Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Mi lisoma Agriculture,na baadhi ya Practical tulienda mabuctcher ya nguruwe na tulikuwa na Waislam, wengine tuliokuwa tunamtumia mdudu tulichomewa kidogo na kula,ni mwanangu Dula tu hakutaka unafiki nayeye alipiga......Kwa kazi sioni shida mwite tu aje amtibu huyo Veterinary Ofdicer
 
Tupe aya au hadith sheikh kuhusu uharam wa sigara.
Uharamu wa sigara

Uvutaji sigara unaharibu matendo ya ibada ya mtu na yanampunguzia malipo. Kwa mfano, inaharibu Swalah, ambayo ni nguzo ya Diyn. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:



“Yeyote anayekula kitunguu thomu au kitunguu maji, akae mbali na sisi na misikiti yetu, na akae nyumbani mwake. Malaika hakika wanaumia kwa mambo ambayo yanawaumiza wanaadamu.” [Imesimuliwa na Jaabir na Swahaba wengine. Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



Wale wenye unadhifu na maumbile yasiyochafuliwa, hapana shaka yoyote kwamba harufu mbaya inayotoka mdomoni mwa mvutaji sigara inakirihisha na imeoza zaidi kuliko ile inayotoka kinywani mwa mtu aliyekula kitunguu thomu au maji. Hivyo, mvutaji sigara yupo baina ya hiari mbili, aidha kuwadhuru watu wanaoswali kwa harufu yake iliyooza na pia malaika, au kuikosa Swalah ya jama'ah.



Uvutaji sigara pia unaharibu funga. Swawmu ni ngumu sana kwa mvutaji sigara. Pale tu siku inapomalizika, anakimbilia kuivunja funga yake kwa uovu wa sigara badala ya utamu wa tende au maji safi. Hata kama akifunga katika mwezi wa Ramadhwaan, mvutaji ana kuwa dhaifu wa kufunga siku zengine. Hivyo, anapoteza malipo bora ya yule anayefunga angalau siku moja kwa ajili ya Allaah.
 
Poleni na majukumu wakuu.
Niende kwenye mada,hivi dakitari wa wanyama (vet) muislam ana ruhusiwa kutibu nguruwe?

Kama hapana je pale vyuo vya kilimo huwa naona wakifuga wanyama tofauti tofauti akiwemo na nguruwe au taaluma haina dini?

Kama ndiyo basi daktari hatakiwi kuwa na itikadi ya dini yoyote kwa maana hakuna kitabu cha dini yotote kinachoruhusu kula nguruwe ila kama mimi sijaelewa basi naomba wajuvi wa mambo haya mnisaidie[emoji120]
Pumbavu wewe kwani Kuna kitabu kinachoruhusu kula binadamu? Mbona waislam wanatibu binadamu?
Au umeambiwa watibu vitu wanavyokula tuu?
 
Poleni na majukumu wakuu.
Niende kwenye mada,hivi dakitari wa wanyama (vet) muislam ana ruhusiwa kutibu nguruwe?

Kama hapana je pale vyuo vya kilimo huwa naona wakifuga wanyama tofauti tofauti akiwemo na nguruwe au taaluma haina dini?

Kama ndiyo basi daktari hatakiwi kuwa na itikadi ya dini yoyote kwa maana hakuna kitabu cha dini yotote kinachoruhusu kula nguruwe ila kama mimi sijaelewa basi naomba wajuvi wa mambo haya mnisaidie[emoji120]

Mbona wanaruhusiwa kumla under conditions. Au hujui
 
Kuna mtu nimemjibu, kuwa imani na ubinadamu ndicho kinachotofanya tuwe na mipanga na baadhi ya mambo, ingawa ukifanya hakuna madhara ya moja kwa moja.

Ni nini kinachokuzia kutembea na ndugu yako wa Damu, ikiwa maumbile ni yaleyale mimba itaingia na mtu atazaa.
Mkuu tatizo unahamisha mada. Tuzungumzie madhara ya nguruwe bila kujusisha vitu vingine.
 
Acheni upotoshaji bandugu. Ngurue na mbwa ni kharam kula sio kufuga, kuna kisa kimoja kinasimuliwa ktk sira mwanamama mmoja ataingia peponi kwa kumsaidia mbwa maji yakunywa. So tuwapende wanyama kwa wale tuliozuiwa kuwala tusiwale ila fi dharurat.
 
Nguruwe ana madhara gani?
Kulingana na Uislamu vitu vinaharamishwa kwa sababu nyingi; ima kwa hekima, au bila hekima ikiwa ni sehemu ya mitihani na kupimwa viumbe utiifu wao, na kwa hekima mfano ni vichafu au vina madhara. Ikiwa kitu chochote kina madhara kinakuwa haraam; na kikiwa kina manufaa kinakuwa halaal; na kikiwa madhara yake ni makubwa kuliko manufaa kitakuwa ni haraam; ilhali madhara yake yakiwa ni kidogo kuliko manufaa kinakuwa ni halaal
 
Bata na nguruwe nani msafi zaidi ya mwezie.??

#MaendeleoHayanaChama
Kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu na hawana dini basi waendelee kuongozwa na utashi wao na maono ya kisayansi. Kwa anayemwamini Mungu atafuata maelekezo yake BILA KUHOJI chochote. Usiulize kwa nini Mungu unayemwamini amekataza kula nguruwe. Huko ni kukosa imani au kumkufuru Mungu. Yeye Mungu hahojiwi wala hachunguzwi. Kumbuka kukataza kula inawezekana kusihusiane na kukataza kutibu
 
Dini zimebaki kutisha wayu eti ukifa ukifa nyoko..hivi ulikua wapi kabla hujaja duniani??

#MaendeleoHayanaChama
Kama Hadi sasahivi hujui nilikua wapi kabla sijaja duniani Basi wewe nipimbi wakutupwa.
 
hivi dakitari wa wanyama (vet) muislam ana ruhusiwa kutibu nguruwe?
Jibu ni: Ndio km anawatibu wala Nguruwe anashindwaje kumtibu Nguruwe?

Udaktari ni wito ni sawa na kujitoa Sadaka hakuna udini huku,
 
Nguruwe ana madhara gani?
Nguruwe ana madhara aya hapa.

KUWA NA VITU VYENYE SUMU

Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi sana. Ikiwa italiwa, mafuta huchanganyika na damu. Kwahiyo, damu huchanganyika na chembechembe za mafuta. Kiwango hiki kikubwa cha mafuta husababisha magonjwa yanayojulikana kama, arteriosclerosis, presha (hypertension) na magonjwa ya moyo (heart infarct). Zaidi ya hayo, vitu vyenye sumu vijulikanavyo kama sutoxines vinapatikana kwenye siagi (lard). Matezi ya limpathik (Lymphatic glands) hulazimika kufanya kazi ngumu ili kuondoa chembechembe hizo za sumu ambazo huingia mwilini. Husababisha maambukizi na kunyonya tezi zijulikanazo kama lymph nodes hasa kwa watoto. Koromeo la mtoto humeza na kuonekana kama la nguruwe. Hivyo basi, maradhi haya yanajulikana kama scrofulosis (maradhi ya nguruwe). Kama maradhi yataongezeka, tezi zote za lymph huathiriwa na kumezwa. Hali joto huongezeka; maumivu huanza na hali ya hatari sana hujitokeza.


KIWANGO KIKUBWA CHA SALFA


Tishu zijulikazo kama kolageni (collagen tissue) zilizopo katika mfumo wa majimaji kamasi (mucus) ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye nyama ya nguruwe, zina kiwango kikubwa sana cha salfa (sulfur). Hivyo, kiwango kikubwa cha salfa huchukuliwa na kuingizwa mwilini. Kiwango hiki cha ziada cha salfa hubaki kwenye misuli (muscles) na mishipa ya neva (nerves), na kusababisha maambukizi kwenye viungio (joints), calcification na ngiri (hernia) kwenye viuno (loins). Ikiwa mtu atakuwa na mazoea ya kula nyama ya nguruwe, sehemu ngumu (hard cartilage) kwenye mwili itaondolewa na tishu za kolageni zenye mfumo wa majimaji (kamasi) kutoka kwa nguruwe. Hatimae, fuvu gumu linalainika; haliwezi sasa kuhimili uzito wa mwili na huvunjika. Hivyo basi, uharibifu kwenye viungo huanza kujitokeza. Miili ya wanaokula nyama ya nguruwe huwa legevu kama jeli; tabaka za mafuta hutengenezeka. Kwa mfano, mwanamichezo akila nguruwe, huwa mchovu, mvivu na kutokuwa madhubuti. Baadhi ya wachezaji wa mpira hufikia hatua ya kukata tamaa kwasababu ya matumizi ya nyama ya nguruwe.


UKUAJI KUPINDUKIA


Kiwango cha vichocheo vya makuzi (growth hormone) kwenye nguruwe ni vingi kupita kiasi. Kitoto cha nguruwe ambazo kina uzito wa gramu mia kadhaa anapozaliwa huwa na kilo mia kwa miezi sita tu. Kwa kiwango hicho cha makuzi ni kutokana na kiwango kikubwa cha vichocheo vya makuzi (growth hormone). Homoni ya makuzi inayobebwa na nyama ya nguruwe husababisha kumezwa kwa tishu na maambukizi kwenye mwili. Husababisha pua, kidevu, mkono na mifupa ya miguu kukuwa katika hali isiyo ya kawaida na mwili kuganda mafuta. Jambo la hatari zaidi kwenye homoni hii ya makuzi ni uwezekano wa kufungua njia ya kupata saratani (cancer). Kwakweli, wachinjaji wa nguruwe wanaeleza kwamba nguruwe dume hupata saratani baada ya umri fulani.


MARADHI YA NGOZI


Chembe chembe zinazojulikana kama histamine na imidazole kwenye nyama ya nguruwe husababisha maumivu kupita kiasi. Pia hurahisisha kutokea kwa maradhi ya kuambukiza ya ngozi kama vile ugonjwa unaojulikana kama eczema, damatiti (dermatitis) na nyurodamatitis (neurodermatitis). Chembechembe hizi huongeza hatari ya kutokea majipu (boils), kidole tumbe (appendicitis), magonjwa ya kibofu (gall bladder diseases), venali (venal) na maambukizi ya ateri (arterial infections). Kwa sababu hiyo, madaktari huwashauri wagonjwa wa moyo wasile nyama ya nguruwe.

NYAMA YA NGURUWE NA MNYOO UJULIKANAO KAMA TRICHINA


Moja ya maradhi hatari sana ambayo yanaaambukizwa kwa mwanadamu kupitia nyama ya nguruwe ni trichina. Ingawa, trichina hausababishi tatizo kubwa kwa nguruwe mwenyewe. Hata hivyo, mnyoo huu unasababisha maradhi hatari sana kwa wanadamu. Mnyoo wa trichina humezwa kupitia nyama ya nguruwe na kwenda kwenye damu kupitia utumbo mkubwa na utumbo mdogo. Hivyo basi, hutapakaa mwili mzima.


Minyoo ya trichina hukaa hasa kwenye tishu za misuli kwenye magego, ulimi, shingo, koo na maeneo ya kifuani. Husababisha kupooza kwenye kutafuna, kuzungumza na misuli ya kumezea. Pia husabisha vikwazo kwenye mishipa, tatizo la meningitis na athari kwenye ubongo. Na hatari zaidi zinaweza kusababisha kifo. Jambo la hatari katika maradhi haya ni kwamba hayana tiba sahihi. Ugonjwa wa trichina ni maarufu hasa kwenye nchi za Ulaya. Mripuko wa maradhi ya trichina umeshuhudiwa kwenye nchi kama vile Uswidi (Sweden), Uingereza, na Poland, licha ya udhibiti wa mifugo. Uturuki, mripuko wa ugonjwa wa trichina haujawahi kuonekana isipokuwa kwenye jamii za Wakristo wanaoishi Uturuki.


CHAKULA NA TABIA YA MWANADAMU


Wanadamu na wanyama huathiriwa na vyakula wanavyokula kwa kiasi fulani. Kwa mfano, inajulikana kwamba wanyama wanaokula nyama (carnivorous) kama paka, mbwa na simba ni wakali na wanyama wanaokula majani (herbivorous ) kama kondoo, mbuzi na ngamia ni watiifu na wapole. Na hivyo hivyo kwa wanadamu. Imeonekana kwamba watu wanaokula mboga kwa ujumla wao ni wapole, na wale wanaokula nyama na yatokanayo na nyama ni wakali. Nguruwe ni mnyama pekee ambae hana wivu kwa mwenza wake wa kike. Imegundulika kuwa hisia za wivu zinadhoofika au kuisha kabisa kwa wanaotumia nyama ya nguruwe. Katika kulipa umuhimu jambo la athari za chakula kwenye tabia, Savorin, mwanafalsafa wa Kifaransa amesema “Niambie unachokula, ntakuambia wewe ni nani.”...

ukitaka jibu la nyongeza au ufafanuzi zaidi pia nipo kwa ajili yako mkuu
 
لا محرم مع الضرور (hii ni kanuni ya kisheria ''Hakuna uharamu inapojitokeza dharura iliyoruhusiwa na sheria"
Mfano..huna kosa Kama utakula mchana wa ramadhan kwa dharura ya maradhi,hedhi,nifasi,uzee, n.k
(2)Hakuna kosa kuonesha uchi wako kwa daktari tofaut na jinsia yako kwa dharura ya kutokuwepo hyo hospitali au hao wahudumu n.k
(3)Hakuna kosa kuvunja ndoa kwa dharura ya maradh mfano ya kuambukiza au mume jogoo hasimami n.k
Kwahyo sheria hii inaruhusu kufanya hilo jambo kwa mlango Huo
N:B ..Dharura iliyoruhusiwa na sharia ni ile ambayo Kama utafanya kinyume chake yatatokea madhara.
 
Kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu na hawana dini basi waendelee kuongozwa na utashi wao na maono ya kisayansi. Kwa anayemwamini Mungu atafuata maelekezo yake BILA KUHOJI chochote. Usiulize kwa nini Mungu unayemwamini amekataza kula nguruwe. Huko ni kukosa imani au kumkufuru Mungu. Yeye Mungu hahojiwi wala hachunguzwi. Kumbuka kukataza kula inawezekana kusihusiane na kukataza kutibu
Kwanini asihojiwe..kama alimua kutupa huo utashi kwa nini tusihoji..hizi dini ni ukanjanja tu wa watu..ndio mana kuna mahali wanasema zijaribuni kila roho..sio zote ni imani za Mungu zingine ni za shetani..hivyo kuhoji kunataka kufahamu ipi ni ipi.

Usiwe kama kikondoo wa kupelekeswa tu na kila jambo..lazima ulihoji uhalali wake.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom