Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Harafu nahisi mzumbe huko unapo sema ni mbali sana...hapo barabarani kulikuwa na uwanja inatizamana na hiyo Sheli...

Uwanja ulikuwa mbele ya nyumba ya warabu Kuna kibinti kimoja kilikuwa kinaitwa SAFAA...ila siku hizi nahisi atakuwa mshangazi🤣🤣🤣

Naizungumzia magomeni ya 1999 ujue​
Kitambo sana hiyo
 
Huu ukoo wa chonji kalibia wote ni watu wa madawa
Na kesi hii ilikuwa na msukumo nyuma yake.... ikimlenga huyu huyu chonji ndy yote haya yakatokea
Kwanza hiyo siku jamaa chonji anapigwa ambush kituo cha polisi magomeni wala urafiki walikuwa hawana taarifa
Umeme ulizimwa eneo lote hilo la magomeni
Baharia siku hiyo nlikuwa grand Hotel pale nna mgeni
Ebwana ilikuwa kama movie....
Chonji walipomtimbia kwake alijua anavamiwa na majambazi
Mule ndani kwqke jamaa alikuwa na mzigo mahela,kuna watu walikuwa wanapack kazi wengine wana hesabu mijihela nk
Jamaa alipelekewa watu wa maana watu walipigika sana maana yeye si alikuwa na watu wapiga ngumi 😄 akapelekewa watu wa ngumi pia
Ila ile operation kwake hata polisi magomeni,urafiki,obay walikuwa haijuwi kama inafanyika

Ova
Halafu hawa jamaa ukoo wao wote ni watu wa madawa huyu ana Yule mdogo wake Kwa dada yake wa pale ilala ametoka juzi tu keko baada ya kukaa miaka 10 na kupata stroke
 
Enzi za uhuni magomeni vijana wengi walizamia na wengine Hadi Leo wapo nchi za mbali..!
Miaka hiyo, vijana wa Dar wanawaza kwenda Ulaya, vijana wa vijijini wanatamani kuja Dar! Huu mtazamo unaenda katika nyanja mbalimbali za kimaisha!

Watoto wa Magomeni, Ilala, Kinondoni na Kariakoo miaka hiyo ndiyo walikuwa DSM! Sinza walikuja baadaye sana! Weka pembeni wale wa kishua from Masaki, Osterbay na Upanga wale walikuwa next level!

Usishangae sana sekta ya michezo na burudani kutawaliwa na watoto wa hayo maeneo! Halafu kwenye biashara na uongozi wamejaa watoto wa kishua kutoka pande hizo! Unaweza kuta hata wanaotamba huko shamba kumbe alitoka DSM!

Sifa kuu ilikuwa kupendana na kutojiona bora kuliko wengine hata kama umetoboa!

Leo mtu akipata kinyumba na gari anahisi ameyapatia na kuwadharau hata wenyeji waliompkea na kuwaona hawana akili! Ukifuatilia makuzi kumbe alikulia shamba! Siyo wote lakini!
 
Enzi hizo kulikuwa na upendo wa kweli...mtu alikuwa ana zamia kwa kucholewa ramani na kweli ramani inaenda kumfikisha anapo pataka.

Yani wahuni wa enzi hizo walikuwa wanavuta bhangi na kupeana michongo ya maana ila wahuni wa siku hizi wanavuta bhangi Hadi wanakuwa mateja...!

Mimi ni chimbuko la vijana wa enzi hizo wa magomeni ila sikuwa muhuni🤣🤣🤣

Ile munkari ya kwenda nje nilikuwa nayo pia🤣🤣🤣​
 
Back
Top Bottom