MTV Mama Awards 2016: Watanzania waambulia patupu, Nigeria na South Africa wang'ara

MTV Mama Awards 2016: Watanzania waambulia patupu, Nigeria na South Africa wang'ara

Diamond katoa nyimbo ngapi bora mwaka huu, na wizkid katoa nyimbo ngapi bora mwaka huu?
Ifike mahali wasanii wa bongo wasitoe nyimbo kama mashindano, we want some quality songs na zinazodumu kwa muda mrefu.
Wizkid hatoi nyimbo ovyo ovyo ila akitoa anatoa jiwe la maana, namkubali sana tekno maana anatoa nyimbo mfululizo lakini mawe. Ila hawa ndugu zetu bongo, wanatoa nyimbo ovyo ili kuziangusha nyimbo za wasanii wengine na huo ndio ujinga wao.
 
Niliacha kumshabikia ndomo kutokana na uswahili wa familia yake na hiyo sababu ya matusi kwenye mitandao imempotezea sana mashabiki dai na ikuja baada ya kumdharau yeye na familia yake
 
Hili lilijulikana kwa hawa wabana pua wetu kuwa kuna siku watakuja kuumbuka kazi ya kurushiana madongo hakuna hata mmoja anayeweza kunata na beats liveee si timu ya kule wala ya pale.

Hivi hawamuoni Cristian Bela anavyonata na beats hata ukimkurupusha usingizini utampenda tu na sauti.

Wengi wa hawa wasanii hawakuimba mitaani kwenye bendi au kwenye kwaya au kaswida wala hawakuanza kuimba toka wakiwa watoto kama wale mastaa wa Marekani waliokuja kuchomoza kwenye Pop Idol, America Idol etc.

Kwa kuwa wameamua kuwa wanamuziki wasione aibu, kwanza wana pesa chafu, wawatafute wazee wetu wa muziki wajifunze kuimba liveee watafunika madhaifu yao wakiwa na bidii.

Huu ujanja ujanja wa kupika pika studio hautawafikisha mbali.
 
Pili, waachane na mambo ya singles au collabo, inawaletea pesa chafu, lakini kipimo cha mwanamuziki bora ni Album iliyo hit na ya kwake, na hakuna kingine. Maana ndiyo identity yake.

Ama sivyo wakubali kuwa watakuwa wanatengeneza mpunga kwa singles na collabo lakini vikombe hawatachukua maana hiyo ni sawa na " chenga twawala".

Sumu ya mwisho ni kuondoa huu ujinga wa timu fulani unless kama unawasaidia kutengeneza mpunga sawaa! Lakini hautawafikisha kokote kwenye tuzo za kimataifa.
 
Ki JPM zaidi
Screenshot_2016-10-23-02-32-38-1.png
 
Back
Top Bottom