Ndio amechana Qur'aan yenyewe.
Waislamu wenye kulichukulia jambo hili kwa jazba, hawana elimu juu ya Uislamu wao, hilo mosi.
Pili,kuna kitu kilichopelekea hili, tumeusiwa sana tusioende mijadala ya dini, kwani mara nyingi hupelekea kutukaniwa vipenzi vyetu (Allah, mtume wetu, na mitume na manabii wengine na waja wema walio pita). Kwahiyo tunatakiwa kujiepusha na mijadala hasa sisi ambao hatuna elimu ya hii dini.
Tatu, uvumilivu jambo la msingi sana ukiwa katika nchi kama hizi ambazo hazitawaliwi kiislamu, kwani kuondoa udhia katika nchi kama hizi kunataka elimu na maarifa mapana tena kwa kuangalia faida na hasara.
Nne, ningekuwa mimi ndio mwenye mamlaka, huyo mtu ningemuachia, ila najua Allah aliye juu hatomuacha hivi hivi, atamlioa stahiki yake tu kwa namna anayoijua Allah.