PostGE2025 Mufti wa Tanzania: Tunawasihi waislamu kutokujihusisha na maandamno ya Desemba 9

PostGE2025 Mufti wa Tanzania: Tunawasihi waislamu kutokujihusisha na maandamno ya Desemba 9

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mufti wajibu wako umeshamaliza, asiyeelewa muache aende nchi ina watu karibia Milioni 65, wakijipunguza wengine haina shida.
Huyo uliyemweka kwenye profile ndio alikuwa kiongozi wa maandamano USA na amechangia pakubwa sana katika kujenga USA ya haki uionayo Leo.
 
Wameamua kuside na udhalimu, historia haitawasahau kwa hili. Na atakuja Rais wa dini nyingine, wasinyanyue midomo yao wapuuzi wakubwa hawa.

Kwani Bakwata walimpinga Magufuli? Walimpiga vita Mkapa? Walitoa matamko mangapi dhidi yao?

Tunaoona wanatoa sana matamko wakati wa watawala Waislam ni hao kina Tec, na watawala wanapokuwa wenzao matamko yao yanakuwa machache na hayana lugha kali. Bali wakati wa Nyerere hawakutoa hata tamko moja dhidi ya Serikali yake.

Na sisi Waislam tumefundishwa namna ya kuishi na watawala, sisi tuna Muongozo katika Dini yetu, Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) katufundisha kuwa tunapotaka kumnasihi mtawala tusimnasihi hadharani, tumnasihi faragha kwa siri.

Na Waislam wanapinga dhulma za watu wote, iwe ya mtawala au raia (dhulma sio mtawala tu ndio anafanya) ila kuna taratibu zake katika kuendea mambo. Dini yetu mambo haijafundisha mambo yaende hovyo hovyo, kumewekwa Muongozo, ndio maana mtawala ikawekwa anasihiwe kwa siri.
 
Serikali haiendeshwi kwa utashibwako. Kuna sheria na kanuni. Ambazo zinakuwa enforced.

Hukonkwenu kwenye familia unasheria gani kwa mfano. Hiwa unawasomea bajeti na kuzitungia sheria?

Acha ujinga wa familia kufanya kama serikali.
Ndio maana watoto,wakwe wanawekwa kwenye uongozi kwa hizi akili.
Jibu maswali niliyo kuuliza.
 
Huyo uliyemweka kwenye profile ndio alikuwa kiongozi wa maandamano USA na amechangia pakubwa sana katika kujenga USA ya haki uionayo Leo.
Lakini haki siyo 100% ndiyo maana kuna Wasomali wanataka kurudishwa kwao, wanaona hawatendewi haki ndani ya US, kuna black americans ambao nao kwanamna moja au nyingine huona hawatendewi haki na whites. Sina shida na upatikanaji wa haki njia tunayotaka kuiendea inaweza kututoa katika kuipata hiyo haki. Msg ilishaeleweka kilichobaki ni utekelezaji, kinachohitajika ni subira.
 
njia tunayotaka kuiendea inaweza kututoa katika kuipata hiyo haki
Wewe unadhani "njia" aliyochagua Samia Suluhu Hassan kulazimisha kutawala kwa nguvu ndiyo njia sahihi ya kutafuta HAKI?

Samia alikuwa na "Subira" alipoamua kwa maksudi kabisa kuwanyima waTanzania HAKI ya kuchagua viongozi wanaowataka wao? Sasa kanyakuwa madaraka, ndipo anawatuma msambaze ujumbe wa subira?

Vichwa vyenu vikoje nyie watu!

Hao" Wasomali na 'blacks" mfano unaotumia kutetea hoja ni wazi hujui unachozungumzia.
 
Na sisi Waislam tumefundishwa namna ya kuishi na watawala, sisi tuna Muongozo katika Dini yetu, Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) katufundisha kuwa tunapotaka kumnasihi mtawala tusimnasihi hadharani, tumnasihi faragha kwa siri.
Tatizo lipo hapa. Huu ni unafiki wa hali ya juu sana, na unafiki mara zote hauna mwisho mzuri mahali popote.

Sasa baada ya kutueleza mwongozo huo, hebu zungumzia hayo yanayotokea Sudan sasa hivi, au Somalia, Syria, na kwingineko.

Hiyo "miongozo" ya karne nyingi zilizopita tuitegemee kwa maisha ya binaadam wa karne hi itawezekana vipi; tena kwenye taifa ambalo wananchi wake siyo wa imani mojai?
 
Shida ya viongozi wa Tanzania wote (wa siasa, taasisi za dini na NGO’s) kupitia hype za social media na mataahira wachache ambao wanasambaza upuuzi wanaoongea.

Wanadhani sisi wenyewe (wengi wetu, kwenye jamii) hatuna akili ya kuamua kutokana na reasoning zetu.

Ni asilimia ndogo sana ya watanzania ambao wanajali what ‘Kitima’ says or sijui ‘Sheikh’ gani.

Wengi wetu tunaimani ya mungu, lakini sio wacha mungu; akili zetu ni namna ya kuishi.

Huu ujinga wa udini ni JF ndio una promote kwa kusambaza.

Sisi wengine hatuitaki hii serikali, sio kwa sababu Kitima sijui TEC kasema nini au kuna Sheikh kasema nini.

All we know watanzania hatumtaki Samia because she is a bad president. Otherwise ain’t nobody cares about religious sentiments.

Ni mataahira tu ndio yanatuletea udini, haw sio wenzetu; as is sisi wenyewe watanzania hatuna akili za kuamua mpaka sijui padre, mchungaji au sheikh atushauri.
 
"Tuepuke upepo mbaya unaosambazwa kwa chuki za kidini, sisi waisalam Mungu hatuktazi kuishi kwa wema na wasiokuwa waislam, maisha ya watu lazime yalindwe nawasihi wote wanaohamasisha matendo ya kuvuruga amani tarehe 9 au 25 waache, pia nawaomba viongozi wa dini zote kuendelea kuwa watulivu hata kwa wananchi pia tuepuke uchochezi unaoweza kutugawa, nawasihi waislamu kote nchini kutojihusisha na maandamano hayo "

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally
Huyu naye ni Mwashambwa tu
 
Tatizo lipo hapa. Huu ni unafiki wa hali ya juu sana, na unafiki mara zote hauna mwisho mzuri mahali popote.

Sasa baada ya kutueleza mwongozo huo, hebu zungumzia hayo yanayotokea Sudan sasa hivi, au Somalia, Syria, na kwingineko.

Hiyo "miongozo" ya karne nyingi zilizopita tuitegemee kwa maisha ya binaadam wa karne hi itawezekana vipi; tena kwenye taifa ambalo wananchi wake siyo wa imani mojai?

Yaliyotokea Sudan, Somalia katika mapinduzi na uasi ni kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na wewe mwenyewe unashuhudia kabisa matokeo ya kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume katika hizo nchi. Namuomba Allah Atusamehe sisi na ndugu zetu Waislam wengine na Awarudishie Amani ndugu zetu waliokosa Amani na Awalipe Kheri.

Ninamuomba Allah Aidumishe Amani Aliyotupa na wala Asitupe Mtihani wala Asituadhibu kwa sababu ya wayafanyayo wapumbavu miongoni mwetu. Ninamuomba Allah Aibariki na Ailinde Tanzania yetu na watu wake, Allahumma Aamiin.
 
Yaliyotokea Sudan, Somalia katika mapinduzi na uasi ni kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na wewe mwenyewe unashuhudia kabisa matokeo ya kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume katika hizo nchi. Namuomba Allah Atusamehe sisi na ndugu zetu Waislam wengine na Awarudishie Amani ndugu zetu waliokosa Amani na Awalipe Kheri.
Sasa nasi hapa Tanzania tuamini tu kwamba hatutafika huko walikofika hao kwa mategemeo tu ya swala zako kwa Mtume?
Hatuwezi kuwa na mategemeo ya namna hiyo. Ndiyo maana hizi dini zinachochea mitafaruku baina ya jamii.
Wee kaa na dini yako, usitake kuieneza kwa wengine kwa kutumia nguvu.
Maswala ya dini yaondolewe kabisa katika kuendesha nchi.
 
Mimi nimelazimisha kwako Dini yangu? Wewe mzee vipi?!

Mimi nimeonesha msimamo wa Uislam juu ya haya, whether unataka au hutaki. Kwani comment yangu ya kwanza uliyo quote wakati namjibu jimama26 comment yake umeisoma mpaka ukaona kwanini nimejibu vile? Unataka kulazimisha Waislam tufanane na nyinyi makafiri?

Sisi Waislam tutaendelea kunasihiana kuilinda Amani ya nchi yetu.

Na hatutokaa kimya pia mkitaka kutoboa meli na wote tupo ndani yake. Lazima tuwaambie mnachofanya sio sawa.
 
Back
Top Bottom