Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
hebu tujadili mada iliyopo mezani tafadhali " kama kuna ambacho kinakukera toka kwangu na umeshindwa ", kukivumilia PM yangu haijafungwa "ruksa kuni pm nakunikosoa "", hivyo ndivyo ambavyo watu makini hufanya "",KARIBU
Ambacho nimeshindwa kuvumilia nimeshakisema ni kuhusu hiyo tabia ya kujichekesha.
 
tayari umeshajibu swali lamtoa mada ",au nawewe waruka ruka tu " MIMI mwenyewe "pia nipo upande WA mtoa mada",,nataka kujua ", hayo matope yapo wapi angani ah hapa duniani "". hebu fuatilia comments za page ya kwanza ", nimeshauliza sana haya maswali" sijakuona ukijibu "", though nimekinai kurudia rudia kuuliza swali hilo hilo moja aiseee
Nimekujibu hicho ni kisa anachosimuliwa mtume kuhusu dhul qarnaini aliyoyafanya na aliyoyaona kwa upeo wa macho ya dhul qarnaini kipi ujaelewa sasa hapo
 
Umeandika maneno mengi lakin pumba....kinachokusumbua wewe na wengine wengi ni tafsiri kaa ukijua kiswahili ni lugha ambayo hajajitosheleza kwa maneno kuna vitu vingi hajitafsiriwa inavyotakikana kutokana na uchache wa kisamiati sio Quran tu hata kwenye bible...sasa kilichopo kwenye hiyo sura Allah ametumia neno maghirib...maghrib linamaana ya kuchwea, au kuelekea mwisho wa kitu au kureflect....maana zote zinafit kwa alichokisema Allah kuwa Dhur alifika eneo muda jua kutuama likiwa lina reflect miale yake kwenye tope sio jua kuzama kwenye tope maana ya hapa Allah alizungumzia nyakati...halafu ni mtu tu umeamua kujitoa akili ni Aya ngapi Quran imezu gumzia jua na muzunguko yake had ambayo sayans mwanzo ilituambja jua halizunguki zinazunguka sayari zingine(kama.ambavyo wewe bado unaamini sababu hutafuti unapenda kulishwa maneno ya upotoshaji) ila Quran imesema jua linazunguka na baada ya sayans kupiga hatua wakagundua jua huchukua siku 26 kumaliza mzunguko wake kuna kitu wanaita black dot kwenye mzunguko wa jua ambayo jua huchukua siku 26 kuifikia ile dot Quran imesema hayo, Quran imezungumzia The big bang kwenye surah ambiya, Quran inazunguzia embriology ambayo hatua za ukuwahi wa binadamu ambazo huwez kuziona kwa macho ya kawaida had microscope ambayo by the time haikuwepo..na ndio maana Allaha kasema mara nyingi hichi ni kitabu kwa watu wenye akili wenye kufikiri...unatakiwa usome sana wengi wenu mnatatizwa na tafsri na mnafata vitabu vya wazungu na wao walivhemka tafsiri au wanapotosha makusud sababu ukiandika kitabu against islam kinapata biashara kubwa sana haswa kwa ulaya na america.!

Allah amezungumza kuchomoza na kuchwea kwa jua ili tuekewa kwasababu ndivyo tynavyozungumza sisi wanadamu ikiwe hata wana sayansi wanatumia neno sun set and sun rise lakin je jua huchomoza?? Jua linaonekana na kupotea kulingana na mzunguko wa dunia.. ALLAH amesema ni yeye ndio analiwezesha hilo mchana ku overlap kiza na kiza ku overlap mchana na akase hii ni kwa watu wenye akili..!

Hich ni kitabu kisicho na shaka ndani na Allah amema "mnasema kitabu hichi kaandika Muhammad basi leten japo mfano wake" pia akajitamba leten japo mfano wa sura moja na kisha akasema leten mfano wa aya kumi na baadae akasema leten mfano wa aya moja...sababu structure ya Quran hajazaliwa mwanadamu wa kuiweka vile ilivyo nikipata muda nitawaletea mada ya muujiza wa Quran kinamba.!
Hakuna kitu Quran inajua ni hadithi tu hata biblia kunavitu havipo sahihi kabisa ila bora biblia ilijikita kwenye Imani na sio sience Sasa nyinyi waislamu mnataka sema kila kitu kinachofanyika kwenye hii Dunia cha kisayansi eti Quran ilishatamka.
 
ulimuona alivyoenda kuzimu,ulimuona alivyotembea kwenye maji?

yote haya tumeandikiwa kwenye vitabu na tuna viamini kabisa,kwa mungu hakishidikani kitu mkuu

na yesu tunaaambia alipaa mbinguni,je alipaaje kwenda huko kupita kwenye ma Galaxy yote hayo hata angeenda kwa speed ya light mpaka leo angekua hata theluthi ya milky way galaxy hajaimaliza

kwa hiyo hapa ukiangalia yote haya ni miujiza tu na ni kwa msaada wa mungu hao mitume ndio wamefika huko au wametenda hayo na si vinginevyo ila kwa upeo wa binadamu hilo tunaona haliwezekani kabisa

Yesu kapaa takribani miaka elfu mbili iliyopita ina maana at a speed of light,ambayo matter yoyote haiwezi kuzidi hapa ina maana mpaka sasa hata kwenye nyota ya Betelgeuse hatakua hajafika bado na voyager ingemuona basi
Ndio tatizo la wakristo humu ndani yesu kupaa sawa akili yao inakubali lakn muhamadi kupaa sio sawa akili yao aikubali ni kazi kwelikweli
 
Baadhi kama siyo mengi ya maandiko ya kwenye vitabu vya dini yanaelezea mambo au vitu ambavyo sisi wanadamu kwa uwezo na utashi inatubidi tuvifanyie utafiti na kuvitafutia majibu...

Ni sawa na chuo pale unapopewa mwanga au kianzio cha jambo fulani alafu unaambiwa kafanye research au iwe assignment...


Cc: mahondaw
 
hahaaa halafu akajiwekea defense mechanism kwamba mtu yeyote atakaye mpinga mtume basi amelaaniwa " means hata ukiona amekwambia uwongo uukubali tu '' Kama huo uwongo wa jua kuzama kwenye matope
Kuna kitabu nilisoma hahaha anakwambia mtu alipoanza akawaambia watu nyie hamjui chochote halafu yeye anajua kila kitu Sasa ndo unajiuliza. Alijuaje kila kitu hata Habari za sperm tu alikua hajui wala genomes n genes
 
Hakuna kitu Quran inajua ni hadithi tu hata biblia kunavitu havipo sahihi kabisa ila bora biblia ilijikita kwenye Imani na sio sience Sasa nyinyi waislamu mnataka sema kila kitu kinachofanyika kwenye hii Dunia cha kisayansi eti Quran ilishatamka.
Umeona sasa Quran aijaandika vitu vingi mfano asili ya muhindi au mjapani quran aijaandika ww ujaelewa quran
 
Binafsi elimu dunia nimeisoma na kuilinganisha na elimu ya Mungu. Elimu ya Mungu iko pure na hapana chembe ya uongo. Suala la jua kutozunguka hiyo ni uongo wa kisayansi, kwani kiuhalisia hata kwa kulitazama jua lina Move.
Kwamba dunia ni elliptical sphere, pamoja kung'ang'anizwa nikariri hivyo mpaka leo hii nimekataa na naona kwa macho yangu dunia ni flat, Jua, Mwezi na Nyota zote zinazunguka juu ya uso wa dunia, Jua na mwezi zikiwa na ukubwa sawa na kiwango cha mwanga tofauti lakini Nyota zikiwa ni ndogo kuliko jua na mwezi.
By the way, Jua sio Nyota na wala Nyota sio jua kama sayansi inavyolazimisha.
Zaidi ya hapo vitu vinavyoitwa sayari is just "sci-fi" tu but in reality hakuna kitu kinaitwa sayari angani but kuna Mwezi, Jua, na Nyota.
Drama za NASA hasa ni za kupinga ukweli halisi (ambao hata wao wa Naujua) na kule launch uongo mkuu kwa malengo maalumu kabisa.
Bila Shaka Dunia sio sayari na haijawahi kuwa, tena ni kweli Antarctica sio bara la saba kwa ukubwa bali ni Sio bara kabisa ndio maana hata kwenye bendera ya UN naya USGS halijaoneshwa kwa kwa kuwa sio bara.
Kwa kumalizia ni kwamba sio wanasayansi wote wanaothibisha kuwa jua ni Immovable objects lipo kundi kubwa tu la wanasayansi wa kale na wa kisasa wanaothibisha pasipo chembe ya shaka kuwa dunia ni immovable, na jua, mwezi na Nyota ni movable objects.
So neno la Mungu always linabaki sahihi na la binadamu (hao wanasayansi) uongo wa makusudi wenye nia ovu!!
Wewe umechanganyikiwa
 
Kuna kitabu nilisoma hahaha anakwambia mtu alipoanza akawaambia watu nyie hamjui chochote halafu yeye anajua kila kitu Sasa ndo unajiuliza. Alijuaje kila kitu hata Habari za sperm tu alikua hajui wala genomes n genes
Nyoosha maelezo
 
Kwani hicho ni kipande cha aya?? Kila aya ndani ya fuqan ina sababu ya kushuka, imeshuka wapi, na baba kassim kaifundishaje! sawa! Nakuulizia tena alicho ongea muhammad kwamba asali ni haramu kasema kweli au ni uongo? Jee allah alikuwa anamsifu au anamkemea?! nimekuletea hiyo ayat baba ya wewe kudai kwamba baba kassim hajawahi kusema uongo!


images
 
Kama Black Hoke ni uongo. Hilo si tatizo kubwa.

Kwa sababu.

1. Sayansi haijawahi kusema kwamba haikosei na kila inachosema ni sawa.

2. Sayansi inasisitiza kukosolewa. Ukiweza kuthibitisha habari za Black Holes ni uongo, sayansi itakupa nishani ya Nobel kwa kuonesha uongo ulipo.

3. Hakuna contradiction wanasayansi kukosea. Wao ni watu tu wanatafuta majibu. Hawana uwezo wote, ujuzi wote wala upendo wote. Hawa kukosea si ajabu.

Habari za Mungu zikionekana na makosa, hilo lina maajabu.

Kwa sababu.

1.Mnasema Mungu hakosei na kila anachosema ni sawa.

2. Mnasema Mungu hakosolewi na kukosolewa ni kufuru.

3. Kuna contradiction kubwa kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwa kakosea.

Ukionesha Black Hokes ni uongo, nitasema hao ni Wanasayansi tu, wamekosea, hawajawahi kusema hawakosei.

Nikikuonesha dhana ya Mungu kuwepo ni uongo utasemaje?
aiseeeee
 
Sijui.Hilo ninswaliblankuchunguzwa.

Katikanuchunguzi wa kupata jibubsahihi **** njia nyingi. Kuna kitu kinaitwa "elimination method". Unaondoa majibu yasiyo sahihi unatafuta sahihi.

Katika elimination method hapa tunaona Mungu si jibu sahihi. Ana contradictions. Hana logicalnconsistency.

Ni kama umeambiwa tafuta square root ya mbili. Umeambiwa ni ndogo kuliko mbili. Halafu mtu anakwambia jibu sahihi ni 10. Hata kablabhujajua square root ya 2 ni nini, utajua si 10. 10bsi jibu sahihi. Kwa sababu lina contradict kanuni inayosema jibu ni lazima liwe dogo kuliko 2. Jibu la square root ya 2 ni 10 halina logical consistency na square root ya 2 kuwa ndogo kuliko 2.

Dhana ya kuwapo Mungu nibkama jibu la square root ya 2 kuwa 10. Majibu yote yana contradictions. Majibu yote hayananlogical consiatency. Ukikubali Mungu huyu yupo, nibsawa nabumekubali square root ya 2 ni 10.

Hata kama sinui tumetoka wapi (sijuibsquare root ya 2 ni nini) najua hatutokani na Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote (najua kwamba square root ya 2 haiwezi kuwa 10).

Tungekuwa tumeumbwa na Mungu huyo, dunia isingekuwa na mabaya. Square root ya 2 ingekuwa 10, kwanza 10 ingekuwa ndogo kuliko 2.

Kusingekuwa na magonjwa, vifo, umasikini etc.

10 ingekuwa square root ya 2, 10 X 10 ingekuwa 2. Lakini tunaona 10 X 10 si 2. Ni 100.
Ina lillah wa Ina lillah rajuun
Mtume Mohammad s.a.w anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Ndugu- Kiranga ukihoji sana utakufuru na kuingia kwenye dhambi ambayo iwezo unao wa kuikwepa
There is no need of apply "Complex parception" towards God..

Mungu ibarik TANZANIA...
 
Wanajukwaa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.


Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?


2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?


3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?


· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?


· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.

Usipotoshe maana halisi ya Aya hizo za Quraan ambayo ni maelezo kuhusu kisa cha vijana wawili walio lala ndani ya cave na kuamka baada ya generation mpya kuzaliwa mahali hapo.
Unajaribu kupotosha maneno ya Allah ili kujipa tamaa kuwa uko sahihi na ukafiri wako.
Jua kuzama , kutua au kuchomoza hotokea magharibi na mashariki ya dunia. Hili limewekwa wazi na Quraan tukufu.
Kama hujui maana ya lugha jifundishe lakini usipotoshe kwa kujifurahisha kupotoka.
Mimi hapa ninapokaa jua huzama nyuma ya nyumba yangu na linainhia baharini ! Na huchomoza Alfajiri upande wa mashariki kutoka kwenye magorofa! Jee maana yake hilo jua linatoka kwenye magorofa na kutokomea baharini !
Kusema hivo ni kujaribu kuonesha upande gani jua lina zama na kutua
Elimu haina kikwazo jaribu kujifunza upate kuelimika . Ujinga ni wa kujitakia hasa unapokubali za kuambiwa tu bila na kuchanganya na za kwako
Tafsiri kwa kiswahili kinacholekea ya aya hizo uliozitaja

85. Kwa kutumia njia hizo aliweza kueneza madaraka yake katika ardhi, na akafuata njia mpaka akafika huko magharibi kunako kuchwa jua.

* 86. Akenda mpaka akafika pahala mbali huko upande wa magharibi, akalikuta jua kwa linavyo onekana kwa macho kama kwamba linazama pahala penye chemchem ya maji ya moto na matope meusi. Na karibu ya chemchem hii Dhul- Qarnaini aliwakuta watu makafiri. Mwenyezi Mungu akamtia moyoni mwake afanye mojapo ya mambo mawili: Ama awaite kwenye Imani, na hili kwa hakika ni jambo zuri; au awapige vita ikiwa hawakuitikia wito wa Imani.


* 87. Dhul-Qarnaini akawatangazia: Katika wao aliye jidhulumu nafsi yake kwa kubakia katika ushirikina, basi amestahiki adhabu ya duniani kutokana naye, na kisha atarejea kwa Mola wake Mlezi. Naye atamuadhibu adhabu kali wasio ijua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom