Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Manka wangu nakupenda,
Hakyamungu nakupenda,
Yesu na maria nakupenda,
Yani ninavyokupenda niko tayari kwenda kuiba dukani kwa urassa nikupe chochote unachotaka.

Wako Mangi.
Haha

Just

Haha
 
Manka wangu nakupenda,
Hakyamungu nakupenda,
Yesu na maria nakupenda,
Yani ninavyokupenda niko tayari kwenda kuiba dukani kwa urassa nikupe chochote unachotaka.

Wako Mangi.
Ngastukaaaaa
 
Jicho lako ni kama kobe,mgongo wako mithili ya mamba mtoa roho!
E mupenzi nikujutiae,uhali gani huko jehanam..?
figure yako namba tasa,ni kama nafungua kurasa
uangaliapo mboga huchacha,kwa tabasam swadakta!.
 
[emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji182] [emoji182] [emoji182] i ddint expect this?!! thank you bae[emoji3] [emoji3]
 
HUBA MITHILI YA RUBA,MAHABA BILA SHULUBA.

IDHILALI BILA SHABA,KIKUKOSA MAHABUBA.

NAPENDA UKIWA SABA,KIUNGO NANE NAKABA.
Najua unaogopa, napia unamashaka
Penzi tamu nitakupa, kamwe huwezi kuchoka
Pili mimi ni kibopa, nyumba gari nitakupa
Ni tayari kwa chochote, nimpokonye mshana.
 
😀 Dah!
Kwako Hassan Mambosasa

Majira hubadilika,
Miaka inasogea,
Nyasi nazo hunyauka,
Mimea kujiozea,
Lakini nina hakika,
Wewe hutonipotea.

Wewe unayo thamani,
Ya upendo ulo kweli,
U pekee duniani,
Ambaye wastahili,
Kukupa yalo moyoni,
Kwa pendo letu wawili.

Mi nawe twapendezana,
Kwa pendo lililoshiba,
Hakika tunatoshana,
Kwa dhati pia kwa huba,
Pendo tunalopeana,
Linayo tele mahaba.

Wanipa mie furaha,
U zawadi maishani,
Kuwa nawe kuna raha,
Ni raha iso kifani,
Nafurahi kwa madaha
 
Najua unaogopa, napia unamashaka
Penzi tamu nitakupa, kamwe huwezi kuchoka
Pili mimi ni kibopa, nyumba gari nitakupa
Ni tayari kwa chochote, nimpokonye mshana.
Moyo wangu, moyo wangu unauadhibu,
Basi fanya japo taratibu!
Niondolee madhila yaliyozidia hesabu,
Utaniuwa mwana wa mwenzio!

Taratibu, twende taratibu basi taratibu,
Nitese tu kidogo ukipata sababu!
Ukizidisha moyo wangu wauharibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!
 
Kwako kipenzi changu moneytalk.

Wangu kipenzi mzuri, mfano kama hariri.

Wewe kwangu ni habari, kifani chako dinari.

Zipite enzi dahari, ubaki wangu uturi.

Mola akujaze kheri, akuepushe na shari.
Ewaaaa acha niringe mie kwakukupata kipenzi cha moyo wangu,unanifanya kila siku nakuona mpya,nakupenda wewe mwifwa wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…