PreGE2025 Muhtasari wa Hoja: Madhara ya kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi

PreGE2025 Muhtasari wa Hoja: Madhara ya kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hii ingekuwa mtaji kwa 2030, pengine wangevipandisha hadi 100-120 you never know
Wewe unataka CHADEMA waamini kitu ambacho hata wewe mwenyewe (mshauri) hukiamini; siyo maajabu haya?
Ni katika mlengo ule ule wa hadaa na ulaghai unaotumiwa na mama,... hivi kuna shule mnako somea udanganyifu wa wazi kama huu? Hizi tamaduni za kigeni mnazoiga sasa waTanzania wamezigundua uhalisia wake ulivyo.
 
Wenye akili karibu wote wapo CCM ila mafisadi wamewashika akili Yao na hawajui wanachomokaje kwenye hiyo mikono miovu maana mbele Yao wanahitaji livelihoods na nyuma yupo ambaye ameshikilia huo ugali akiwagawia kimkakati🥲
Sasa mwenye akili ni nani hapo...!?..Mafisadi au hao "wenye akili"..!?
 
Nchi imeingizwa kwenye mtego na mgogoro na msajili kwakujua ama kutokujua...CDM watazuia uchaguzi kirahisi zaidi sasa kuliko kabla...CDM Wana haki ya kwenda mahakamani kuzuia uchaguzi kwakua ni haki Yao kikatiba kushiriki uchaguzi na hakutakuwa na uchaguzi mpaka huo utata wa tume utakapopatiwa ufumbuzi na hiyo ita set precedence ya kutokuwa na Imani ya hicho chombo.. whoever advised Tume na wao kukubali wamemeza ndoana kirahisi sana......Thinking loud!
Mahakama ipi?

Amandla...
 
Hizi ni habari za kuokoteza kwenye vijiwe vya kahawa.

Mimi nimekua kwenye hizo chaguzi tangu mwaka 1995 najua kila kinachofanyika .
Hii nchi imetulia kwa sababu Nyerere alijenga misingi ya ujamaa .
Kule Zanzibar hakuna kuvumiliana kwa sababu ya misingi yake,

Kulinganisha uchaguzi wa Lowasa na Nyingine ni kufikiri kwa kutumia mataqo.
Kwanza Lowasa angekua na afya nzuri kabisa uchaguzi wake usingeporwa . Walihofia kuwa atafia madarakani maana genge la wahuni walikadiria kuwa walichomfanyia hangetoboa .

Matendo ya CCM ya Azimio la Zanzibar ni CCM ya watu binafsi sio ya Jamii nzima .
Hawa mpaka ikulu ni mali yao ndio maana haieleweke iko Dodoma au Chato au Kizimkazi au Dar es salaam.

Kama vile CCM wanavyowachukia wapinzani wao basi hivyo hivyo wanajenga hulka kwa wapinzani na mwisho ni kulipizana visasi huko mitaani .

Kizazi kilichopo ni kizazi kisicho na hulka ile ya ujamaa kuanzia kwenye familia
 
Maelezo mengine kutoka vijiwe vya kahawa.
 
Kupata haki is a process siyo QED. Mimi naamini kama CHADEMA wangeshiriki uchaguzi wa Oktoba 2025 wangepata hata viti 70 vya ubunge.

Hii ingekuwa mtaji kwa 2030, pengine wangevipandisha hadi 100-120 you never know.

Ukijijenga kwenye ubunge unakuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya miswaada mibovu na sheria mbovu. Hata kuleta Katiba mpya kwaweza kuanzia bungeni kuliko hii inayotafutwa kwa kutumia public sympathy.

Chama hakina Wazee wa kutoa ushauri. Tundu mwenye miaka 57 sasa ndiyo Mzee wa chama, hana mtu juu wa kumshauri.

Hao G55 kuna watu wazuri sana, lakini ame wa-ignore kabisa na kuanza kuwafukuza kwenye teuzi.

Heche naye ni mtu mwenye munkari. Lema yeye ni mtu wa FURSA, na anapita palipo na shillingi.

Unapata wapi watu wa kuishauri CHADEMA vizuri
Uchaguzi wa 2020 na Serikali za mitaa walienguliwa na tume hiihii au hii ni nyingine, shida tume yenyewe
 
1. Maadili ya Uchaguzi ni Suala la Kisheria

Yameainishwa katika Kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024.

Tume ya Uchaguzi hutunga kanuni hizo kwa mashauriano na vyama vya siasa na Serikali, kisha huzichapisha kwenye Gazeti la Serikali.

2. Nani hupaswa kusaini?

Sheria inahitaji kila chama cha siasa, kila mgombea, Serikali na Tume kusaini.

Mgombea anapaswa kusaini kabla ya kuwasilisha fomu ya uteuzi.

3. Wakati wa Kusaini ni Upi?

Sheria haijaweka muda mahsusi kwa vyama au Serikali kusaini.

Kwa mantiki hiyo, chama kinaweza kusaini wakati wowote kabla ya kuanza kampeni.

4. Tafsiri ya “Kusaini” Kisheria

Neno “ kusaini ” halijapewa tafsiri finyu; linaweza kumaanisha pia kuridhia au kukubaliana kwa namna yoyote rasmi.

Mgombea anaridhia kanuni zilizopo, hata kama hajasaini moja kwa moja.

5. Madhara ya Kutosaini

Sheria haijaeleza adhabu au athari ya moja kwa moja kwa chama au mgombea asiyesaini.

Haki ya kushiriki uchaguzi ni ya kikatiba na haiwezi kuondolewa kwa kutokuwepo saini ya kanuni.

Kifungu 162(2) kinaelekeza waliotia saini kuzingatia kanuni, lakini hakielezi kuhusu wasiosaini.

Hii inaacha mwanya wa kisheria (lacuna) unaoweza kutumiwa na baadhi ya wadau.

6. Hitimisho

Sheria hii ina utata na inaweza kuleta sintofahamu katika utekelezaji.

Kukataa au kushindwa kusaini hakumaanishi kufutwa kwa haki ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi.

Haki inaweza kuondolewa tu kwa msingi ulioelezwa wazi na Sheria au Katiba, si kwa tafsiri au hisia.

Imeandikwa na Mhe. Edson Kilatu, esq.,

View attachment 3302325
Hebu tuambie kwanini sheria huwa zinatungiwa kanuni? Lengo la kanuni ni nini?

Katika hili kanuni zinasemaje?
 
Kupata haki is a process siyo QED. Mimi naamini kama CHADEMA wangeshiriki uchaguzi wa Oktoba 2025 wangepata hata viti 70 vya ubunge.

Hii ingekuwa mtaji kwa 2030, pengine wangevipandisha hadi 100-120 you never know.

Ukijijenga kwenye ubunge unakuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya miswaada mibovu na sheria mbovu. Hata kuleta Katiba mpya kwaweza kuanzia bungeni kuliko hii inayotafutwa kwa kutumia public sympathy.

Chama hakina Wazee wa kutoa ushauri. Tundu mwenye miaka 57 sasa ndiyo Mzee wa chama, hana mtu juu wa kumshauri.

Hao G55 kuna watu wazuri sana, lakini ame wa-ignore kabisa na kuanza kuwafukuza kwenye teuzi.

Heche naye ni mtu mwenye munkari. Lema yeye ni mtu wa FURSA, na anapita palipo na shillingi.

Unapata wapi watu wa kuishauri CHADEMA vizuri
Hizo hisia za kupata viti 70 sijui 100 au 20 mnazitoa wapi? Chadema wameenda kiuhalisia zaidi au kisayansi kuliko hisia. 2019 wamepigwa chini viti vya mitaa, 2020 wamepigwa chini ubunge, 2024 wamepigwa chini viti vya mitaa Tena bila huruma. Ni kitu gani kina kupa moyo kwamba 2025 Dola au Tume ya uchaguzi itawaonea huruma iwaachie hivyo viti vya ubunge!?
 
Usipokuwa na dream (hisia) huwezi kufika popote. Hata kama utakuwa umelenga kupata 70, pengine waweza kuangukia 30 au 40, siyo mbaya.

Huwezi kuishinda CCM kama utakuwa nje ya mfumo kama raia
 
Yale yalikuwa maamuzi ya Mwendazake na ndiyo maana alikufa kwa dhambi zake.
Kufa ni wajibu na kila mtu atakufa. Adhabu mtu anapata hapahapa duniani kama kufungwa, kuumizwa kivyovyote vile.
 
Lowasa alikua na Wakurugenzi wengi waliokua wanamuunga mkono .
Ni wazi kama Lowasa angekua na ujasiri wa Tundu Lisu angeingia ikulu asubuhi na mapema . Bahati Mbaya sana watanzania ni wasahaulifu .

Lowasa alikua anapokelewa uwanja wa ndege na RPC na kusindikizwa mpaka kwenye uwanja anayofanyia mkutano 📌🔨.
Afya ilim-bugudhi pia mwamunyange alivyotengenezewa ugonjwa Kwa Sumu , wakuu wa idara wengine usalama na IGP wakafyata maagizo ya Mzee lowasa
 
Back
Top Bottom