Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Mzew unaona unavyoviandika vya maana sana mpaka unaeka hashtag ya saini yako chini..
Ukishindwa kukubali kitu,inabidi ukiheshimu..
Huwezi kukuta muislam anachana bible kwanaza tunaamini ni moja ya kitabu cha Mungu na pili tunaheshimu wanachokitumia kama muongozo.
Kwanini iwe sahivi wakati Serikali haina dini?? Na kuchana kwake hicho kitabu kuna uhusiano gani na kazi yake??

#Bagwell

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni mihemko isiyokuwa na maana ktk utumishi wa umma. Amemsimamisha kazi kwa kutumia kifungu kipi cha sheria za kazi? Kuna mahali pameandikwa kuwa mtumishi wa umma akichana kohorani asimamishwe kazi? Aache hizo. Analogia Malenga,

Sent using Jamii Forums mobile app
Amesimamishwa kutokana na kukashifu imani za dini nyingine,Kumbuka hii nchi inasheria za kwa upande wa kutambua uhuru wa mtu kuabudu,Fikiria hapo alipochana iyo Quraan pangepita kama wiki ivi basi pangetokea uvunjifu wa amani,kumbuka waislamu ni watulivu sana na pia wana jazba katika mambo kama haya
 
Si kinunuliwe kingine maisha yaendelee, hizi dini/Imani zina mambo mengi sana.
Usihukulie poa katika jambo kama hili,Jana kafanya hilo jambo lakini ukumbuke napo uko alikochana kuna jamii inayomzunguka ya imani iyo fikiria pangetokea nini nyumbani kwake
 
Usihukulie poa katika jambo kama hili,Jana kafanya hilo jambo lakini ukumbuke napo uko alikochana kuna jamii inayomzunguka ya imani iyo fikiria pangetokea nini nyumbani kwake
Hivyo vitabu/vijizuu si vinachapishwa tu? Au vimeshushwa moja kwa moja toka kwa Allah?
 
Dah,Ajira yake ndio basi tena,na ivi kuna vijana wapo katika database ya utumishi wiki ijayo nafasi yake itakuwa ishazibwa..........
 
Hivyo vitabu/vijizuu si vinachapishwa tu? Au vimeshushwa moja kwa moja toka kwa Allah?
We chukulia tu masihara,icho kitendo alichokifanya ni cha uvunjifu wa amani katika jamii ya kilosa
 
Nimeiona hiyo video ,kiuhalisia yule Jamaa kama dish limeyumba vile , kwa hivyo ni sawa kusimashwa kazi , sion Kama ni sawa serekali kua na watumishi machizi na pia kwa hatua hiyo serekali iliyomchukulia itapunguza jazba kwa waislam.

Haya mambo ya kiimani sio mazuri hua yanaleta machafuko kwa hiyo huyo Jamaa kakosea Sana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unaona kwamba dish lake limeyumba kwa nini tena useme kakosea sana tu? Aliyeyumba dish ufanya mambo kwa utashi wake wa kawaida?
 
Awaombe msamaha waumini wa dini ya kiislam kwa kitendo chake kisichokuwa cha kistaarabu cha kukichana na kukinajisi kitabu kitakatifu kwa waislam. Yawezekana kilichomsukuma kufanya hivyo ni pombe ambazo baada ya kumtoka kichwani huenda akili yake itakaa vizuri na baadaye kuanza kujuta.....
awaombe msamaha waislamu au allah mwenye kitabu chake,angalia mnavyojipa mamlaka ya kuhukumu na kujitukuza,mnasahau hata nafasi zenu duniani.

huyu alikuwa wa kuachwa tu.hana tofauti na anayeua mende sababu anamchukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom