Muda ni protocol ya usafiri kwenye msiba wa Malkia, kila kiongozi angetumia usafiri wake kungekuwa na foleni

Muda ni protocol ya usafiri kwenye msiba wa Malkia, kila kiongozi angetumia usafiri wake kungekuwa na foleni

Hii ndo ilikua hoja ,na ndo maana mjadala umekua mkubwa, watu wasijifiche kwenye kichaka Cha kuita watu sijui wajinga, watu wanaelewa why wanahoji na why imekua story, hasa KWa viongonzi watokao afrika
Kabisa mkuu,utashangaa akirudi bongo ataenda kupokewa na viongozi 50 airport kila mmoja na V8 lake,kwa nini wasipakiwe kwenye basi
 
MARAIS WA AFRIKA KUPAKIWA KWENYE BUS NI DHIHAKA?

Na Abbas Mwalimu
(0719258484).

Jumatatu tarehe 19 Septemba, 2022.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu viongozi wa Afrika kupakiwa kwenye usafiri (bus) wa gari moja wakati wakielekea kwenye ibada ya mazishi Westminster Abbey.

Swali ni je walikuwa viongozi wa nchi za Afrika pekee?

Kwa nini matukio makubwa au mikutano hutumia mabasi?

Kimsingi hawakuwa viongozi wa Afrika pekee waliopanda kwenye mabasi bali viongozi wengi walioalikwa walitumia mabasi.

Tukumbuke kuwa tukio lile lilikutanisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali na Wawakilishi zaidi ya 500 kutoka nchi na taasisi mbalimbali duniani hivyo maandalizi ya usafiri yalihitaji kuratibiwa vizuri.

Kimsingi baadhi ya viongozi waliopanda mabasi ni Waziri Mkuu wa Ireland Micheál Martin, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, Mfalme Abdullah II wa Jordan na mkewe Malkia Rania.

Aidha wengine waliopanda mabasi ni Rais wa Malaysia Agong Al-Mustafa Billah Shah, Rais wa Singapore Halimah Yacob, Mfalme wa Japan Naruhito, Rais wa Poland Andrzej Duda, na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Vilevile, Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden na mkewe Silvia, Malkia Margrethe II wa Denmark, Mfalme Felipe na Malkia Letizia wa Hispania, Rais wa Italia Sergio Mattarella, Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Mfalme Harald wa Norway na mkewe Malkia Sonja nao walipanda mabasi.

Matukio makubwa kama mikutano au msiba kama ule wa Malkia Elizabeth II ambao ulikutanisha viongozi wengi njia rahisi ya kuwafikisha katika tukio kwa muda uliopangwa ni kutumia usafiri wa pamoja.

Tufahamu kuwa matukio ya namna ile yanaongozwa na itifaki (protocol) na miongoni mwa mambo muhimu katika protocol ni muda.

Sasa tujiulize kama kila kiongozi angepangiwa muda wake na msafara wake (motorcade) hali ya msongamano ingekuwaje?

Ni muda gani ungetumika kukamilisha idadi ya viongozi wote kufika Westminster Abbey?

Hatudhani kuwa muda wa ibada ya mazishi ungeathiriwa na misafara ya viongozi?

Ifahamike kuwa katika matukio kama lile na yafananayo na lile utaratibu wa usafiri, malazi na usafiri huratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi husika.

Katika muktadha huu suala la usafiri wa viongozi wa nchi na serikali liliratibiwa Ofisi ya Masuala ya Kigeni, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (Foreign, Commonwealth and Development Office/ FCDO) ya Uingereza.

Utaratibu huu hufanyika ili kurahisisha usalama wa viongozi mbalimbali duniani kwa wakati mmoja na hii ni kwa sababu itifaki na usalama wa viongozi ni mambo yanayoenda pamoja na kamwe hayawezi kutenganishwa.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi kupakiwa kwenye mabasi kwa sababu hata katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola mwaka 2018 (CHOGM2018) uliofanyika London na Windsor viongozi kutoka nchi zaidi ya 54 walipakiwa kwenye mabasi kwenda na kurudi kwenye mikutano kwa siku zote za mikutano.

Hayo yamekuwa yakifanyika hata Tanzania pia labda kwa bahati mbaya wengi huwa hawafuatilii.

Hivyo si dhihaka kama wengi wanavyodhani bali ni sehemu ya utaratibu katika kurahisisha usalama wa viongozi.

Zaidi, kitendo hiki cha kuwapatia usafiri mmoja viongozi hutoa nafasi kwa viongozi kuyasoma mazingira ya nchi au eneo husika na wao kupata muda wa kuchanganyika na kubadilishana mawazo ambapo kitendo hicho huitwa poding.

Wenu:

Abbas Mwalimu
(Facebook|Instagram|Twitter|Clubhouse).

+255 719 258 484.

Uwanja wa Diplomasia
(Facebook|WhatsApp).
View attachment 2362139View attachment 2362140View attachment 2362141
Ni.ngumu mtanzania kumuelewesha. Ubaya watanzania tuna jiona tuna jua kila kitu. Mimi sijaona kosa lolote kwa viongozi wetu na mataifa mengine kupanda bus. Ukichoandika mkuu umeelezea vzr. Kama watu hawatakuelewa basi wana mtindio tu wa ubongo. Sio kila jambo la.kubisha. Viongozi zaidi ya 500 wote na misafara yao au hata na gari moja moja aisee pasingetosha kwa kweli
 
Ni.ngumu mtanzania kumuelewesha. Ubaya watanzania tuna jiona tuna jua kila kitu. Mimi sijaona kosa lolote kwa viongozi wetu na mataifa mengine kupanda bus. Ukichoandika mkuu umeelezea vzr. Kama watu hawatakuelewa basi wana mtundio tu wa ubongo. Sio kila jambo la.kubisha. Viongozi zaidi ya 500 wote na misafara yao au hata na gari moja moja aisee pasingetosha kwa kweli
Ume quote vizuri " ujuaji" ni tatizo linakuja kwa kasi hapa nchini
 
Walisha wahi kuja Marais hata 10 kwa wakati mmoja hapa kwetu?
Unaukumbuka mkutano wa Sulivan kipindi cha JK,
AICC arusha huwa inajaza mikutano ya AU marais zaidi ya 50
Tuje nchini mawaziri siku ya msiba wa Jpm kwa nini hawakupakizwa kwenye mabasi,hatupingi mabasi bali tunataka wayatumie hata huku
 
Kabisa mkuu,utashangaa akirudi bongo ataenda kupokewa na viongozi 50 airport kila mmoja na V8 lake,kwa nini wasipakiwe kwenye basi
Halafu barabara zote zitafungwa na njia nzima watatapakaa maaskari wenye silaha nzito nzito utadhani wanaenda vitani.

Ni wachache sana wataelewa kwa nini maRais wetu kupakiwa kwenye basi kumekuwa gumzo. Miunguwatu kwenye basi!
 
Ila kweli kwa zile nyuzi na comments za jana, sisi weusi tuna shida sana sana. Yaani Raisi wa Ujerumani kapanda basi na raia wake wala hawana shida. Waziri mkuu wa New Zealand, Raisi wa Italia, Raisi wa EU n.k... vile vile na huoni malalamiko yoyote. Ndio utajua wengi hatuna exposure, tuna uelewa mdogo, tunapenda ufahari. Hizi ni dalili za udumavu wa akili na sababu kubwa ni lishe duni kabla na baada ya kuzaliwa na wakati wa makuzi yetu.
Shida ni kwamba kwanini wakirudi nyumbani msafara unakuwa na magari 80+,kwanini yasipatikane mabasi mawili na magari manne madogo kwenye Convoy??
 
Halafu barabara zote zitafungwa na njia nzima watatapakaa maaskari wenye silaha nzito nzito utadhani wanaenda vitani.

Ni wachache sana wataelewa kwa nini maRais wetu kupakiwa kwenye basi kumekuwa gumzo. Miungumtu kwenye basi!
Naona akili zenu zimeathiriwa na mazingira tuliyopo, na mazoea, ni kama vile hamkuwahi kudhania iko siku mtamuona Rais kwenye bus!.

Kama mngejua Samia yupo nchi nyingine, yenye sheria na taratibu tofauti, sidhani kama mngeshangaa kwake kupandishwa bus.

Binafsi ningeshangaa Samia kupandishwa bus, kama ingefanyika hivyo ndani ya hizi nchi zetu zinazofanana tabia ambazo marais wao walikuwa kwenye bus moja na Samia.

Simply mnachotetea nyie, ni kama vile mlitaka Rais wetu akavunje sheria na taratibu za wengine, ambapo naamini kama angefanya hivi, mngesema pia.
 
Halafu barabara zote zitafungwa na njia nzima watatapakaa maaskari wenye silaha nzito nzito utadhani wanaenda vitani.

Ni wachache sana wataelewa kwa nini maRais wetu kupakiwa kwenye basi kumekuwa gumzo. Miunguwatu kwenye basi!
Kama hawajapata cha kujifunza hawatajifunza
 
Back
Top Bottom