Kwanza ni jambo nzuri kupata mjadala kama huu, lakini napenda kuonyesha mleta mada hii haikuwa mtu wa kwanza kujadili mada hii kwa kuwa hata yeye amekwenda kuchukua sehemu nyingine na nitaweka source mojahapa
Answering Muslims: 2011
UONGO WA MTUME MUHAMMAD NA QURAN KUHUSU KUPASUKA KWA MWEZI NA KUTEMBEA KWA JUA
Ukifungua link hiyo ndio mleta mada alipo itoa mada hii.
Pili hata mleta mada hakuchukua muda kupitia aya husika kama alivyo dai amepitia aya husika zaidi amechukua mawazo ya watu ambao wanafikiri kulikuwa na makosa kwenye aya hii, tofauti ni kwamba mleta mada amejaribu kumuweka Mtume Muhammad S.A.W kama muhusika lakini kwenye source nyingine wao wanashutumu Quran kuwa imepotosha kwenye jambo hili.
Lakini kwa kuwa mada ipo mezani ina hitaji majibu then nitapenda kwanza watu wafahamu kujadili jambo la imani ni sawa na elimu ya ukubwa wa bahari, lakini uzuri Quran na mafundisho ya mtume yana elekeza umuhimu wa elimu, na pili yana ruhusu ku challenge Quran kama unaweza kwa kuwa "Quran ni kitabu kisicho kuwa na shaka" kwa hiyo Mungu ana ruhusu watu kujadili na kutoa hoja zao ili wapate majibu kwani wakiridhika watafata muongozo wa haki. Hivyo mleta mada yupo sahihi kabisa anayo haki ya msingi kuhoji kwani Mungu alimpa binaadamu akili lakini pia alimpa na yakini ambayo yakini ndio inayo mfanya mtu kuafiki au kupinga.
Lakini kwanini wana science wanachagua vitu vichache kati ya vingi mfano
Vipi Quran ina sema kuhusu hatua za uzazi?
Vipi Quran inasema kuhusu kukutana kwa bahari ya maji baridi na maji chumvi
Vipi Quran inasema kuhusu kulea kwa watoto na hasa kwenye swala la kunyonyesha
Vipi Quran inasema kuhusu vinasaba
Ukipita kwenye mambo haya ambayo kwa kiwango kikubwa yapo prove wakati huu wa modern science but Quran imeongelea kipindi cha nyuma sana mambo hayo.
Mwisho napenda ku wajulisha wadau wa science kuwa ugunduzi hauna mwisho ndio maana mwanzo walisema dunia ipo kama meza,mara dunia ipo round, mara jua limesiamama, wengine jua lina tembea, wengine dunia ina tembea but as technology inavyo zidi kwenda mbele ndio hata watu wa sayansi wanapinga ungunduzi wa mwanzo hivyo na imani siku za usoni watakuja wana sayansi kupinga dhana hii unayo hoji wakati huu kwani ujuzi unakuwa na vyombo vinabadilika so sayansi ni kitu kisicho baki kwenye ukweli bali ni fikira za wakati fulani na hubadilika vitendea kazi vinapo badilika kwani huleta majibu mengine tofauti na yale ya mwanzo
Hivyo na amini kuwa wakati technology and tools za kisasa ukifika wanasayansi watakuja ku prove hizo verse (aya) zipo sahihi kwa kuwa wakati hata Mtume alipo kuwa ana pewa Quran aliambiwa kuwa tunakujuza habari zilizo pita,wakati huu na wakati ujao So kuna vitu ambavyo vipo kwenye simulizi vimesha kuwa proved na vingine bado kwa kuwa ni simulizi zilizo katika makundi tofauti na imani tunacho hoji leo na kuona hakiwezekani kuwa kilivyo kwenye Quran then kitakuwa prove siku za mbele.
Je kwanini Mungu amefunga mambo kwenye mafumbo ni kutoa nafasi ya binaadamu ku challenge uweza wake ili kupata yakini