Miaka hiyo, vijana wa Dar wanawaza kwenda Ulaya, vijana wa vijijini wanatamani kuja Dar! Huu mtazamo unaenda katika nyanja mbalimbali za kimaisha!
Watoto wa Magomeni, Ilala, Kinondoni na Kariakoo miaka hiyo ndiyo walikuwa DSM! Sinza walikuja baadaye sana! Weka pembeni wale wa kishua from Masaki, Osterbay na Upanga wale walikuwa next level!
Usishangae sana sekta ya michezo na burudani kutawaliwa na watoto wa hayo maeneo! Halafu kwenye biashara na uongozi wamejaa watoto wa kishua kutoka pande hizo! Unaweza kuta hata wanaotamba huko shamba kumbe alitoka DSM!
Sifa kuu ilikuwa kupendana na kutojiona bora kuliko wengine hata kama umetoboa!
Leo mtu akipata kinyumba na gari anahisi ameyapatia na kuwadharau hata wenyeji waliompkea na kuwaona hawana akili! Ukifuatilia makuzi kumbe alikulia shamba! Siyo wote lakini!