Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

View attachment 2095724

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7...
Ya Zombe na wenzake yamejirudia
 
Ukweli ni kwamba tuna jeshi la polisi ambalo limejaza majambazi.

Kuna wakati mpaka wananchi tunasema aheri kusingekuwepo polisi, hawa vibaka tungepambana nao hata kwa rungu kuliko haya majambazi yanayotumia bunduki SMG na AK47, tena yakiwa kwenye gari za polisi. Tena yanaua na kupora yakiwa yamevaa nembo ya Taifa.

Maiti nyingi zinazotupwa ni mauaji yanayofanywa na haya majambazi polisi.
 
Huyo alieuliwa huenda ni mtoto, ndugu au rafiki wa polisi mwenye cheo kizito sana kama rpc au ocd ndio maana jambo limekuwa zito hivi, na hao waliomuua hawachomoki hapo. ila ingekua ni kivingine ingepita tu fasta
 
Huyo alieuliwa huenda ni mtoto, ndugu au rafiki wa polisi mwenye cheo kizito sana kama rpc au ocd ndio maana jambo limekuwa zito hivi, na hao waliomuua hawachomoki hapo. ila ingekua ni kivingine ingepita tu fasta
No mkuu nikupaza sauti ndugu kutokuwa waoga.
 
Muuaji na mporaji wa fedha za watu hawezi kuwa sawa.

Hapo kuanzia RPC, RCO na hao wengine, wote ni syndicate ya ujambazi.

Si uliona hata ile syndicate ya Kingai, Jumanne, Goodluck na Mahita?
Ukiacha RPC nashindwa elewa..
RCO ameshindwa vipi kujumuishwa?! Pa1 nae Staff officer ukizingatia tukio limefanyika mkoa mwingine?!
 
Katika nchi yetu hii kumkuta kijana wa miaka 25 ana milioni 33 si jambo dogo, kijana alikuwa ni mfanyabiashara wa madini lakini huenda vitu kama mtaji wa biashara alipigwa jeki na mzazi.

Huenda kijana huyo ni mtoto wa mtu mzito kama Rpc wa mkoa fulani, Ocd, mwanajeshi mwenye cheo, mwanasiasa, n.k.

Kiufupi huenda kuuawa kwa kijana huyo mdogo kulifanywa bila kujua mzazi wake ni nani, Uchungu wa mtoto anaeujua ni mzazi aisee!! kuna watoto sio hata wa kuwagusa maana kitachokukuta hata kazi yako unayoona inakulinda haitakusaidia.
 
Back
Top Bottom