Tia Neno na hapo
View attachment 880246 usiangalie picha tupu ya ushuzi ilaha na ujumbe picha [emoji38] [emoji38]
zawadi yako hii
NAFSI MBALI MBALI ZIKISHIRIKIANA KATIKA UMILELE:
Kama sehemu za mungu wa Kikristo ni nafsi tatu mbalimbali zikishirikiana pamoja milele, hapo swali litazuka kuhusu uhusiano
wa ndani wa nafsi hizo.
Kama hizo ni tatu daima zikifanyiza mungu mmoja, haikosi kila moja katika hizo tatu itakuwa na fikra yake na upendo wake binafsi hata kwamba taabu ya mmoja, kama anaweza kutaabika, ni taabu yake tu.
Nafsi nyingine mbili zinaweza kuihurumia tu bila ya kushirikiana katika shida yake.
Naam, haiwezekani kuwaza namna Mungu anavyofikiri na kuamua, lakini madai haya ya kwamba yeye kwa hakika ni nafsi tatu zilizounganika pamoja kufanyiza Mungu mmoja yanatupatia haki ya kujaribu kutafuta uhusiano wa ndani baina ya mifumo
mitatu ya kujitegemea ya kufikiria.
Mfano wa kwanza unaweza kuwa wa mtoto mmoja aliyezaliwa na vichwa vitatu. Hali hiyo mbaya kupita kiasi inamaanisha ya
kwamba huyo ni mtu mmoja kwa sababu kuna kiwiliwili kimoja, mikono miwili na miguu miwili, lakini vichwa vitatu vinaleta
matatizo yasiyoweza kuelezeka hakika hasa ya kila kichwa katika hivyo vitatu.
Kama viumbe visivyo vya kawaida vikiishi muda wa kutosha mpaka viweze kusema na kujieleza, hapo tu ndipo twaweza kuwauliza yanayofanyika katika vichwa vyao vitatu mbali mbali.
Bila ya kuwa na ujuzi huo haiwezekani kuamua huyo ndiye mtu mmoja ambaye anashirikiana katika mawazo matatu ama ni watu watatu wanaoshirikiana katika mwili mmoja.
Ni la ajabu ya kwamba jiha hiyo ya muhimu sana ya itikadi ya Kikristo haikuelezwa kabisa katika maandiko. Naam, kuhusu
Kristo na Roho Mtakatifu kuna ushuhuda mwingi wa kuhakikisha ya kuwa hao ni wawili mbalimbali wasioshirikiana katika fikara
wala katika maono.
La sivyo, itakuwa vigumu kufahamu madhihirisho ya Roho Mtakatifu tofauti kabisa na Kristo, hususan katika kipindi ambamo Kristo alikuwa amefungwa katika mwili wa mtu.
Maswali ambayo yangezuka kuhusu kilichotendeka kwa Kristo, katika muda wa kusumbuka kwake, kwa kulinganishwa na sehemu mbili nyingine za Mungu wa Kikristo, ni haya yafuatayo:
1. Je, nafsi nyingine mbili, Mungu Baba na Roho Mtakatifu, zilishirikiana kwa njia yoyote katika mwili wa Yesu Kristo au katika majaribu yake kwa kulingana na mwili huo?
2. Je, Yesu peke yake alikuwa ndani ya mwili huo, na kwa hiyo yeye hakushirikiana na nafsi nyingine mbili za Utatu katika majaribu yake kwa kulingana na mwili huo?
Matokeo ya hilo la kwanza yamekwisha zungumzwa tayari. Na kuhusu hilo la pili tatizo jingine tena linazuka kuhusu uhusiano wa Yesu na nafsi nyingine mbili za utatu katika muda wa Yesu kuwa katika mwili wa mtu.
Je, katika muda huo wote Yesu alitengwa kikamilifu na nafsi nyingine mbili na akajitegemea, ama bado alibaki kuwa sehemu isiyoweza kutengwa na nyingine mbili isipokuwa tu yeye akashika makao yake katika mwili wa mtu pasipo kushirikiana na wenzake wawili?
Sasa tunalo swali jingine tena la kulijibu:
3. Je, uungu wake mzima-mzima ulikuwamo ndani ya mwili wake wa kibinadamu, ama huo ulijitokeza tu nje kutoka kwenye 'sura' ya Mungu Baba na Roho Mtakatifu ambayo alishirikiana nao katika hiyo, kama kajidole kadogo kale kanakojitokeza nje ya mwili wa vidudu vidogo vidogo mno visivyoonekana pasipo kutumia darubini kali?
Jambo hilo litatufanya tuamini pia ya kwamba katika kipindi hicho Yesu alikuwa mkubwa kuliko wenzake wawili, kwani yeye
alishirikiana kwa usawa pamoja na Mungu Baba na Roho Mtakatifu katika 'mwili' wa kiungu, lakini hao wawili hawakushirikiana naye katika 'kajidole' kale kalikojitokeza ka 'mwili' wa mtu.
Hivyo basi, ili kurahisisha kuelewa habari yenyewe twajaribu kufafanua hitilafu zilizomo humo na mambo yasiyoeleweka akilini kwa kueleza hali mbalimbali za kukisia ili kutafuta ukweli.
Naam, mifano hii isichukuliwe na wasomaji kuwa hasa ndivyo ilivyotendeka.
Suala lililoko mbele yetu ni kwamba je, yupo mtu mmoja anayedhihirisha sifa tatu ama anapitia hali tatu tofauti. Hiyo itazusha swali la kufikiria shauri ya 'Watatu katika Mmoja' na 'Mmoja katika Watatu', hususan kwa jiha malimbali tofauti, na yule yule mmoja kudhihirisha mienendo na hali mbalimbali.
Hali hiyo imekwisha elezwa kirefu katika mlango uliopita. Hapa iko haja ya kusisitiza tena habari hii ya kwamba ikiwa mtu mmoja
ama dhati moja inadhihirisha hali mbalimbali, basi haiwezi kuzidhihirisha hali hizo tofauti wakati huohuo mmoja bila ya kujigawa katika sehemu mbalimbali.
Kwa mfano, chukua maji kiasi fulani maalum. Maji hayo yanaweza kugeuzwa yote kuwa mvuke ama barafu pasipo kubakiza sura ya maji.
Kama kunahitajika kuyaona katika sura zote tatu, hamna budi kuyagawa hayo maji katika sehemu tatu ili theluthi moja igeuzwe kuwa barafu na theluthi nyingine kuwa mvuke na theluthi moja ibakie kuwa maji.
Kila sura itakuwa tofauti na sura ya sehemu nyinginezo wala yoyote katika hizo haitashirikiana na nyingine mbili wakati uleule mmoja.
Kiasi hicho cha maji chaweza kugawanywa katika hali tatu, lakini ukubwa wa kila sehemu utakuwa mdogo kuliko yale maji kwa
jumla yaliyochukuliwa mwanzoni, wala hamna yeyote awaye awezaye kusema kwamba hayo ni 'moja katika tatu' na 'tatu katika
moja'.
Kadhalika, basi, kudhihirika Kristo kwa sura ya binadamu ya Yesu, ilhali aliendelea kuungika na Yesu-mtu na Mungu Baba,
haiwezekani asilani kueleweka akilini.
Wanadamu wote wameumbwa kwa vitu vilevile vimoja, lakini kufanana kwao wao kwa wao hakuwafanyi kuwa mtu mmoja
pekee. Sifa zao tofauti, dhati zao mbalimbali, na wote hao kuwepo mbalimbali vinawagawa na wakagawanyika kuishi kila mmoja
peke yake, ijapokuwa wote hao wameumbwa kutokana na kitu kilekile kimoja. Huwezi kuwaita 'mmoja katika bilioni tano' na
'bilioni tano katika mmoja' juu ya wote hao kushirikiana katika uanadamu.