Hatukutakiwa kufanya majaribio kwenye uhai wa watu Kwa kifupi walikuwa wanatafuta publicity
Mbona wale mapacha wa Mbeya walipona acheni kuingiza Siasa kwenye taaluma za watu.Naomba uelewe kuna chama cha ma daktari bingwa duniani hasa wa upasuaji.Pasuaji kama hizi zikitaka kufanyika wanapeana taarifa kuhusu uwezo na taaluma wanaofanya hivyo na WHO lazima wajue hilo ndio go ahead inatolewa
Mwaka 1986 prof Philip alifanya upasuaji kama huu Muhimbili na akafanikiwa.
Kwa taarifa yako kama hujawahi fanyiwa operation huwezi Jua kila operation ina ukubwa wake hata kupasuliwa jipu ni operation pia lakini anakufanyia ni dk mmoja tu.Na inatemea limetokea wapi.
Ikifika issue kama hii watoto kuungana pamoja inategemea wameungana sehemu gani kuna wanaoungana sehemu ambazo ukizikata hakuna madhara.
Ila ikifikia hatua wameungana kwenye viungo nyeti sana kwa mwili wana share mfano maini,figo,kichwa,tumbo issue inakuwa very complicated na ndio maana utasikia kunakuwa na wapasuaji hata 20 mabingwa kila mmoja anakuja anafanya chake anamuachia mwingine afanye yake nitakupa mfano.
Kwa upasuaji kama huo kunakuwa na bingwa wa dawa ya usingizi anakuja anafanya part yake anaondoka,anakuja bingwa wa mifumo ya hewa anafanya yake anaondoka,kunakuwa na bingwa wa damu anafanya yake anaondoka,anakuja bingwa wa moyo na mishipa ya fahamu anafanya yake anaondoka,anakuja bingwa wa maini yaani hepatologist huyu ndio main stelling kwenye operation hii maana tatizo ndio liko kwake nimekupa mfano tu hapo kwa hiyo unakuta ni jeshi kubwa mno usifikirie ni mmoja tu anakata na kumaliza operation inaweza chukua hata masaa10.
Ni vigumu hapo kusema ni nani alikosea hapo hapo ukae ukijua kuna bwana mkubwa kuliko wote hao ambaye ndio daktari bingwa wa dunia na ulimwengu mzima anaitwa MUNGU.
Naongea haya kwa ushahidi nina mdogo wangu wa kike ni dr bingwa wa upasuaji wa watoto alishiriki kutenganisha wale watoto wa Mbeya kwa mafanikio makubwa ndio alinieleza yote haya.
Hawa ma dr wanahistahili pongezi.
Nchi hii inashida moja mambo mengine watu wanaingiza siasa