Mleta mada Amani iwe nawe.
Katika suratul Kahfi aya ulizozinukuu kuhusu Dhul Qarnayn na kuzama kwa jua kwenye Chemchem yenye matope meusi. Ili uweze kuielewa hiyo aya na Qur'an kwa ujumla wake kuna mambo inabidi uyafahamu. Ulichokinukuu wewe ni Fasiri INA maana kwa hali ile iliyoandikwa kwa Kiarabu umeipeleka kwa Kiswahili. Vilevile kuna tafasiri kwa maana kilichoandikwa kinaelezewa kwa undani ili upate mantiki nzima na uelewe kile kinachokusudiwa.
Tukirudi katika hiyo aya inaanza kwa "Wanakuuliza habari za Dhulqarnayn. Sema; kwa yakini nitawasomea katika hadithi yake".
Na wanakuuliza, kwa maana Mtume anaulizwa, ni akina nani wanauliza habari za Dhul- Qaryn? Hii hoja itajibu swali lako linalouliza ni nani huyu mtu, Dhul Qarnayn?
Maqurayshi wa Makkah waliambiwa na Wayahudi wa Madinah, wakamuulize Mtume maswali 3 na nia ni kutaka kupima kama kweli Muhammad ni Mtume ama laa. Maswali yalikuwa ni kuhusu Roho, kuhusu Dhul Qarnayn na ahlul kahf(watu wa mapangoni) ambayo imebeba jina la Sura. Kwa sababu hakuna hayo mambo anayeyajua isipokuwa ni mitume tu, na hizo habari za hayo maswali 3 yalikuwepo katika vitabu vya watoto wa Israel. Kuhusu Dhul Qarnayn katika Qur'an tumepewa habari yake kidogo tu kama aya inavyosema "kwa yakini nitawasomea katika( baadhi) hadithi yake. Huyu mtu, Dhul Qarnayn alikuwa ni mtumishi( Mfalme) aliyetawala na kueneza sheria ya Mungu. Alikuwa mshindi mkuu wa vita. Alisafiri yeye pamoja na jeshi lake kuelekea sehemu tatu(3) za Dunia, magharibi ya mbali ya Dunia, mashariki ya mbali ya Dunia na mwishoni kaskazini mwake mwa Dunia. Alikwenda upande wa magharibi na akashinda vita sana mpaka alipofika mahali akaona jua linatua ndani ya chemchem ya maji yaliyovurugika.
Aya inayoendelea inasema "bila shaka tulimwamrisha katika ardhi na tukampa njia za kupatia kila kitu", kwa maana mradi wake ni kila kitu kilichohitajiwa kwa kumalizia kazi yake Mungu alimpatia huo uwezo. Maneno haya, akaliona Jua linatua katika chemchem iliyovirugika, tafsiri yake ni hii; kwa maana mahali alipofika maji yake yalikuwa mapana sana yaani bahari, Hata inakuwa ukisimama pwani wakati wa magharibi jua linaonekana linatua ndani ya bahri. Ukiwa pwani ukiangalia kuzama kwa jua unaona kama linatua kwenye tope au chemchem iliyovurugika. Ndivyo Dhul Qarnayn alivyoona na ndivyo Qur'an inavyoelezea kama Dhul Qarnayn alivyoona na hiyo bahari kuzama kwa jua na akaona hiyo hali ni bahari Nyeusi iliyoko Asia minor.
Watu wanatafsiri Qur'an kwa kusoma maneno yaliyofasiriwa kwa lugha mama( Kiarabu) na kwenda lugha nyenginezo wakidhani kwamba tafsiri yake ndiyo IPO hivyo hivyo hapana, Qur'an ina somo kabisa LA tafsiri yake.
Kuhusu Jua tangu kale INA njia yake. Kwenye Qur'an suratul Anbiyaa aya 33 na Suratul Yaasin aya ya 38 zinaelezea Jua na Mwezi zina njia sake(orbits) zinazopitia. Na si kama baadhi ya watu wanajaribu kufananisha na Sura ya Al Kahfi kuhusu Dhul Qarnayn. Kuhusu jua ndilo linalozunguka badala ya Dunia hili ntakujibu baadae utanisamehe afya yangu imetetereka kidogo tangu Jana kwa hiyo sipo vizuri sana.