halihitaji hirizi,wala usijisumbuwe
watakupiga fitizi,wataka wakuganguwe
hao wote ni walozi,nimekupenda mwenyewe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi
halihitaji hirizi,nimekupenda mwenyewe
sitaki masimulizi,,juu yako niambiwe
kwa hila za kibazazi,kwangu zitangonga jiwe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi
halihitaji hirizi,tulia kwangu utuwe
tuama nita kuenzi,kama baba na mwanawe
moyo umekufa ganzi,stamani penginewe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi
halihitaji hirizi,nikoseapo upowe
nijapo itaka razi,msamaha usikawe
niaminini laazizi,furaha yangu ni wewe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi
halihitaji hirizi,kikubwa ni thaminiwe
kwako niwe mwenye hazi,mfano wangu pasiwe
kwenye wako usingizi,sura yangu ndio iwe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi.
Kwako nimekufa nimeoza usinitese tafadhali
Mshana Jr