Well, theory yako ina walaki kutokana na hakuna mwenye uhakika kama ni kweli ugongwa ilianzishwa na Wachina au Wamarekani. sisemi kama ni kweli au sio kweli lakini kuna sababu nyingine pia zinazoweza kuchangia kwanini huu ugonjwa umeweza kutapakaa mchi za Magharibi kwa haraka ukilinganisha na nchi za India, Russia au Afrika.
kilichopelekea huu ugongwa kukuwa sana kwenye nchi za Magharibi na Marekani, ni pamoja na nchi hizo kuwa na kipato cha juu kinachowawezesha kusafiri kati ya China na nchi zao za Maghararibi. Nchi nyingi za Magharibi walifunga viwanda vyao vya kuzalisha bidhaa ndogo-ndogo ktk miaka ya 70, China akachangamkia fursa miaka ya 80, leo hii hakuna nchi inaweza kujitosheleza bila ya bidhaa za kutoka China. Japo India ni nchi inayo pakana na China, lakini wahindi wengi bado ni watu kipato chini na hapo hapo wanategema sana bidhaa zinazo zalishwa ndani ya India kuliko nje.
Ugonjwa umeweza kushamiri kwenye nchi za Magharibi kwa kasi kutokana na sababu mbili, kwanza nchi za Magharibi watu wao wako very social and free (hakuna vita na wengi wanakazi na pesa mifukoni), na cha pili, nchi za Magharibi zina wazee wengi wanaoishi maisha mrefu 70,80,100 years old. Lakini hapo hapo hao wazee wengi wana underline health issues ikiwa pamoja na magonjwa ya kupumua, virusi vya corona vinapenda kukaa kwenye mapafu ya watu na kuwapunguzia uwezo wa kupumua kirahisi.