kwa kutumia njia hizo aliweza kueneza madaraka yake katika ardhi, na akafuata njia mpaka akafika huko magharibi kunako kuchwa jua.
* 86. Akenda mpaka akafika pahala mbali huko upande wa magharibi, akalikuta jua kwa linavyo onekana kwa macho kama kwamba linazama pahala penye chemchem ya maji ya moto na matope meusi. Na karibu ya chemchem hii Dhul- Qarnaini aliwakuta watu makafiri. Mwenyezi Mungu akamtia moyoni mwake afanye mojapo ya mambo mawili: Ama awaite kwenye Imani, na hili kwa hakika ni jambo zuri; au awapige vita ikiwa hawakuitikia wito wa Imani.
* 87. Dhul-Qarnaini akawatangazia: Katika wao aliye jidhulumu nafsi yake kwa kubakia katika ushirikina, basi amestahiki adhabu ya duniani kutokana naye, na kisha atarejea kwa Mola wake Mlezi. Naye atamuadhibu adhabu kali wasio ijua.
siamini hadithi mkuu labda iwe imeendana sawa sawa na quran,vinginevyo sitaiamini kabisa maana hadithi nyingi zimechakachuliwa
Mleta mada Amani iwe nawe.
Katika suratul Kahfi aya ulizozinukuu kuhusu Dhul Qarnayn na kuzama kwa jua kwenye Chemchem yenye matope meusi. Ili uweze kuielewa hiyo aya na Qur'an kwa ujumla wake kuna mambo inabidi uyafahamu. Ulichokinukuu wewe ni Fasiri INA maana kwa hali ile iliyoandikwa kwa Kiarabu umeipeleka kwa Kiswahili. Vilevile kuna tafasiri kwa maana kilichoandikwa kinaelezewa kwa undani ili upate mantiki nzima na uelewe kile kinachokusudiwa.
Tukirudi katika hiyo aya inaanza kwa "Wanakuuliza habari za Dhulqarnayn. Sema; kwa yakini nitawasomea katika hadithi yake".
Na wanakuuliza, kwa maana Mtume anaulizwa, ni akina nani wanauliza habari za Dhul- Qaryn? Hii hoja itajibu swali lako linalouliza ni nani huyu mtu, Dhul Qarnayn?
Maqurayshi wa Makkah waliambiwa na Wayahudi wa Madinah, wakamuulize Mtume maswali 3 na nia ni kutaka kupima kama kweli Muhammad ni Mtume ama laa. Maswali yalikuwa ni kuhusu Roho, kuhusu Dhul Qarnayn na ahlul kahf(watu wa mapangoni) ambayo imebeba jina la Sura. Kwa sababu hakuna hayo mambo anayeyajua isipokuwa ni mitume tu, na hizo habari za hayo maswali 3 yalikuwepo katika vitabu vya watoto wa Israel. Kuhusu Dhul Qarnayn katika Qur'an tumepewa habari yake kidogo tu kama aya inavyosema "kwa yakini nitawasomea katika( baadhi) hadithi yake. Huyu mtu, Dhul Qarnayn alikuwa ni mtumishi( Mfalme) aliyetawala na kueneza sheria ya Mungu. Alikuwa mshindi mkuu wa vita. Alisafiri yeye pamoja na jeshi lake kuelekea sehemu tatu(3) za Dunia, magharibi ya mbali ya Dunia, mashariki ya mbali ya Dunia na mwishoni kaskazini mwake mwa Dunia. Alikwenda upande wa magharibi na akashinda vita sana mpaka alipofika mahali akaona jua linatua ndani ya chemchem ya maji yaliyovurugika.
Aya inayoendelea inasema "bila shaka tulimwamrisha katika ardhi na tukampa njia za kupatia kila kitu", kwa maana mradi wake ni kila kitu kilichohitajiwa kwa kumalizia kazi yake Mungu alimpatia huo uwezo. Maneno haya, akaliona Jua linatua katika chemchem iliyovirugika, tafsiri yake ni hii; kwa maana mahali alipofika maji yake yalikuwa mapana sana yaani bahari, Hata inakuwa ukisimama pwani wakati wa magharibi jua linaonekana linatua ndani ya bahri. Ukiwa pwani ukiangalia kuzama kwa jua unaona kama linatua kwenye tope au chemchem iliyovurugika. Ndivyo Dhul Qarnayn alivyoona na ndivyo Qur'an inavyoelezea kama Dhul Qarnayn alivyoona na hiyo bahari kuzama kwa jua na akaona hiyo hali ni bahari Nyeusi iliyoko Asia minor.
Watu wanatafsiri Qur'an kwa kusoma maneno yaliyofasiriwa kwa lugha mama( Kiarabu) na kwenda lugha nyenginezo wakidhani kwamba tafsiri yake ndiyo IPO hivyo hivyo hapana, Qur'an ina somo kabisa LA tafsiri yake.
Kuhusu Jua tangu kale INA njia yake. Kwenye Qur'an suratul Anbiyaa aya 33 na Suratul Yaasin aya ya 38 zinaelezea Jua na Mwezi zina njia sake(orbits) zinazopitia. Na si kama baadhi ya watu wanajaribu kufananisha na Sura ya Al Kahfi kuhusu Dhul Qarnayn. Kuhusu jua ndilo linalozunguka badala ya Dunia hili ntakujibu baadae utanisamehe afya yangu imetetereka kidogo tangu Jana kwa hiyo sipo vizuri sana.
Kaka kuchunga adabu za kielimu,naomba ukiri ya kuwa umeandika maneno ya uongo,tena ukiri ya kuwa ulikurupushwa na hisia ndio maana ukaandika uongo huu. Hisia zenyewe zilizo kukurupusha ni hisia za chuki yaani CHUKI.
Ni suala la muda tu. Nipatie muda mengine yatafuata.Kwa hiyo ni kweli kwamba Jua linazunguka kupitia hizo njia unazozisema?
Acha kusema uongo. Aliendelea vipi kuwa bikra wakati alijifungua mtoto au alifanyiwa upasuaji? Leta uthibitisho na sio maneno yako...
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea, akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena; “soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia; “soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake. Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.
Mara, yule mtu (Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia” Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
Nani amekwambia Dhulqarnayn ndio Alexander the Great ? Nipe ushahidi.
Mayahudi waliwaamnia maqurayshi wakamuulize mtume Muhammad kuhusu habari za mja mwema huyo,ili wapate kumsadikisha kama kweli yeye ni mjumbe wa Allah.
Kuhusu tafsiri ya Qur'an siku zote iko vile vile. Tatizo nyinyi huwa hamsomi tafsiri za aya za Qur'an na wala hamjui mtazipata wapi,ndio maaana mnakosea sana.
Sasa ukitaka kujishughulisha na Qur'an mzee inabidi utenge muda usome tena usome hasa,ila kwa kuperuzi na kuendekeza chuki lazima utaangukia pua.
Na kaa ukijua hakuna wa kuichallange Qur'an na hatotokea sababu Qur'an imekamilika.
Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
toa andiko acha kubuniBro Qur'an is full of violence and laws
Discrimination against women etc
Aya 84. Dhul-Qarnain. Maelezo ya Qur'an juu ya huyu Dhul-Karnain yanapatana sana
na habari za mfalme Cyrus aliyetawala nchi ya Ajemi baada ya kifo cha baba yake, na baadaye
akaishinda Media ambayo ilikuwa ufalme mkubwa kuliko Ajemi yenyewe. Qur'an imeonyesha
alama nne za huyu Dhul-Karnain: (1) Alikuwa Mtumishi mtawa wa Mwenyezi Mungu na alikuwa
akipokea wahyi (ufunuo) (Aya 87, 92 na 99). (2) Alikuwa mshindi mkuu wa vita na mtawala
mwema mwenye haki; na mataifa aliyoyashinda akayatendea kwa ukarimu kabisa (Aya 85, 89).
(3) Alikwenda upande wa magharibi na akashinda vita sana mpaka alipofika mahali akaona jua
linatua ndani ya chemchem ya maji yaliyovurugika, kisha akaelekea upande wa Mashariki na
akashinda nchi nyingi (Aya 85, 87, 88, 89). (4) Mwisho akaenda sehemu za katikati ambako
kulikaa washenzi, na ambako Gog na Magog (Yajuja na Majuja) walikuwa wakishambulia, na
akajenga ukuta kuzuia mashambulio hayo (Aya 94-98). Sasa katika wafalme wakubwa wa zamani
Cyrus ndiye anazo sifa hizo nne kwa wingi kabisa. Hivyo, yeye anastahili kufikiriwa kuwa Dhul-
Karnain anayeelezwa na Qur'an.
Aya 85. Kila kitu, mradi wake ni kila kitu kilichohitajiwa kwa kumalizia kazi yake.
Aya 87. Maneno haya, Akaliona linatua katika chemchem iliyovurugika, yanaonyesha
ya kwamba maji yale yalikuwa mapana sana, yaani bahari. hata inakuwa ukisimama pwani
wakati wa magharibi jua linaonekana linatua ndani ya bahari. Bahari hiyo inaitwa Bahari nyeusi
iliyoko Asia Minor.
Mkuu, hayo siyo maelezo yangu mi nimecopy tu kutoka kwenye hicho kitabu.Mkuu,elezeni vitu kwa uyakini na sio kuongezea chumvi!
Kwa maelezo yako hapo juu, ina maana maelezo ya Khadija juu ya tabia njema ya Muhammad kabla ya ufunuo, ndiyo yanatoa ushuhuda kwamba kile kilichomkuta Muhammad pangoni ilikuwa ufunuo kweli na si vinginevyo? Kwa maelezo yako, ina maana hata maelezo ya Khadija nayo yana ufunuo?Kwa maana kwamba kila alichokiongea Khadija kuhusu ufunuo wa Muhammad ndiyo ukweli?
Mkuu hayo siyo maelezo yangu mi nimecopy tu kutoka kwenye kitabu cha kislam.Malaika wa kweli asingaliweza kufikia kumkaba Muhammad kwa kushindwa kusoma jambo lolote.Ikiwa Jibrili alitumwa na Mungu kwa Muhammad ina maana Mungu MWENYE UWEZO wa kufahamu yote, hakuwa akifahamu kuwa Muhammad hajui kusoma wala kuandika na hivi atafute njia ya kufanya mapema kuliko kusubiria hadi Jibrili aende kumkwida kiasi kile Muhammad hata kumsababishia homa?
Je,ina maana Mungu alikuwa ameishiwa uwezo wa kumfanya Muhammad aelewe kusoma aliyokuwa anaambiwa ayasome ndio maana aliamua kutumia nguvu?
Je,kwa maelezo yako, ina kipigo ndio mwishowe kilimfanya Muhammad aweze kusoma alichokuwa anaelezwa kusoma?
Nani amekwambia Dhulqarnayn ndio Alexander the Great ? Nipe ushahidi.
Mayahudi waliwaamnia maqurayshi wakamuulize mtume Muhammad kuhusu habari za mja mwema huyo,ili wapate kumsadikisha kama kweli yeye ni mjumbe wa Allah.
Kuhusu tafsiri ya Qur'an siku zote iko vile vile. Tatizo nyinyi huwa hamsomi tafsiri za aya za Qur'an na wala hamjui mtazipata wapi,ndio maaana mnakosea sana.
Sasa ukitaka kujishughulisha na Qur'an mzee inabidi utenge muda usome tena usome hasa,ila kwa kuperuzi na kuendekeza chuki lazima utaangukia pua.
Na kaa ukijua hakuna wa kuichallange Qur'an na hatotokea sababu Qur'an imekamilika.
Lengo la mada yako haikua kutafuta ukweli bali kuushambulia uislam huo ni udhaifu mkubwa nimefuatilia mjadala mzima mpaka sasa nimekuelewa vyema, nikujuze huyo Alexander sio Dhurqarnain, Dhurqarnain kwa mujibu wa Qur'an alikutana Nabii Musa swali je huyo Alexander alikuwepo kipindi cha MusaMkuu:
Ninaona hatari moja katika baadhi ya waumini wa Kiislamu.Kwamba ninyi munajitahidi kuinyoosha Kurani kwa kuipa ujumbe mwingine zaidi hata ya Muhammad alivyokusudia.Alexander the Great alifariki miaka mia tatu kabla Yesu hajaliwa na Miaka 800 kabla Muhammad hajazaliwa.Ilikuwaje watu wamuulize Muhammad habari za Dhul-Qarnaini (Alexander the Great).Ni lini Muhammmad alionana na Alexander the Great?