MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Kuna taarifa kuwa basi la Shule ya King David iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani limepata ajali mbaya iliyopelekea vifo vya wanafunzi na dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina moja Hassan anayekadiriwa kuwa na umri wa mika (54-60)

Miili imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Ligula na majeruhi wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kama Kuna mzazi au mlezi mwenye mtoto huko afuatilie kinachoendelea. Pole kwa wafiwa na majeruhi, Mungu mwenye Enzi awaponye.

======
TAARIFA YA AWALI YA JESHI LA POLISI

Gari namba T207 CTS la Shule ya Msingi na Sekondari ya King David iliyopo Mtwara limepata ajali maeneo ya Mji Mwema, leo Julai 26, 2022 na kusababisha vifo vya Wanafunzi, dereva na Msaidizi.

Msaidizi wa Kamanda wa Polisi wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa taarifa za awali waliofariki ni Wanafunzi Nane, Dereva mmoja na Mwangalizi wa Wanafunzi.

Naye RPC mwenyewe ACP Nicodemus Katembo alipopatikana alisema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Ligula lakini watatoa taarifa zaidi baadaye.

UPDATES: 1130HRS

Watu kumi wamefariki dunia wakiwemo wanafunzi nane wa shule ya King David, huku wengine 19 wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kufeli break na kutumbukia kwenye korongo, Mji Mwema mkoani mtwara. Kamanda wa polisi mkoani humo, Nicodemus Katembo amethibitisha

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Kupitia akaunti yake rasmi Twitter, Rais Samia ameandika hivi

''Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa shule ya msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbulikia shimoni. Nawapa pole wafiwa, Mkuu wa Mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu Marehemu na kuwaponya majeruhi.''

m1.jpg
m2.jpg

1658819812830.png


1658820287140.png
 
Kuna taarifa kuwa basi la shule ya King David iliyoko manispaa ya Mtwara Mikindani limepata ajali mbaya iliyopelekea vifo vya wanafunzi na dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina moja Hassan anayekadiriwa kuwa na umri wa mika (54-60)
Oooh ni taarifa ya kustusha na kuhuzunika.

Walale pema malaika wetu pamoja na Dereva.

Mungu awajaalie majeruhi nafuu ya haraka
 
Mungu awenanyi, awape matumaini ,Wahanga wote .
 
Kuna taarifa kuwa basi la Shule ya King David iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani limepata ajali mbaya iliyopelekea vifo vya wanafunzi na dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina moja Hassan anayekadiriwa kuwa na umri wa mika (54-60)...
R.I.P kwa wanafunzi wote, dereva na msaidizi wa wanafunzi
 
Hili swala la gari za shuke inabidi serikali ianze kukagua magari yanayopereka watoto wetu, am sure watapata zaidi ya 80% nibmabovu na hayafai kuingi barabarani,

Kwa uzoefu wangu, naonaga wamiriki wa shule huwa wanaenda gereji kutafuta gari la kufufua na wamekuwa wakipata gari na tair zake hukohuko, ni shida sana
 
Back
Top Bottom