Muda ni protocol ya usafiri kwenye msiba wa Malkia, kila kiongozi angetumia usafiri wake kungekuwa na foleni

Siyo kwamba watu hawana exposure au udumavu wa akili.Tatizo hapa ni hawa viongozi wa afrika na matumizi mabaya ya fedha za umma.mfano Rais kuwa na msafara wa magari zaidi ya 40 ya nini sasa tena v8.Ukiangalia ulaya wao hawana hiyo mbwembwe,misafara yao haizidi magari kumi.yaani Nchi tajiri zinatumia rasilimali vizuri kuliko viongozi wa afrika ndiyo maana nchi ulizozitaja kama ufaransa nk wananchi wake hawajawaponda viongozi wao tofauti na na wa huku afrika
 
Kwani viongozi wahusika wamelalamika? Shida watanzania ni wanafki sana utafikiri wanawajali viongozi wao wakati kila siku wanamtukana mama yetu humu mtandaoni. Hata hivyo uongozi ni utumishi ni kupata fursa ya kutafuta ubwana mkubwa, kuwa wa pekee. Bahati nzuri Mungu anawapaga uongozi wa juu watu wanyenyekevu km Rais wetu.
 
Wananchi wana hasira jamani sio kwa kule kufoka kuna mambo viongozi wetu huwa wanafanya hawajali ..wanafanya wanavojisikia na majibu wanayotoa pia huwa yanawauzi wananchi ndio matokeo yake hayo.
 
Nakuelewa mkuu, ila tatizo la v8 hapa Tz unalionaje, hatuwezi kua na njia mbadala wa kumpunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kweli lipo Jambo umeliongea hapo nimekuelewa,

Je haiwezekani waziri na naibu wake kwenda kwenye kikao na gari MOJA nzuri ila ambayo sio v8,

Najua mawaziri lazima kutembelea Miradi mbali mbali kwenye Mikoa tofauti, na ikumbukwe KILA mkoa yapo magari ya serikali , vipi waziri akiwa na ziara mfano Kigoma, akapanda ndege mpaka kigoma, hawezi pewa usafiri katika mkoa husika na kukamilisha ziara yake , na kupanda ndege kurudi, au ni lazima ungurumisha li v8 from Dom to kigoma,
 
Uko sahihi kabisa. Ukuaji duni ukihusisha kwashiakor akili nzuri utaipata. Alikuwa anatutukana Prof Ngware chuo kikuu cha Dar Es Salaam kuwa tulianza kujifunza kula mayai kwa pesa za Boom wakati watoto wake walikuwa wanakula kila siku tusingekuwa na akili sawa na watoto wake. Kuna ukweli.
 
Hii ndo ilikua hoja ,na ndo maana mjadala umekua mkubwa, watu wasijifiche kwenye kichaka Cha kuita watu sijui wajinga, watu wanaelewa why wanahoji na why imekua story, hasa KWa viongonzi watokao afrika
Na kwanini mhoji nyie watu weusi na akili yenu nyeusi wakati wazungu na akili zao hawahoji. Hamuoni hata aibu? Mna akili ndogo km K ya mjusi
 
Machawa ya mama yanajitahidi kuficha aibu
 
Kama hukuwaelewa waleta nyuzi useme wakufafanulie walimaanisha nini. Mimi si mmojawapo lakini nyuzi zào zilikuwa na maana kubwa Sana. Ni mwwndelezo wa maoni yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Umma kwenye misafara. Mwezi uliopita baadhi ya Watanzania walilalamikia wingi wa magari ya misafara kwenye ziara za viongozi wa kitaifa. Msafara wa Rais Samia kwenda Kyela ulikuwa na magari ya kifahari zaidi ya 70 yenye high fuel consumption level, kilichoongeza msafara ni idadi kubwa ya Mawaziri kwenda kwenye ziara eti kutoa ufafanuzi wa masuala yanayohusu wizara zào wakati na wao wametoka huko kwenye ziara wakiwa Peke yao hata mwezi haujaisha. Wakifika eneo la Mkutano Waziri anapewa dakika 2 kuongea Yale Yale anayokuja kuongea Rais. Kichekesho zaidi kilikuja kwenye msafara wa Waziri wa fedha eti anakwenda kuwasilisha bajeti ya serikali akiwa na msafara mkubwa wa pikipiki 3 na magari utadhani ni msafara wa Makamu wa Rais.
Leo Rais amefika Ulaya amepanda basi la pamoja na wenzake lakini ameshindwa kukemea matumizi Makubwa ya Mawaziri na Wakuu wa mikoa na wilaya wanaofanya ziara Kwa misafara mikubwa isiyo na tija. Tumesikia kelele za Watanzania kuhusu ununuzi wa magari ya kifahari wa zaidi ya mil.500 Kwa Gari, lakini Waziri anainuka na kujibu "Waziri hawezi kupanda pick up". Yaani ukitoa pick up magari mengine yaliyobaki yanauzwa mil.500+?
Kwa hili la Marais kipandishwa basi si ajabu Kwa Marais wazungu, lakini Kwa Marais Waafrika liwe funzo Kwa jinsi wanaoishi maisha ya kifahari huku Wananchi wao wakiwa Hohe hahe.
 
Akili za kiafrika bado sana
 
Chawa hawawezi kuelewa hii mantiki miaka mia moja,ila hicho ulichokielezea ndio uhalisia wa hoja
 
Hata Mimi siwapendi mambo yao, lakini huwezi kunitowa akili ya kutofautisha msiba na official state visit.

Hao wote Leo wanakwenda Marekani UN, fuatilia mapokezi yao utaona tofauti ya protocol ilivyo.

Tusiache mioyo yetu ikajaa chuki ya kupitiliza.
Si kama ile chuki uliyonayo kwa Magufuli?
 
Nilielewa sana mkuu, wapo waliokuwa na mtazamo kama ulivyosema. Ila kuna nyuzi nyingi tu zilikuwa zinalaumu sana na hata kutoa lugha kali kwa waliojaribu kufafanua tena kwa vielelezo. Ninawaongelea hawa ambao walikuwa wakali kwelikweli kwa wote walioonekana kutetea utaratibu wa viongozi wetu kutumia mabasi, tna wakidai tumedhalilishwa sana, nilipata muda wa kupitia karibu nyuzi zote kwenye hili sakata.
Asante kwa ufafanuzi
 

Mkuu ukifuatilia survey iliyofanywa na kituo cha chakula na lishe Tanzania (Tanzania Food and Nutrition Centre-TFNC), Takribani 32% ya watoto chini ya miaka mitano wana utapiamlo mkali (Severe/acute undernourished) na mikoa inayoongoza kwa kilimo ndio ina tatizo hili sana.

Nutrition and Food Security Situation in Tanzania
Nutrition and Food Security Situation According to the 2018 SMART survey, 32 percent of children under five years are stunted, which is a significant decrease from 35 percent in 2014. The most affected regions with a prevalence of stunting exceeding 40 percent were Ruvuma (41 percent), Iringa (47 percent), Rukwa (48 percent), Kigoma (42 percent), Njombe (54 percent), and Songwe (43 percent). In Zanzibar, stunting rates ranged from 20–24 percent in Stone Town and Unguja North, respectively. Between 2014 and 2018, a significant decrease of the prevalence of stunting was observed in Dodoma, Morogoro, Pwani, Lindi, Tabora, Kagera, Mwanza, and Katavi (MoHCDGEC, MoH, TFNC, NBS, OCGS, and UNICEF 2018).

According to the 2015–2016 DHS-MIS, 5 percent of children under five are wasted. Wasting is more common in Zanzibar than in Tanzania Mainland (7 percent versus 4 percent) and is very high in Kusini Pemba (9 percent), Kaskazini Pemba (9 percent), and Kusini Unguja (8 percent). In Tanzania, 14 percent of children under five are underweight (too thin for age). At the other extreme, 4 percent are overweight. Rates of stunting, wasting, and underweight generally decrease as maternal education increases. All three nutritional status indicators are highest among children in the lowest wealth quintile and lowest among children in the highest wealth quintile (MoHCDGEC, MoH Zanzibar, NBS, OCGS, and ICF 2016).

Fifty-nine percent of infants under six months are exclusively breastfed in Tanzania. Exclusive breastfeeding declines rapidly with age; only 27 percent of infants aged four to five months are exclusively breastfed compared with 84 percent of infants aged zero to one month and 59 percent of infants aged two to three months. Complementary feeding practices are inadequate, with only 10 percent of breastfed children 6–23 months receiving a minimum acceptable diet, which has a major impact on growth and development (MoHCDGEC, MoH Zanzibar, NBS, OCGS, and ICF 2016). A recent presentation shows that 59 percent of the Tanzanian population cannot afford a nutritionally adequate diet (TFNC and WFP 2017).

Early childbearing also contributes to malnutrition in Tanzania. By age 19, 57 percent of adolescent girls had begun childbearing in 2015–2016, which is an increase from 44 percent in 2010 (MoHCDGEC, MoH, NBS, OCGS, and ICF 2016; NBS and ICF Macro 2011). Tanzania is also experiencing the double burden of malnutrition, with 28 percent of women and 4 percent of children under five years suffering from overweight and obesity (MoHCDGEC, MoH Zanzibar, NBS, OCGS, and ICF 2016).

Source: https://www.usaid.gov/sites/default/files/documents/Copy_of_tagged_Tanzania-Nutrition-Profile.pdf
 
Sawa mkuu ila 32% ya watoto chini ya miaka mitano wana udumavu mkali kabisa (Severe/acute undernourished)
 
Wanakuwa "salama" zaidi wakiwa nje kuliko nyumbani,Tanzania!!!

Ushawahi kushuhudia msafara ,wakiwa nchini? Ama unaishi "ughaibuni"?
Nimekuwa nikishuhudia misafara kila siku. Ungepata wasaa wa kupitia nyuzi zote kuhusu hiyo mada ungeona kuna tatizo mahali. Yaani kuna watu mpaka wanatukana. Nilimsikia Waziri mkuu wa New Zealand akisifia na kusema hata mawaziri wake anawa encourage kutumia usafiri nafuu.
Kiufupi kuna watu wametoa povu kwelikweli na kuna wengine pia walisupport kilichotokea.
 
Shida ni kwamba kwanini wakirudi nyumbani msafara unakuwa na magari 80+,kwanini yasipatikane mabasi mawili na magari manne madogo kwenye Convoy??
Hilo ni tatizo kubwa sana na hata comments nyingi tu zilikuwa zinaliongelea hilo. Pengine ni genetical make up yetu, kiufupi sijui haswa sababu halisi zaidi ya ulimbukeni, ubinafsi, tamaa, kutokujali unaowaongoza n.k....
Huku kwetu mtu akiwa kiongozi anaona wote anaowaongoza ni swekeni tu na hatuna mfumo wa kuwawajibisha au wao kuwajibika. Limekuwa ni kama gang of wolves (genge la mbwa mwitu tu)
 
Hatutaki kuelewa sisi tunachojua wamewekwa kama abiria😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…