MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Pole kwa wazazi na wote waliofikwa na msiba huu,, Mungu awapumzishe mahali pema peponi
 
Wazazi wengi wanalipa pesa nyingi watoto wao wasome hizi shule zenye school bus lakini wengi hawafanyi ufuatilizi wa usalama wa huo usafiri kwa watoto wao.

Mungu awapumzishe wote waliopoteza maisha kwenye ajali hii.
 
Seat belt kwa dereva au abiria wa nyuma,
Maana kwa kawaida nchi yetu seat belt ni kwa dereva na mtu mbele

#Pole kwa wafiwa
Kwa dereva na abiria, tena hizi Schoolbus wafanye sharti ni lazima ziwe na seat belt alafu zisiwe zile gari zilizochoka choka ndo zikafanywa schoolbus
 
Poleni sana wazazi wa watoto walioaga dunia. Gari imejichokea ndo inafanywa School bus haina hata seat belt
Mkuu Kuna magari mangapi yamechoka hayana seatbelt na ni school bus? Ikifika imefika tu. Mungu awarehemu.
 
Poleni wazazi na walimu kwa msiba mzito uliowakumba, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu sana cha kuwapoteza watoto wetu wapendwa.
Mungu azipokee roho zao.
Hakika inaumiza na kusikitisha sana.
 
Kuna taarifa kuwa basi la Shule ya King David iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani limepata ajali mbaya iliyopelekea vifo vya wanafunzi na dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina moja Hassan anayekadiriwa kuwa na umri wa mika (54-60)....
Ni uchungu sana kupoteza idadi kubwa hiyo ya watu.
Palifanyika ukaguzi wa magari ya shule ilipotokea ile ajali Arusha, na kama kawaida hali ikapoa na wenye magari hayo ni wazi wamejisahau tena. Kwa picha tu hii gari iliyopata ajali leo na kusababisha vifo hivyo inaonekana ni chakavu
 
Mungu wangu! so sad,malaika Hawa mungu uwapumzishe kwa amani,poleni sana wazazi ,ndugu ,jamaa na marafiki kwa ujumla.
 
changamoto hizi za ajali sijui hata zitaisha lini ?
poleni sana shule wazazi na wote walioguswa.
mungu awajalie pumziko jema la milele .
 
Hii mbaya sana. Pole kwa wafiwa. Nini kifanyike? Kwa wenzetu gari za wanafunzi hupewa upendeleo wa pekee sana. Tunaweza kufanya kitu gani kuzuia misiba ya watoto kama hii?
Kiwepo kitabu maalum katika Kila gari ambacho Trafic watakagua seat belts za school Bus na kusign, pia ule utaratibu kwa lazima school bus zote zipelekwe garage Kila mwezi uzingatiwe, kwa kupeleka Traffic mmoja Kila garage ili ahakikishe gari zinatengenezwa
 
Hizi taaratibu zikianza katikati huko zinapotea.

Unakumbuka ya Lucky Vicent?
 
Wazazi wengi wanalipa pesa nyingi watoto wao wasome hizi shule zenye school bus lakini wengi hawafanyi ufuatilizi wa usalama wa huo usafiri kwa watoto wao.

Mungu awapumzishe wote waliopoteza maisha kwenye ajali hii.
Kuna Mzee mmoja tulisoma na mtoto wake O-level,yule Mzee alikuwa anafika Kila me kutazama mazingira,anaingia mpaka vyooni kuona mwanae anaishi vipi
 
Back
Top Bottom