Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
Mkuu brazaj,
Mageuzi ndani ya vyama vya upinzani ni mkakati unaotumiwa na ccm kuvuruga vyama husika na kupandikiza mamluki wao huko!
Ni vizuri kujihadhari kucheza mziki usioujua..

Ndiyo maana tunashauri kuwa, wewe na wenye maono yanayofanana anzisheni chama kipya. Kwa kuwa mnaamini mnayo maono na dira yenye tija mtapata wafuasi wengi tu.
 
Jambo unalo zungumza mkuu ni mpango mzuri lakini kasoro iliyopo inayo tia ukakasi wa kutekelezeka kwa mpango wako kwa kuwa vyama vya kisiasa hapa nchi vimekwisha kuwa mali za baadhi ya familia na makunfi yao ya karibu kwa hiyo kuleta mageuzi/ mapinduzi katika mfumo wa namna hii ngumu kutekelezeka labda uundwaji wa vyama vipya vyenye sera dhabiti vitakavyo leta upinzani dhabiti wa hoja na vyama hivi vya sasa vilivyopo nchini . Vyama vipya sharti vinapaswa kuwa na watu ambao falsafa zina fanana na vilivyo wazi kwa wanachama wote.

Ninakiona unachosema lakini ni vyema kuanzisha chama kingine kubakia kuwa option ya mwisho.

Tunayo haki ya kujua mikakati ya kutuvusha iko je.

Mbona wenye kuongoza majahazi haya salama kwenye vyama hivi hivi wamo wengi tu?

Ni jambo muhimu awaye yote akajua hayupo mwenye hati miliki navyo.

Penye nia pana njia.
 
Mkuu brazaj,
Mageuzi ndani ya vyama vya upinzani ni mkakati unaotumiwa na ccm kuvuruga vyama husika na kupandikiza mamluki wao huko!
Ni vizuri kujihadhari kucheza mziki usioujua..

Ndiyo maana tunashauri kuwa, wewe na wenye maono yanayofanana anzisheni chama kipya. Kwa kuwa mnaamini mnayo maono na dira yenye tija mtapata wafuasi wengi tu.

Mkuu antimatter tunayoomba ni mambo ya msingi yasiyohalalisha mpambanaji awaye yote kubwaga manyanga au hata kuhimizwa kufanya hivyo.

1. Hatupendezwi na ukimya wa viongozi wetu. Zaidi sana tunashangazwa na pongezi zenu kwao eti kwa kukaa kimya na kwamba eti kuwa huo ndiyo uwe mwendo.
2. Tumekuwa tukiomba mikakati iliyopo ya ukombozi, tuijue ili tukomae nayo.
3. Tumekuwa tukiomba mikakati ya ushirikishwaji wa wote wenye kutuunga mkono ili tusimwache mtu nje.
4. Tumekuwa tunaamini kwenye siasa za kiana uharakati. Hajashindwa mtu kwenye njia hii.
5. Tunahitaji kujua mikakati ya kuwahami wahanga kwenye mapambano.
6. Kwa vile wenye vyama ni sisi, kulikoni kuhofia chaguzi za wazi kwa agenda zetu zilizo wazi?

Tuna kipi cha kuficha kiasi cha kuwachagiza wajumbe wenye mawazo ya kuhitaji matokeo kama hivi kuondoka?

Kipi kinakuvutia wewe ndugu mjumbe kwenye kimya hiki kinachoendelea kutamalaki kutoka kwa waliopaswa kuwajibika kwetu?

Ni miye nisiyeelewa?
 
Ninakiona unachosema lakini ni vyema kuanzisha chama kingine kubakia kuwa option ya mwisho.

Tunayo haki ya kujua mikakati ya kutuvusha iko je.

Mbona wenye kuongoza majahazi haya salama kwenye vyama hivi hivi wamo wengi tu?

Ni jambo muhimu awaye yote akajua hayupo mwenye hati miliki navyo.

Penye nia pana njia.
“Hakuna mwenye hakimiliki ya chama” chama ni cha wanachama wote wenye nia dhabiti. hoja yako ni dhabiti haswa yenye ujazo inanikumbusha baada ya chairman Mao kufariki baadae kamanda Deng kushika hatamu alifanya kitu kinachoitwa political reform/ mageuzi ya kisiasa ndani ya chama [ CPC ] alipinga namna chama kilivyo kuwa kinaenda kuonekana wale walio upande wa Chairman Mao ndio wenye nguvu na mamlaka ya CPC , Deng alikata mirija yote na akasema hakuna mtu au kikundi cha watu chenye mamlaka ya CPC bali CPC ni ya Wana CPC wote na wananchi wote wa China na sio kikundi kidogo cha watu mfano wafahidhina wa Chair Mao na Gang of Four .

Ni kweli kabisa Vyama vya sasa havipaswi kuonekana kuwa ni mali ya mtu au kikundi cha watu fulani pekee bali chama kinapaswa kuwa mali ya wanachama wote wenye nia njema na maendeleo ya chama.

Tunapaswa kuhimiza demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu vya siasa na sio kuhimiza demokrasia danganya toto tutakuwa hatujengi chama bora bali tunajenga chama kinachomzunguka mtu binafsi au kikundi cha watu fulani na sio falsafa ya chama iliyo chanzo cha uwanzishwaji wa chama.
 
Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
Ndio haya hapa yanaendelea huku msibani 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220824-184732.png
    Screenshot_20220824-184732.png
    99.7 KB · Views: 4
“Hakuna mwenye hakimiliki ya chama” chama ni cha wanachama wote wenye nia dhabiti hoja yako ni dhabiti haswa yenye ujazo inanikumbusha baada ya chairman Mao kufariki baada kamanda Deng kushika hatamu alifanya kitu kinachoitwa political reform/ mageuzi ya kisiasa ndani ya chama [ CPC ] alipinga namna chama kilivyo kuwa kinaenda kuonekana wale walio upande wa Chairman Mao ndio wenye nguvu na mamlaka ya CPC , Deng alikata mirija yote na akasema hakuna mtu au kikundi Cha watu chenye mamlaka ya CPC bali CPC ni ya Wana CPC wote na wananchi wote wa China na sio kikundi cha kidogo cha watu mfano wafahidhina wa Chair Mao na Gang of Four .

Ni kweli kabisa Vyama vya sasa havipaswi kuonekana kuwa ni mali ya mtu au kikundi Cha watu fulani pekee bali chama kinapaswa kuwa mali ya wanachama wote wenye nia njema na maendeleo ya chama.

Tunapaswa kuhimiza demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyama vyetu vya siasa na sio kuhimiza demokrasia danganya toto tutakuwa hatujengi chama bora bali tunajenga chama kinachomzunguka mtu binafsi au kikundi cha watu fulani na sio falsafa ya chama iliyo chanzo cha uwanzishwaji wa chama.

Haya ndiyo maneno. Kwa njia hii ya demokrasia inayo nafasi ya kutamalaki vyamani, na tutavuka.

Nia yetu dhidi ya walamba asali ni wazi. Hatuna cha kuficha.

"Hatufurahishwi na mwendelezo wao wa kupora haki za zetu."

Haki zetu "matter."
 
mwigulu shikilia hapo hapo ongeza tozo zingine kwa mpigo kama nne hivi Ili tukae SAwa Burundi kumejaa
 
mwigulu shikilia hapo hapo ongeza tozo zingine kwa mpigo kama nne hivi Ili tukae SAwa Burundi kumejaa

Pongezi kama hizi zina marks zote za mlamba asali, chawa au mnafiki. Unaangukia wapi hapo mkuu?
 
Haya ndiyo maneno. Kwa njia hii ya demokrasia inayoogopa nafasi ya kutamalaki chamani, na tutavuka.

Nia yetu dhidi ya walamba asali ni wazi. Hatuna cha kuficha.

"Hatufurahishwi na mwendelezo wao wa kupora haki za zetu."

Haki zetu "matter."
Ni kweli kabisa inabidi ifike wakati vyama vya kisiasa viweze kujitanabaisha kitofauti tofauti lazima uwepo utofauti kati ya chama tawala na vyama pinzani kitu ambacho kwa sasa hakipo ni ngumu sana kwa sasa hapa Tanzania kutofautisha Kati ya chama tawala [ CCM ] na vyama vya upinzani namna ya kutuvusha hapa tulipo vyama vyote vya kisiasa vimekosa agenda ya kuwaelezea WATANZANIA ipi ni mikakati yao kama chama kuwa vusha hapa walipo WATANZANIA na wapi watawapekeka na kuwa fikisha , vyama vya upinzani kuchezeshwa ngoma ya mtindo mmoja na chama tawala[ CCM ] nao kuicheza hii Ngoma katika mtindo ambao chama tawala kina wafurahisha [ wanufahisha ] , vyama kukosa falsafa inayo tambulika na wanachama wake na wananchi wote wa Tanzania ili wananchi wajue ni zipi falsafa bora zitakazo wafaa wao . Vyama vya upande wa upinzani kutokuweka kujitanabaisha ni mbinu ipi iliyo bora kwao katika kudai haki kutoka chama tawala [ CCM/ walamba asali ] je kwao kuungana na walamba asali ndio njia iliyo bora ya kudai haki zao na za WATANZANIA kutoka kwao? Je njia ya mapambano/ harakati zisizo na kikomo ni njia iliyo bora kwao ? vyama vya upinzani vinapaswa kuji uliza na kujijibu.

Ni mengi sana vyama vyetu vya kisiasa vinapaswa kurekebisha bisha [ vyama vyetu vinahitaji “Political reform” ili kutibu matatizo yanayo vikabili ]
 
Kuanzisha vyama ni kuwachanganya wananchi. Vyama hivi tumevipigania sote hadi kuvifikisha hapa vilipo.

Kipi tunachoomba kilicho kinyume cha utaratibu:

"Iko wapi mikakati ya ukombozi? Iko wapi mikakati ya kutuvusha?"

Kwanini isiwe asiye na majibu hapo hatufai aingie mwenye majibu?

Ninakazia hivi vyama si mali binafsi.
Kabisa!

Tumpindue mwamba, haiwwzekani awe anaramba asali tu
 
denooJ na brazaj napenda Sana misimamo yenu Ni watu mlio neutral katika mambo ya msingi..
Hizi tabia za kuwa mfuasi kindakindaki ndio chanzo cha uozo vyamani...
Rasimu ya Warioba irudi mezani watu tumchague Mgombea huru...
Maana hivyi vyama vina udwanzi mwingi...Ukishindwa kuongoza watu ng'atuka upishe wengine..
 
Ni kweli kabisa inabidi ifike wakati vyama vya kisiasa viweze kujitanabaisha kitofauti tofauti lazima uwepo utofauti kati ya chama tawala na vyama pinzani kitu ambacho kwa sasa hakipo ni ngumu sana kwa sasa hapa Tanzania kutofautisha Kati ya chama tawala [ CCM ] na vyama vya upinzani namna ya kutuvusha hapa tulipo vyama vyote vya kisiasa vimekosa agenda ya kuwaelezea WATANZANIA ipi ni mikakati yao kama chama kuwa vusha hapa walipo WATANZANIA na wapi watawapekeka na kuwa fikisha , vyama vya upinzani kuchezeshwa ngoma ya mtindo mmoja na chama tawala[ CCM ] nao kuicheza hii Ngoma katika mtindo ambao chama tawala kina wafurahisha [ wanufahisha ] , vyama kukosa falsafa inayo tambulika na wanachama wake na wananchi wote wa Tanzania ili wananchi wajue ni zipi falsafa bora zitakazo wafaa wao . Vyama vya upande wa upinzani kutokuweka kujitanabaisha ni mbinu ipi iliyo bora kwao katika kudai haki kutoka chama tawala [ CCM/ walamba asali ] je kwao kuungana na walamba asali ndio njia iliyo bora ya kudai haki zao na za WATANZANIA kutoka kwao? Je njia ya mapambano/ harakati zisizo na kikomo ni njia iliyo bora kwao ? vyama vya upinzani vinapaswa kuji uliza na kujijibu.

Ni mengi sana vyama vyetu vya kisiasa vinapaswa kurekebisha bisha [ vyama vyetu vinahitaji “Political reform” ili kutibu matatizo yanayo vikabili ]

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Tufike mahali tuelezane ukweli. Kwamba viongozi wako mstari wa mbele wa maandamano, wafuasi wa kutosha watakosekana vipi?

Mbona tulikuwapo kwa maelfu yetu JKNIA na hata Kiluvya, Hizi ikiwa kinyume mno cha matakwa ya Sirro, mwendazake na magenge yao ya wasiojulikana?
 
Back
Top Bottom