Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Askari aliekimbia ni Zabroni ndio mtu wao wa connection, mara nyingi anakaa kwenye Bar ya shooters akichunguza nani ana pesa za kutosha na kuwatonya kundi lake la kigaidi.
Aiseee kwahiyo hajulikani yuko wapi?
 
Iko kiasi cha pesa kipoje hapo? Hiyo shilingi 80 ya mwishoni inamaana ipi?
 
Yale yaleeee Ya Hamza . inatia hasira sana wamemuua kwasababu wameogopa kwamba wakimuacha hai atakuja kuwamiminia risasi kama zile za Hamza.
Hamza alikosea sana kuwaua hawa wajinga bila kutoa taarifa angetoa taarifa kwanza kuwa anaenda kuua sababu wamemdhulum pesa zake. Ukitaka kujua polisi ni wezi ukishikwa pale kaunta ukiacha mkanda mzuri hauwezi kuupata kamwe.
 
KUTOKA KWA VYANZO MBALIMBALI, Huu ni mtiririko wa matukio ya Mauji hayo.

NACHINGWEA.....
Kijana mmoja ambaye ni mkazi wa NACHINGWEA, LINDI ambaye pia anajihusisha na biashara ya madini, mwishoni mwa mwaka uliopita yaani 2021, alipata bahati ya kupata madini yenye thamani kadhaa, hali hii ilimpelekea kupata connection moja na mzungu ambaye alimuuzia madini hayo na kupata Dola za kimarekani Elfu kadhaa.

Mara baada ya kupata kiasi hicho cha fedha, ilibainika wazi kuwa asingeweza badilisha pesa zile ktk wilaya ya Nachingwea, hivyo akaona bora aende MKOANI MTWARA ambako ndio makao makuu ya benki karibia zote kwa Mikoa ya Kusini. Mkoa ambao pia wanapatikana ndugu zake kadhaa pia ambapo mjomba wake anayejishughilisha na ukatishaji wa tiketi za magari katika stendi ya Mkanaledi Mjini hapo.

Mkoani MTWARA...
Mara baada ya kuwasili mjini hapo, alimjulisha Mjomba wake huyo juu ya kile kilichompeleka hapo ili awe msaada wake. Hapo wakachagua Benki ya NMB kwenda kubadilishia Fedha hizo.

NMB MTWARA....
Mara baada ya kufika benki hapo, alipokelewa na Mhudumu wa benki mmoja wa kike, ambapo alimshughulikia kama mteja mpaka kufanikisha kupata fedha zinazokadiriwa kufikia au kuvuka mil 70 za Tanzania.

TATIZO LINAANZA....
Mara baada ya kuchukua Fedha hizo, mhudumu huyo wa NMB alimuuliza kijana yule kuwa anataka kurudi LINDI siku ile ile, ambapo alijibiwa na kijana huyo kuwa ndio anataka kurudi kwao.
Hapa sasa yule mhudumu wa BENKI akamshauri yule kijana asiondoke na pesa zote zile kwa siku ile, ni bora atafute Lodge nzuri apumzike ili kesho yake aweze kuondoka kwa amani zaidi. Kijana yule alikubali na kwa ugeni wake akaamua kumuuliza Mhudumu yule ni Lodge ipi nzuri kwake, ndipo akaelelezwa na akaenda huko ambapo pia alimjulisha mjomba wake.

[emoji117][emoji117][emoji117] INASEMEKANA SASA YULE MHUDUMU WA NMB ALIWATONYA MAMWELA (POLISI) KUWA KUNA ISHU YA PESA NDEFU NA MUHUSIKA YULE YUPO LODGE FULANI MJINI PALE.

LODGE....
Mara baada ya kuwasili Lodge hiyo, hapo ndipo tatizo lilianza rasmi, usiku alifuatwa na Polisi kadhaa ambapo walimtishia na kuchukua vitu vyake vyote. Waliondoka nae mpaka kituo kikuu cha polisi mjini hapo. Huku akipewa masharti ya kuwa akiulizwa kwanini amekamatwa aseme alikuwa anendesha pikipiki hivyo alivunja sheria za barabarani. Inasemekana sasa alipewa Laki moja aondoke na atarudi tar 6 mwezi huu. Lakini inasemekana askari wale kutokana na tamaa zaidi ya fedha walimchukua mpaka NACHINGWEA na wakamchukulia pesa zake zingine na kumuacha.

ANARUDI KITUONI...
Kama alivyoambiwa arudi kituoni hapo, alirudi kituoni hapo akiwa na mjomba wake ambapo sasa alikuja kufuata vitu vyake alivyoporwa ikiwa sambamba na pesa zake. Mara baada ya kufika askari wale walimchukua kwa madai wanaenda kumhoji. Wakati huo mjomba wake akiwa nje ya kituo hiko akimsubiri mpwawe huyo.
Dakika zikapita, masaa yakapita, hatimaye siku ikaisha bila kumuona mpwa wake huyo.

Siku ya pili, mjomba alirudi polisi kujua hasa mpwa wake alikopelekwa, lkn hakupata majibu sahihi. Hali hii ilipelekea kutoa taarifa NACHINGWEA na hapo familia ikaenda kwa Mkuu wa wilaya ya NACHINGWEA ili wapatiwe msaada wa kumpata ndugu yao huyo. Taarifa zilifika mbali zaidi ambapo sasa uchunguzi ulifanyika kubaini nini tatizo halisi.

YAGUNDULIKA KUUAWA...
Watoa taarifa wanadai ikagundulika kuwa kumbe alichukuliwa na kwenda kuuawa tena kwa kupigwa sindano ya Sumu, kisha mwili wake kwenda kufukiwa kusikojulikana.

ASKARI WASAKWA WAKAMATWA.
Maafisa waandamizi wa Polisi mkoani hapo wamekamatwa wapo gereza laLILUNGU mjini hapo, MKUU WA KITUO, OC-CID na askari kadhaa, pia yupo askari amekimbia lkn taarifa zinadai pia mhudumu wa NMB anasakwa kuunganishwa kwenye kesi hiyo ya kikatili zaidi.

Askari mmoja ajiua...
Inasemekana mara baada ya kesi hii kujulikana, basi askari mmoja wapo mara baada ya kukamwatwa na kuwekwa mahabusu alijiua kwa kujinyonga kwa kutumia shati lake.

Hadi sasa bado familia hawajakabidhiwa mwili wa kijana wao.
KUTOKA KWA WASIMULIAJI WA MKONI MTWARA NA VYANZO VYA HABARI KAMA ITV, MWANANCHI NK
Japokua wewe ni ling'ombe tu, Ila huu mtiririko upo vizuri na wa ukweli
 
Polisi wengi ni wauaji sana wa raia wema ila basi tu mambo yao mengine yanaishia chini ya kapeti
Yule jamaa hamza aliyeuliwa pale ubalozi wa ufaransa lazima kulikuwa na kitu kama hiki ila aliamua kuchukua njia yake nyingine kulipiza kisasi labda naye angekwenda kudai madini yake angeuwawa akaamua afanye vile alivyofanya.
Polisi jirekebisheni mnazulumu sana raia wema

Labda walimwambia tutakuuwa akajiongeza
 
View attachment 2095563


Jeshi la Polisi Mkoani limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba (7) kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kijana Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Mauaji hayo yamefanyika baada ya marehemu Mussa Hamisi kudai fedha zake shilingi Milioni 33,748,980 ambazo maafisa hao wanadaiwa kuzichukua kutoka kwa kijana huyo baada ya kumfanyia upekuzi.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera amesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari wilaya ya Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango -Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza -Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga- Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Source: Kusiniyetu Online Tv.

46D5EEC8-911F-4050-B44C-6DCE03DD125D.jpeg
 
Mkuu wao ajiuzuru kwa aibu hii
Haiwezekani askari wote hao na bado yupo yupo tu
Hawa wana damu nyingi sana ambazo zinajificha na hizi za wazi
 
Waandishi wa habari walitaka kupata Maelezo ya kilichosababisha mfanyabiashara wa madini afariki akiwa mikononi mwa polisi lakini IGP Sirro akasema yeye yuko kwenye ziara ya Waziri hivyo ni vema waandishi hao wakamuuliza Waziri.

Source: ITV habari
Siro ni kada wa ccm hana jibu zaidi ya kusema uwongo,policeccm imeua watu wengi sana chini ya utawala wa meko na hangaya
 
Utakuta hapo walijiwekea mgao wa 4,820,682
Tamaa imewaponza wanaenda ishia jela na kuacha familia ikiteseka kwasababu ya hela hiyo.
Hapo bado roho ya marehemu haitowaacha salama .
Dah!Mungu tuepushie mana tunakoelekea sasa ni kubaya mauaji yamezidi.
Yameanza kwa raia kwa raia sasa ni walinda usalama wa nchi kwa raia.
Sijui tukimbilie wapi penye ahueni mana tunaowategemea nao wameanza kukengeuka.
 
Hawa wanatakiwa waje watandikwe shaba pale uwanja wa mkapa live na siku hiyo inakuwa mapumziko ili kutoa funzo na inakuwa live tv zote.
 
Mama samiah bado ana entertain huu upuuzi? Ni vyema akamdalisha haraka SIRRO maana umri umemtupa mkono hivyo kila kinachofanyika yeye anaona ni sawa tu…

Jeshi hili chini ya mzee Nyakoro limepoteza ufanisi wake kwa 100%
Toka ameingia madarakani kuna vijana zaidi ya 10 hawajulikani walipo,yeye na meko mulemule
 
Back
Top Bottom