Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Mkuu brazaj,
Mageuzi ndani ya vyama vya upinzani ni mkakati unaotumiwa na ccm kuvuruga vyama husika na kupandikiza mamluki wao huko!
Ni vizuri kujihadhari kucheza mziki usioujua..

Ndiyo maana tunashauri kuwa, wewe na wenye maono yanayofanana anzisheni chama kipya. Kwa kuwa mnaamini mnayo maono na dira yenye tija mtapata wafuasi wengi tu.
 

Ninakiona unachosema lakini ni vyema kuanzisha chama kingine kubakia kuwa option ya mwisho.

Tunayo haki ya kujua mikakati ya kutuvusha iko je.

Mbona wenye kuongoza majahazi haya salama kwenye vyama hivi hivi wamo wengi tu?

Ni jambo muhimu awaye yote akajua hayupo mwenye hati miliki navyo.

Penye nia pana njia.
 

Mkuu antimatter tunayoomba ni mambo ya msingi yasiyohalalisha mpambanaji awaye yote kubwaga manyanga au hata kuhimizwa kufanya hivyo.

1. Hatupendezwi na ukimya wa viongozi wetu. Zaidi sana tunashangazwa na pongezi zenu kwao eti kwa kukaa kimya na kwamba eti kuwa huo ndiyo uwe mwendo.
2. Tumekuwa tukiomba mikakati iliyopo ya ukombozi, tuijue ili tukomae nayo.
3. Tumekuwa tukiomba mikakati ya ushirikishwaji wa wote wenye kutuunga mkono ili tusimwache mtu nje.
4. Tumekuwa tunaamini kwenye siasa za kiana uharakati. Hajashindwa mtu kwenye njia hii.
5. Tunahitaji kujua mikakati ya kuwahami wahanga kwenye mapambano.
6. Kwa vile wenye vyama ni sisi, kulikoni kuhofia chaguzi za wazi kwa agenda zetu zilizo wazi?

Tuna kipi cha kuficha kiasi cha kuwachagiza wajumbe wenye mawazo ya kuhitaji matokeo kama hivi kuondoka?

Kipi kinakuvutia wewe ndugu mjumbe kwenye kimya hiki kinachoendelea kutamalaki kutoka kwa waliopaswa kuwajibika kwetu?

Ni miye nisiyeelewa?
 
“Hakuna mwenye hakimiliki ya chama” chama ni cha wanachama wote wenye nia dhabiti. hoja yako ni dhabiti haswa yenye ujazo inanikumbusha baada ya chairman Mao kufariki baadae kamanda Deng kushika hatamu alifanya kitu kinachoitwa political reform/ mageuzi ya kisiasa ndani ya chama [ CPC ] alipinga namna chama kilivyo kuwa kinaenda kuonekana wale walio upande wa Chairman Mao ndio wenye nguvu na mamlaka ya CPC , Deng alikata mirija yote na akasema hakuna mtu au kikundi cha watu chenye mamlaka ya CPC bali CPC ni ya Wana CPC wote na wananchi wote wa China na sio kikundi kidogo cha watu mfano wafahidhina wa Chair Mao na Gang of Four .

Ni kweli kabisa Vyama vya sasa havipaswi kuonekana kuwa ni mali ya mtu au kikundi cha watu fulani pekee bali chama kinapaswa kuwa mali ya wanachama wote wenye nia njema na maendeleo ya chama.

Tunapaswa kuhimiza demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu vya siasa na sio kuhimiza demokrasia danganya toto tutakuwa hatujengi chama bora bali tunajenga chama kinachomzunguka mtu binafsi au kikundi cha watu fulani na sio falsafa ya chama iliyo chanzo cha uwanzishwaji wa chama.
 
Ndio haya hapa yanaendelea huku msibani 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220824-184732.png
    99.7 KB · Views: 4

Haya ndiyo maneno. Kwa njia hii ya demokrasia inayo nafasi ya kutamalaki vyamani, na tutavuka.

Nia yetu dhidi ya walamba asali ni wazi. Hatuna cha kuficha.

"Hatufurahishwi na mwendelezo wao wa kupora haki za zetu."

Haki zetu "matter."
 
mwigulu shikilia hapo hapo ongeza tozo zingine kwa mpigo kama nne hivi Ili tukae SAwa Burundi kumejaa
 
mwigulu shikilia hapo hapo ongeza tozo zingine kwa mpigo kama nne hivi Ili tukae SAwa Burundi kumejaa

Pongezi kama hizi zina marks zote za mlamba asali, chawa au mnafiki. Unaangukia wapi hapo mkuu?
 
Haya ndiyo maneno. Kwa njia hii ya demokrasia inayoogopa nafasi ya kutamalaki chamani, na tutavuka.

Nia yetu dhidi ya walamba asali ni wazi. Hatuna cha kuficha.

"Hatufurahishwi na mwendelezo wao wa kupora haki za zetu."

Haki zetu "matter."
Ni kweli kabisa inabidi ifike wakati vyama vya kisiasa viweze kujitanabaisha kitofauti tofauti lazima uwepo utofauti kati ya chama tawala na vyama pinzani kitu ambacho kwa sasa hakipo ni ngumu sana kwa sasa hapa Tanzania kutofautisha Kati ya chama tawala [ CCM ] na vyama vya upinzani namna ya kutuvusha hapa tulipo vyama vyote vya kisiasa vimekosa agenda ya kuwaelezea WATANZANIA ipi ni mikakati yao kama chama kuwa vusha hapa walipo WATANZANIA na wapi watawapekeka na kuwa fikisha , vyama vya upinzani kuchezeshwa ngoma ya mtindo mmoja na chama tawala[ CCM ] nao kuicheza hii Ngoma katika mtindo ambao chama tawala kina wafurahisha [ wanufahisha ] , vyama kukosa falsafa inayo tambulika na wanachama wake na wananchi wote wa Tanzania ili wananchi wajue ni zipi falsafa bora zitakazo wafaa wao . Vyama vya upande wa upinzani kutokuweka kujitanabaisha ni mbinu ipi iliyo bora kwao katika kudai haki kutoka chama tawala [ CCM/ walamba asali ] je kwao kuungana na walamba asali ndio njia iliyo bora ya kudai haki zao na za WATANZANIA kutoka kwao? Je njia ya mapambano/ harakati zisizo na kikomo ni njia iliyo bora kwao ? vyama vya upinzani vinapaswa kuji uliza na kujijibu.

Ni mengi sana vyama vyetu vya kisiasa vinapaswa kurekebisha bisha [ vyama vyetu vinahitaji “Political reform” ili kutibu matatizo yanayo vikabili ]
 
Kabisa!

Tumpindue mwamba, haiwwzekani awe anaramba asali tu
 
denooJ na brazaj napenda Sana misimamo yenu Ni watu mlio neutral katika mambo ya msingi..
Hizi tabia za kuwa mfuasi kindakindaki ndio chanzo cha uozo vyamani...
Rasimu ya Warioba irudi mezani watu tumchague Mgombea huru...
Maana hivyi vyama vina udwanzi mwingi...Ukishindwa kuongoza watu ng'atuka upishe wengine..
 

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Tufike mahali tuelezane ukweli. Kwamba viongozi wako mstari wa mbele wa maandamano, wafuasi wa kutosha watakosekana vipi?

Mbona tulikuwapo kwa maelfu yetu JKNIA na hata Kiluvya, Hizi ikiwa kinyume mno cha matakwa ya Sirro, mwendazake na magenge yao ya wasiojulikana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…