Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Kama Hadi sasahivi hujui nilikua wapi kabla sijaja duniani Basi wewe nipimbi wakutupwa.
Wewe ndio upimbi..mana hujui uliko toka na hujui utakako kwenda zaidi ya kukaririshwa illusions za wajinga wa zamani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wale ni viumbe wa Mungu haitakiwi wateseke. Tutawatibu vyema
 
Nguruwe ana madhara aya hapa.

KUWA NA VITU VYENYE SUMU

Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi sana. Ikiwa italiwa, mafuta huchanganyika na damu. Kwahiyo, damu huchanganyika na chembechembe za mafuta. Kiwango hiki kikubwa cha mafuta husababisha magonjwa yanayojulikana kama, arteriosclerosis, presha (hypertension) na magonjwa ya moyo (heart infarct). Zaidi ya hayo, vitu vyenye sumu vijulikanavyo kama sutoxines vinapatikana kwenye siagi (lard). Matezi ya limpathik (Lymphatic glands) hulazimika kufanya kazi ngumu ili kuondoa chembechembe hizo za sumu ambazo huingia mwilini. Husababisha maambukizi na kunyonya tezi zijulikanazo kama lymph nodes hasa kwa watoto. Koromeo la mtoto humeza na kuonekana kama la nguruwe. Hivyo basi, maradhi haya yanajulikana kama scrofulosis (maradhi ya nguruwe). Kama maradhi yataongezeka, tezi zote za lymph huathiriwa na kumezwa. Hali joto huongezeka; maumivu huanza na hali ya hatari sana hujitokeza.


KIWANGO KIKUBWA CHA SALFA


Tishu zijulikazo kama kolageni (collagen tissue) zilizopo katika mfumo wa majimaji kamasi (mucus) ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye nyama ya nguruwe, zina kiwango kikubwa sana cha salfa (sulfur). Hivyo, kiwango kikubwa cha salfa huchukuliwa na kuingizwa mwilini. Kiwango hiki cha ziada cha salfa hubaki kwenye misuli (muscles) na mishipa ya neva (nerves), na kusababisha maambukizi kwenye viungio (joints), calcification na ngiri (hernia) kwenye viuno (loins). Ikiwa mtu atakuwa na mazoea ya kula nyama ya nguruwe, sehemu ngumu (hard cartilage) kwenye mwili itaondolewa na tishu za kolageni zenye mfumo wa majimaji (kamasi) kutoka kwa nguruwe. Hatimae, fuvu gumu linalainika; haliwezi sasa kuhimili uzito wa mwili na huvunjika. Hivyo basi, uharibifu kwenye viungo huanza kujitokeza. Miili ya wanaokula nyama ya nguruwe huwa legevu kama jeli; tabaka za mafuta hutengenezeka. Kwa mfano, mwanamichezo akila nguruwe, huwa mchovu, mvivu na kutokuwa madhubuti. Baadhi ya wachezaji wa mpira hufikia hatua ya kukata tamaa kwasababu ya matumizi ya nyama ya nguruwe.


UKUAJI KUPINDUKIA


Kiwango cha vichocheo vya makuzi (growth hormone) kwenye nguruwe ni vingi kupita kiasi. Kitoto cha nguruwe ambazo kina uzito wa gramu mia kadhaa anapozaliwa huwa na kilo mia kwa miezi sita tu. Kwa kiwango hicho cha makuzi ni kutokana na kiwango kikubwa cha vichocheo vya makuzi (growth hormone). Homoni ya makuzi inayobebwa na nyama ya nguruwe husababisha kumezwa kwa tishu na maambukizi kwenye mwili. Husababisha pua, kidevu, mkono na mifupa ya miguu kukuwa katika hali isiyo ya kawaida na mwili kuganda mafuta. Jambo la hatari zaidi kwenye homoni hii ya makuzi ni uwezekano wa kufungua njia ya kupata saratani (cancer). Kwakweli, wachinjaji wa nguruwe wanaeleza kwamba nguruwe dume hupata saratani baada ya umri fulani.


MARADHI YA NGOZI


Chembe chembe zinazojulikana kama histamine na imidazole kwenye nyama ya nguruwe husababisha maumivu kupita kiasi. Pia hurahisisha kutokea kwa maradhi ya kuambukiza ya ngozi kama vile ugonjwa unaojulikana kama eczema, damatiti (dermatitis) na nyurodamatitis (neurodermatitis). Chembechembe hizi huongeza hatari ya kutokea majipu (boils), kidole tumbe (appendicitis), magonjwa ya kibofu (gall bladder diseases), venali (venal) na maambukizi ya ateri (arterial infections). Kwa sababu hiyo, madaktari huwashauri wagonjwa wa moyo wasile nyama ya nguruwe.

NYAMA YA NGURUWE NA MNYOO UJULIKANAO KAMA TRICHINA


Moja ya maradhi hatari sana ambayo yanaaambukizwa kwa mwanadamu kupitia nyama ya nguruwe ni trichina. Ingawa, trichina hausababishi tatizo kubwa kwa nguruwe mwenyewe. Hata hivyo, mnyoo huu unasababisha maradhi hatari sana kwa wanadamu. Mnyoo wa trichina humezwa kupitia nyama ya nguruwe na kwenda kwenye damu kupitia utumbo mkubwa na utumbo mdogo. Hivyo basi, hutapakaa mwili mzima.


Minyoo ya trichina hukaa hasa kwenye tishu za misuli kwenye magego, ulimi, shingo, koo na maeneo ya kifuani. Husababisha kupooza kwenye kutafuna, kuzungumza na misuli ya kumezea. Pia husabisha vikwazo kwenye mishipa, tatizo la meningitis na athari kwenye ubongo. Na hatari zaidi zinaweza kusababisha kifo. Jambo la hatari katika maradhi haya ni kwamba hayana tiba sahihi. Ugonjwa wa trichina ni maarufu hasa kwenye nchi za Ulaya. Mripuko wa maradhi ya trichina umeshuhudiwa kwenye nchi kama vile Uswidi (Sweden), Uingereza, na Poland, licha ya udhibiti wa mifugo. Uturuki, mripuko wa ugonjwa wa trichina haujawahi kuonekana isipokuwa kwenye jamii za Wakristo wanaoishi Uturuki.


CHAKULA NA TABIA YA MWANADAMU


Wanadamu na wanyama huathiriwa na vyakula wanavyokula kwa kiasi fulani. Kwa mfano, inajulikana kwamba wanyama wanaokula nyama (carnivorous) kama paka, mbwa na simba ni wakali na wanyama wanaokula majani (herbivorous ) kama kondoo, mbuzi na ngamia ni watiifu na wapole. Na hivyo hivyo kwa wanadamu. Imeonekana kwamba watu wanaokula mboga kwa ujumla wao ni wapole, na wale wanaokula nyama na yatokanayo na nyama ni wakali. Nguruwe ni mnyama pekee ambae hana wivu kwa mwenza wake wa kike. Imegundulika kuwa hisia za wivu zinadhoofika au kuisha kabisa kwa wanaotumia nyama ya nguruwe. Katika kulipa umuhimu jambo la athari za chakula kwenye tabia, Savorin, mwanafalsafa wa Kifaransa amesema “Niambie unachokula, ntakuambia wewe ni nani.”...

ukitaka jibu la nyongeza au ufafanuzi zaidi pia nipo kwa ajili yako mkuu
Kila mnyama ana magonjwa ndiomana huli nyama yoyote bila kuipika ikaiva vzr usimsingizie nguruwe tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kila mnyama ana magonjwa ndiomana huli nyama yoyote bila kuipika ikaiva vzr usimsingizie nguruwe tu.

#MaendeleoHayanaChama
ebu soma kwanza hiyo comments hapo nadhani utajua utofaut wa nguruwe na wanyama wengine.

la nyongeza tu nguruwe wa kike anapata ada yake mwisho wa mwezi ( HEDHI & ANA BLOOD) . kama binadamu
 
ebu soma kwanza hiyo comments hapo nadhani utajua utofaut wa nguruwe na wanyama wengine.

la nyongeza tu nguruwe wa kike anapata ada yake mwisho wa mwezi ( HEDHI & ANA BLOOD) . kama binadamu
Hapo kwenye hedhi hujatumia sayansi zaidi ya kutumia myth tu..kuna cycle mbili tu nazo ni menstrual na estrous cycle..binadamu tu ndio mwenye menstrual wanyama wengine wote wana
estrous cycle.

Kadanganye wajinga wenzio huko madrasa..nikuulize tu swali la haraka tu huyo nguruwe ana bleed kwa siku ngapi?na ulishahudia hizo siku za bleed??

Kuhusu magonjwa ya wanyama hasa hiyo minyoo kuna taeni saginata pia wapo kwenye ng'ombe...infact hakuna nyama salama ndio mana unapika hadi ziive ndio ule..hata hao unaoita harari lazima uwapike waive ndio uwale usipo fanya hivyo lazima zoonotic diseases zikutandike na ukichelewa kupata matibabu unakufa.


#MaendeleoHayanaChama
 
Tatizo hapa sio kutibu nguruwe ila hawa madaktari wa mifugo huwa wanawala wateja wao
 
Hapo kwenye hedhi hujatumia sayansi zaidi ya kutumia myth tu..kuna cycle mbili tu nazo ni menstrual na estrous cycle..binadamu tu ndio mwenye menstrual wanyama wengine wote wana
estrous cycle.

Kadanganye wajinga wenzio huko madrasa..nikuulize tu swali la haraka tu huyo nguruwe ana bleed kwa siku ngapi?na ulishahudia hizo siku za bleed??

Kuhusu magonjwa ya wanyama hasa hiyo minyoo kuna taeni saginata pia wapo kwenye ng'ombe...infact hakuna nyama salama ndio mana unapika hadi ziive ndio ule..hata hao unaoita harari lazima uwapike waive ndio uwale usipo fanya hivyo lazima zoonotic diseases zikutandike na ukichelewa kupata matibabu unakufa.


#MaendeleoHayanaChama
Screenshot_20221114-142053.png



tuendelee kusema maendeleo hayan chama dr jiwe angavu
 
Nenda sua utawakuta madaktari wengi wa mifungo wanatibu wanyama wote hadi nyoka
 
Kilichowatuma kuandaa kombe ni kitu gani? Si wangewaachia wengine waandaye kama wao hawataki vitu haramu? Hilo wanalo kumkataza binadamu mwenye utimamu kitu akipendacho wao waandaye tu magereza sijui watafunga wageni wangapi, kwahiyo mlevi akilewa akae baa mpaka pombe iishe kichwani [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kweli wanalo, kitimoto italiwa tu mpaka kizazi chao watajifunza umagharibi.
 
Logically ingawa mimi sio dini yangu na hata kama wanakataza ndio anweza kumtibu...

Labda nikuulize wewe ukikutana na Shetani ana shida huwezi kumsaidia? Sababu nadhani kutoa msaada kuna pre-empt katazo la uharamu wake

Yaani kuacha kutoa msaada ni kuua; na nadhani kuna katazo la kuua pia..., Wewe kama Daktari umekula kiapo cha kutibu (sasa kuacha kutibu unavunja kosa la kuwajibika na ufisadi) Ufisadi which is Dhambi in anyone's books... (Hapa ya Kaisari anaachiwa Kaisari)
 
uislamu umetokea nchi ya jangwa na kumbuka jangwa hakuna nguruwe !. leo ulazimishe watu wale tende au ngamia wakati sehemu zengine hivo vitu havipo.
 
Labda cheti chake cha udaktari wa wanyama kina kipengele kinachomkataza kutibu nguruwe.
 
Poleni na majukumu wakuu.
Niende kwenye mada,hivi dakitari wa wanyama (vet) muislam ana ruhusiwa kutibu nguruwe?

Kama hapana je pale vyuo vya kilimo huwa naona wakifuga wanyama tofauti tofauti akiwemo na nguruwe au taaluma haina dini?

Kama ndiyo basi daktari hatakiwi kuwa na itikadi ya dini yoyote kwa maana hakuna kitabu cha dini yotote kinachoruhusu kula nguruwe ila kama mimi sijaelewa basi naomba wajuvi wa mambo haya mnisaidie[emoji120]
Achaneni na primitivity, tuko kaline ya 21
 
Back
Top Bottom