Toad darasa hapo mkuu hoja yako ipo very interesting
Popote penye conflict, mwanaume anapoambiwa asimame kama mwanaume, utaona anayepata manufaa ni mwanamke.
Mfano:
Kumuoa mwanamke aliyeshika ujauzito wako japo hamkupanga
Kulea ujauzito usio wako na mtoto asiye wako kwasababu umempenda mwanamke husika
Kumsamehe mwanamke anayezingua ili kukwepa kuvunja familia, ati watoto watapata shida
Kumuacha bila shari mwanamke uliyemjenga kimaisha pale anapopata mwanaume mwingine wa hadhi yake mpya
Tunategemewa tutafute hela, tuwahudumie, tuwasikilize, tuwakabidhi uhuru wetu, mali zetu na bado tusiwadai chochote mara tu wanapobadilisha mawazo ya kuwa nasi kimapenzi kwa sababu wanazozijua wenyewe.
Kwa kulitambua hili, vijana wanatakiwa wajiandae kisaikolojia, na wasijisahau wanapokuwa kwenye mahusiano kiasi cha kuwekeza imani na mategemeo yao yote kwa mwanamke mmoja. Wanatakiwa wajue siku ikifika, mwanamke hatajali yote unayofanya au uliyofanya kwa ajili yake.
Wanaume wengi waliopigwa matukio heavy wana msemo mmoja "I didn't see it coming - Sikulitarajia hilo kabisa"
Hivyo vijana inabidi walitarajie hili na wachukue hatua za kujilinda. Waache kujisahau pale mahusiano yanapokwenda vema. Waulinde uhuru wao kwa gharama zote, na wailinde hadhi yao kama wanaume. Waulinde uanamme wao, wasiruhusu uchezewe na mwanamke awapande kichwani.
Wawe na utayari na uwezo wa kumuacha mwanamke mara tu anapotikisa kiberiti. Msimamo ndio unajenga heshima kwa mwanamke.