lakini hapo hapo na mimi pia nina binti ninayemfahamu na hata sasa yupo na atakuwa ameshakua pia anaishi hapo sinza nyuma tu ya hiyo hostel ya udsm ( jina nalihifadhi yasije nikuta ya kamukara mie mtoto wa watu ) ambapo huyo binti alikuwa anahadithia kuwa yeye anachokumbuka ni kuwa alichukuliwa pamoja na wenzake kama wanne hivi kisha wakati wanapelekwa kupimwa kwa daktari ambaye na yeye pia alishapewa maelekezo nyeti na ya kimafia zaidi ni kwamba walivuliwa nguo zao za ndani kisha zile nguo zikapakwa chilli source ili kusudi tu wakipelekwa hospitalini kupimwa basi ionekane kuwa walibakwa na kuumizwa. sasa kama huyu binti alitudanganya ni shauri yake ila ukweli huo alituthibitishia mwenyewe kwa mdomo wake na bahati nzuri mtoto mdogo hua haongopi na ndiyo maana hata mkienda mahakamani na unashindanishwa na mtoto basi jua tu kuwa 95% imekula kwako kwani wanasikilizwa, wanaaminika mno lakini hata psychologically au naturally watoto wako very faithfull. na ili kulithibitisha hili wewe fanya tu kitendo kibaya nyumbani kwako kwa mfano ni baba halafu mkeo kasafiri na ukajitusu kuingiza mwanamke ndani basi kaa ukijua kuwa hata kama utajifanya kumpiga mkwara mwanao kuwa asiseme au ukamuhadaa kwa vijizawadi jua tu kwamba siku akiwa tu amekaa na mama yake ( mkeo ) dogo atafunguka kila kitu na hatimaye kitasanuka. kwa kumalizia tu ni kwamba hili suala la akina babu seya na mwanae papii lina confusions nyinginyingi tu kwa mfano wewe umemtaja " mjomba " kuwa kahusika lakini kuna taarifa kuwa bifu halikuwa la " mjomba " bali ni yule i.g.p wetu mstaafu aishie morogoro na ambaye amejenga bonge la msikiti maeneo ya misufini jirani kabisa na soko la manzese la morogoro na alishawahi hata kukumbwa na kashfa ya kukataa mti wake mzuri wa mbegu aliyoipanda mwenyewe na beki tatu ndani ya 6 * 6 na wengine pia wanahusisha na " mtangaza nia ambaye mpaka jana tunaaminishwa kuwa ameshajikusanyia saini laki 7 na elfu hamsini ". sasa sijui tuamini lipi na tushike lipi labda kuna wengine wanaweza wakawa wanalijua hili hivyo si vibaya na wao tukapata mtazamo au ufahamu wao wa hili suala.