MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Inaonekana kule upande ilipoangukia imejibamiza kwa nguvu na body likarudi huku upande wa dereva na kuwabana ukiangalia kwa makini.

Wapunzike kwa amani Marehemu wote waliotangulia kwenye ajali hiyo na maheruhi Mungu awasimamie wapate kupona haraka. [emoji17]
Hapo walibebana mzee ndio tatizo hyo hiace afu jumla wapo 29... Wamekaaje humo
 
Inalilah wainalilah Rajiun jaman Pole kwa familia za waliopatwa na janga hili.😢
 
Watu 10 wakiwemo wanafunzi nane wa Shule ya Msingi ya King David iliyopo mkoani Mtwara wamefariki dunia katika ajali ya gari ya shule hiyo iloyotokea katika eneo la Mjimwema, Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni gari kufeli breki.

Katika ajali hiyo, dereva na mwalimu mmoja nao pia wamefariki, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa amethibitisha.

Chanzo: AZAM TV NEWS
 
Poleni sana wafiwa!!
Kwa upande mwingine unaeza sema mwenye shule katimiza shughuli yake
 
Hii habari bora hata vyombo vya habari visiirushe kwenye taarifa ya HABARI USIKU italeta TAHARUKI NA HOFU MIOYONI
 
Poleni wazazi kwa kumpoteza watoto. Pumzikeni salama watoto wetu.
 
Ndio nakumbuka Dear, ile ajari ndio ilisababisha serikali itowe Amri gari ziende garage Kila mwezi na zilipelekwa kweri, naona yule Waziri alipoondoka na utaratibu ukafa
Ila madereva wa hizo gari za shule nao Vimeo sana! Yaani unajua kabisa gari lako bovu,kwa Nini ukimbize speed badala ya kwenda nalo adoado hadi ufike salama!!!? Gari bovu ni la kubembelezwa Kama huna pesa ya kulipeleka garage,ukitaka ma mbio peleka gari lako garage ili lichekiwa kwenye kila sector Kama liko OK!!
 
Duh! taarifa mbaya sana hii...

Lakini hadi sasa najiuliza hiyo ajali imekuaje imeua watu wengi hivyo, ukitazama picha ni kama impact sio kubwa na gari imeingia kidogo tu katika korongo...
Binafsi nilipooana picha niliamini hakuna madhara yoyote hasa kifo.

Ila si unajua ukaaji wa Watoto wetu kwenye hizo School Bus...kwanza huwa hawakai...

Unakuta Wemesimama kwenye siti...Wengine wamesimama wanaongea na wenzao wapo siti za nyuma huko....

Matokeo yake ndiyo kama hivyo, Ajali ikitokea Wanaumia au kufariki kwa wingi..
 
Kuna shule hapa Iringa inatumia yale madaradara yanayopakia abira wakati wa mchana na mbaya zaidi kila siku hayo magari yanapita katika check point ya polisi Kihesa kilolo na baada ya hapo yanapita kwenye mteremko mkali sana ambao hata TANROAD wameweka kibao kua ni mteremko hatari.
 
Seatbelts zinaweza kusaidia sana. Lakini ukiangalia school buses za wenzetu huwa hazina seatbelts. Watoto wengine wadogo sana. Lakini barabarani wana sheria ambazo zinayapa magari ya wanafunzi. Mfano gari ya wanafunzi ikisimama kupakia wanafunzi, gari zingine zote zinasimama.
Upo sahihi, wale watoto wa kindergarten Ni ngumu kuwafunga belts
 
Tena nisisikie naambiwa michango ya study tour bora tununue jogoo tutafune
 
Back
Top Bottom