Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

halihitaji hirizi,wala usijisumbuwe

watakupiga fitizi,wataka wakuganguwe

hao wote ni walozi,nimekupenda mwenyewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,nimekupenda mwenyewe

sitaki masimulizi,,juu yako niambiwe

kwa hila za kibazazi,kwangu zitangonga jiwe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,tulia kwangu utuwe

tuama nita kuenzi,kama baba na mwanawe

moyo umekufa ganzi,stamani penginewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,nikoseapo upowe

nijapo itaka razi,msamaha usikawe

niaminini laazizi,furaha yangu ni wewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,kikubwa ni thaminiwe

kwako niwe mwenye hazi,mfano wangu pasiwe

kwenye wako usingizi,sura yangu ndio iwe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi.


Kwako nimekufa nimeoza usinitese tafadhali Mshana Jr
Mshana anatumia hirizi siyo siri
 
Kwa sababu umependa wazi wazi, basi na sisi tunamuweka apate kuona.
Kudunda wanawake wazi wazi ,halafu unategemea kuna watu hawakuona.
Nataka umwagwe wazi wazi, ili ujue kuwa mwanamke ni ua na si ngoma.
Aiseee ngoja niweke kambi hapa
 
Back
Top Bottom