Muhimbili, kulikuwa na haja gani ya upasuaji kutenganisha watoto mapacha?

Sio kwenye afya ya binadamu aiseee
Mzee kifo hakikwepeki, uzuri wale wametoka theatre vizuri tu, suala la msingi ni kujiuliza je, kifo chao kimesababishwa na makosa katika huo upasuaji?

Operation ngapi za kutenganisha watu huko kwa waliotuzidi teknolojia nao wamekufa?
 
nimekuandikia hapa nikiwa najua ninachoongea wewe unaongea theory mimi nime practice mambo kama haya haya japo nyanja tofauti kidogo wewe unaongwa sawa na wale wanaosema ilani.
 
Mzee kifo hakikwepeki, uzuri wale wametoka theatre vizuri tu, suala la msingi ni kujiuliza je, kifo chao kimesababishwa na makosa katika huo upasuaji?

Operation ngapi za kutenganisha watu huko kwa waliotuzidi teknolojia nao wamekufa?
anyway kila mtu na jinsi anavyoona ila kwa bongo naona bado sana
 
Naunga mkono hoja,wangewapeleka wale pacha Nje ya Nchi na wataalamu wetu wangeshiriki kuliko kufanyia majaribio watoto wa mwenzio..

R.I.P pacha.
 
anyway kila mtu na jinsi anavyoona ila kwa bongo naona bado sana
Yes, si lazima tufanane mitazamo, nakubaliana nawe bongo bado kiutaalamu na expirience pia.

Lakini kama walitoka theatre salama, na vifo vyao havijasababishwa na makosa ya daktari, madaktari hawana lawama,

Pili hata huko walikotuzidi teknolojia na expirience, nao wana vifl kibao vya watu wanaotenganishwa.
 
Mbna Ile ya kule walikopelekwa uarabun ulifanikiwa.. don't put ur theories sema walijal kupata Jina kuliko gharama za maisha ya hao watoto. Ukwel ni Kuwa hili zoez lilikuwa gumu sana Kwa upande wao. Na ninadhan ndo po Yao ya kwanza Kama sikosei,? Kuna vitu vingi vilitakiwa kuangaliwa vizur.

Najua Pia Kuwa Kama ingefanyika njee na watoto wangefarik lawama zisingekuwepo kutokana na teknolojia na ubobevu walionao wenzetu.

Ila Kwa muhimbil mtuache tuwalaumu tu ni njuka kwenye Hyo kazi so lawama lazima wapewe tu Kwa kweli, hata wao watakuwa wanafanya analysisi wapi walipokosea Jpo kiprofeshno hawawez kutuambia.
Muhimbil mnastahil pongezi kidoogo lawama nyingi sana
 
Yule dokta aposema kwamba walipata ugumu sana kutokana na mapacha hao ku share ini nikajua tu !!
 
Kitaalam bado wangekuwa na uwezekano mkubwa wa kufariki wakiwa watu wazima, kama ilivyotokea kwa wale mapacha wawili wa Iringa; Maria na Consolata.

Hivyo upasuaji ulikuwa haukwepeki.
Lakini waliishi Miaka Zaidi ya 20yrs huoni ni Neema hyo
 
Kama aliye wekewa moyo wa nguruwe huko kwa mabeberu Marekani hatunaye na ndiko unakokokusifia kwamba hawana majaribio, basi Madaktar wetu wamethubutu na wameweza.Lengo halikua kuua bali kuwatenganisha kila mtu aishi kivyake na aenjoi privacy yke binafsi
 
Kila Kitu Kina level yake, Hyo Op Kwao ilikuwa kubwa Sana kuliko uwezo wao. Na kingne walitaka publicity, Leo yametokea ya kutokea Wacha walaumiwe tu.
 
Nimechelewa kukutana na huu uzi na tayari kuna comment nyingi hivyo nadhani nitakacho comment huenda Mwingine kesha elezea.

Kwanza kazi ile haikufanywa na Madaktari wa Tanzania peke yao.

Pili bila shaka wewe sio Daktari na hukubahatika kuwaona hao Watoto wanaozungumziwa hapa..mimi pia, ila kwa kuelezewa tu namna walivyokuwa huoni kuwa bado walikuwa kwenye changamoto?.

Hivi huoni kuwa kujaribu kuwasaidia mapema kuliko kuwaacha wakomae ili hali nafasi yao ya kuishi kama Binadamu wenzao wengine ilikuwa rehani?.

Na kama wangekutana na tatizo kubwa mbeleni huoni kuwa bado ingeonekana kwa nini hawakuamua angali wakiwa bado viungo havijakomaa.

Kwa maoni yangu ni bado tu ingefika mahali wangekwama na ingebaki kusubiri wapoteze maisha mmoja baada ya mwingine bila nafasi wala uwezo wa kuwasaidia kwa wakati huo...maisha yao yalikuwa 50 kwa 50 kama hata sio chini ya hapo.
 
Ukishaingia ICU theater una mambo mawili tu, kufanikiwa kupona ama kufa, hata hivyo madaktari walijitahidi kadri walipoweza na hakuna namna unaweza kuwalaumu kwa sababu walifanikisha zoezi,na patients waliendelea kusurvive. Mengine mwachie Mungu.
Mapacha waliiungana hata ulaya wapo na wengine huachwa hadi wanazeeka kama possibilitues za fatallity baada ya operation ni kubwa.
Kuna mengi sana yanaangaliwa hadi operation ya kuwatenganisha iruhusiwe.
Mimi sio dokta au expert lakini kupitia documentaries na maarifa ya huku ba kule , nafahamu fika kuwa kutenganisha watoto walioungana sio kitu cha mzaha mzaha.
 
Kila upande una tabia ya kumdiss mwenzie.
Kuna dokta mmoja alikuwa anatusema Sana kwamba tunalala tunaamka kazi yetu Ni mpira na tunacheza hovyo Kama wehu, je tungekuwa madaktari nchi ingekuwa nyeupe hii.

Haya Sasa watu 30+ Operation iliozaa matokeo kifo.
#Narudi kwa dokta muda huu
 
Madaktari wengine wa huku jf tunasema, pale Muhimbili wale doctors wangeangalia possibility ya kuokoa mtoto mmoja,

Vinginevyo wengeamua kuomba msaada huko nchi za wenzetu
 
Hakukuwa na haja
..Nilivyoona ile habari jana nikajisemea moyoni kuwa aheri wangebaki tu vilevile.
 
Kwenye operesheni kama hiyo hata kwa mabeberu chance of survival huwa ni ndogo sana
 
Ila tukubaliane tu hata hao mabeberu nao walianza hivi hivi. Hivyo wakati mwingine tuwaunge mkono madktari wetu kwa jitihada zao.

Sidhani kama walidhamiria kutokea kwa hayo mauti ya mabinti zetu wapendwa.
Wewe unaweza kubali mwanao afanyiwe majaribio?
Ni kweli mabeberu walianza hivyo..lakini nadhani kulikuwa na haja ya kuwapeleka huko ili madaktari wetu pia waende kujifunzia huko wakiwa chini yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…