Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Mleta mada Amani iwe nawe.Wanajukwaa:
Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.
Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.
Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.
Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.
Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):
“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”
Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.
Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).
Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki. Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.
Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.
Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.
Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).
Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:
1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?
2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?
3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi
Katika suratul Kahfi aya ulizozinukuu kuhusu Dhul Qarnayn na kuzama kwa jua kwenye Chemchem yenye matope meusi. Ili uweze kuielewa hiyo aya na Qur'an kwa ujumla wake kuna mambo inabidi uyafahamu. Ulichokinukuu wewe ni Fasiri INA maana kwa hali ile iliyoandikwa kwa Kiarabu umeipeleka kwa Kiswahili. Vilevile kuna tafasiri kwa maana kilichoandikwa kinaelezewa kwa undani ili upate mantiki nzima na uelewe kile kinachokusudiwa.
Tukirudi katika hiyo aya inaanza kwa "Wanakuuliza habari za Dhulqarnayn. Sema; kwa yakini nitawasomea katika hadithi yake".
Na wanakuuliza, kwa maana Mtume anaulizwa, ni akina nani wanauliza habari za Dhul- Qaryn? Hii hoja itajibu swali lako linalouliza ni nani huyu mtu, Dhul Qarnayn?
Maqurayshi wa Makkah waliambiwa na Wayahudi wa Madinah, wakamuulize Mtume maswali 3 na nia ni kutaka kupima kama kweli Muhammad ni Mtume ama laa. Maswali yalikuwa ni kuhusu Roho, kuhusu Dhul Qarnayn na ahlul kahf(watu wa mapangoni) ambayo imebeba jina la Sura. Kwa sababu hakuna hayo mambo anayeyajua isipokuwa ni mitume tu, na hizo habari za hayo maswali 3 yalikuwepo katika vitabu vya watoto wa Israel. Kuhusu Dhul Qarnayn katika Qur'an tumepewa habari yake kidogo tu kama aya inavyosema "kwa yakini nitawasomea katika( baadhi) hadithi yake. Huyu mtu, Dhul Qarnayn alikuwa ni mtumishi( Mfalme) aliyetawala na kueneza sheria ya Mungu. Alikuwa mshindi mkuu wa vita. Alisafiri yeye pamoja na jeshi lake kuelekea sehemu tatu(3) za Dunia, magharibi ya mbali ya Dunia, mashariki ya mbali ya Dunia na mwishoni kaskazini mwake mwa Dunia. Alikwenda upande wa magharibi na akashinda vita sana mpaka alipofika mahali akaona jua linatua ndani ya chemchem ya maji yaliyovurugika.
Aya inayoendelea inasema "bila shaka tulimwamrisha katika ardhi na tukampa njia za kupatia kila kitu", kwa maana mradi wake ni kila kitu kilichohitajiwa kwa kumalizia kazi yake Mungu alimpatia huo uwezo. Maneno haya, akaliona Jua linatua katika chemchem iliyovirugika, tafsiri yake ni hii; kwa maana mahali alipofika maji yake yalikuwa mapana sana yaani bahari, Hata inakuwa ukisimama pwani wakati wa magharibi jua linaonekana linatua ndani ya bahri. Ukiwa pwani ukiangalia kuzama kwa jua unaona kama linatua kwenye tope au chemchem iliyovurugika. Ndivyo Dhul Qarnayn alivyoona na ndivyo Qur'an inavyoelezea kama Dhul Qarnayn alivyoona na hiyo bahari kuzama kwa jua na akaona hiyo hali ni bahari Nyeusi iliyoko Asia minor.
Watu wanatafsiri Qur'an kwa kusoma maneno yaliyofasiriwa kwa lugha mama( Kiarabu) na kwenda lugha nyenginezo wakidhani kwamba tafsiri yake ndiyo IPO hivyo hivyo hapana, Qur'an ina somo kabisa LA tafsiri yake.
Kuhusu Jua tangu kale INA njia yake. Kwenye Qur'an suratul Anbiyaa aya 33 na Suratul Yaasin aya ya 38 zinaelezea Jua na Mwezi zina njia sake(orbits) zinazopitia. Na si kama baadhi ya watu wanajaribu kufananisha na Sura ya Al Kahfi kuhusu Dhul Qarnayn. Kuhusu jua ndilo linalozunguka badala ya Dunia hili ntakujibu baadae utanisamehe afya yangu imetetereka kidogo tangu Jana kwa hiyo sipo vizuri sana.