Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
Si ulikuwa unaimba CCM mbele kwa mbele? Isome namba sasa? Hamia umoja party
 
Mwarobaini wa haya yote uliyo ya zungumza mkuu ni :-
i, Uwanzishwaji wa vyama vipya vya kisiasa vilivyo imara na vilivyo na sera dhabiti zilizo wazi na vinavyo endeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ya kweli na sio demokrasia maigizo.

ii, Ugombea binafsi [ mgombea binafsi ] aliye na sera dhabiti za kutuvusha hapa tulipo.

Tulipo hoja hizi zinaishi. Tunaochoshwa na hali hizi tujuane. Ilikuwa kwa sababu kama hizi kulikuwa na PAC na ANC. Chris Hani kutokea PAC akawa mkuu wa Umkonto we Sizwe, yaliyokuwa majeshi ya ANC.
 
Back
Top Bottom