Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Kwanza marehemu Said alikuwa kolo Sana,Hana exposure,yaani akajua hapa duniani huyo swala ndio mwisho hakuna wanawake wengine!..na Nyie wanaume wa humu wote mnajifanya kumsupport Said hamna exposure Kama marehemu...Maisha Ni zawadi nzuri tuliyopewa huwezi poteza uhai wako kisa mtu wakati Kuna mamilioni ya watu ulimwenguni,,eti alikuwa anampa hela kwa hela gani Bwana za kumtoa mtu uhai?kwa hiyo mitumbwi ya mbao?Sasa Kama issue Ni uchungu wa pesa Bill gate itabidi atumie Nukes

Nimekupenda sana!
Joannah
Mwanaume anaeuwa auwawe tuu hakuna namna!
Utamuuaje mtu Mzima mwenzako?
Wewe mwanaume Ukikosa nani anakuadhibu?
Kama Umemshindwa mwanamke kwaninibusimrudishe kwao?
Inaudhi sanaa kwa wanaume wanaochukua maamuzi ya Kidwanzi eti anauaaa..Wanaume woote wanaoua nao wauwawe tuu..
Kazi ya Kuua ni ya Alieumba tuu
Over!
 
Ndio ujinga wa kujiona pisi kali huku akili za kisoda. Itaishia kudanga mwishowe uzeeni unaanza kusimbua watu. Kuna wadada nawafahamu wakati nasoma walikuwa pisi kali balaa, sasa hivi wanatia huruma maana wamekuwa watu wazimz na hata hela ya kula hawana. Hata uwe pisi kali vipi, fainali uzeeni.
Hawajui hata bibi alikuwa binti tena pisi ya ukweli ila Leo ameinama na hana jino hata moja... upisi kali unaishaa [emoji1787][emoji1787]
 
Unajuaje kama hakuwa na nafasi?labda alikuwa na kazi, au alikuwa safarini n.k
Halafu sio kila anachotaka mke wako unafanya eti ili aridhike hata kama una uwezo huo.
Sintofahamu na imejuaje ilikuaje nk hayo yote tumeshajua ilikuaje
 
Ndiyo,kuliko kwenda kumtesa mtoto wa watu na kumrudisha nyuma kimaendeleo,

Sass Kama hapo wanaoumia zaidi ni upande wa mwanaume,ndo wanajua leo kumbe ndugu yetu alioa shda na alikuwa asemi,

Lakini upande wa mwanamke wanajua kuwa ndugu yao alikuwa kibwengo.
Eti kibwengo hahaha
Yani ukweli usemwe tu japo unauma. Mpaka unamiminiwa risasi basi shida ilikuwa kubwa sana.
 
kuna watu humu mkisoma vizuri mtajifunza sana...Wapo watu kwenye huu uzi wanaandika maneno ya busara sana ambayo yanatoa funzo kwenye jamii na hata kuijenga kwa wale wanaozingatia..

Japo pia wahuni hatukosekani na maneno magumu magumi tusameheane, lakini lengo kuu kujifunza na kuijenga jamii..
 
Tuko wachache sana. Mimi nategemea kipato changu 100% , sijawahi tegemea hela ya mtu toka nimeanza maisha. Wanawake wanaopenda starehe mara nyingi hela sio za jasho lau, hela unayoipata kwa kukomaa ni lazima uitumie kwa staha. Mapenzi yanaumiza , lakini ukiona mtu huendani naye mwache aende, usifanye maamuzi ambayo yatakufanya uumie maisha yako yote. Bora uumie kwa muda
Wewe umenielewa dada.

Mwanamke yoyote anaetafuta hela ni lazima aelewe circumstances mbalimbali na chagamoto ambazo zipo katika utafutaji kwahiyo hata hela zake au anazopewa ni lazima aziheshimu na kuzitumia kwa staha.

Wadangaji wengi nimewagunda kupitia huu uzi.
 
Ni rahisi sana kusema hivi ikiwa haufahamu mapenzi yanavyoumiza

Mapenzi yana nguvu kuliko uhai
Na ndiyo kilichojidhihiri hapo kwa hao ndugu
Wewe ni weak man, yani mzaifu kukufanya mapenzi yatawale hisia zako, mnapenda kijanga sana hamuna namna mnauweka mioyo yenu ikawa salama, mnapenda na kudumbikia wazima kama mchuzi na mnakua hamna namna yakutoka, hamna akili maana mwanaume dhaifu hawezi kufikiri kwa undani akili imekua kama imeganda, muwe majasiri ndugu zangu msiwe kama toys
 
USIWE ZEZETA MZEE, MWANAMKE KAMA HAKUTAKI, MPE TALAKA AENDE ZAKE, KIRI ULIFANYA MAKOSA KUCHAGUA NA USONGE MBELE, MAMBO YA HUYU NI MALI YANGU, SIJUI BLAH BLAH, NDIO MNAISHIA KUPANIKI NA KUUA KISHA NA NYIE MNAJIUA AU KUOZEA JELA
Na ndio shida ya kua na mwanamke mmoja. Ukishakua na mwanamke mmoja tu, akili yako na focus yako yote unaielekeza kwake. Unaanza kumuona kama mama yako vile na mda wote unamfatafata kujua yuko wapi, anafanya nini nk. Ukiwa nao watano you dont give a shit.

Na hakuna kitu cha hatari duniani, kama mwanamke ajue kwamba yuko peke yake!
 
Hivi kwani bunduki tu ndiyo zinahamasisha kudhuru au kujidhuru
Kwani angekuwa hana bunduki kuna visu mapanga hata kamba zipo
tutumie njia gani kudhibiti kamba na silaha nyingi watu wanazotumia kujidhuru

Kama hakuna njia ya kudhibiti hizi silaha nyingine hakuna sababu ya kuzuia watu kumiliki bunduki
Bundiki ni rahisi kutumia kurahisisha mauaji tofauti na kisu wewe ni mwelewa nimeshanga umewaza kama mtoto wa darasa la pili
 
Kabisa!

Nilifanya maamuzi magumu mapema sana ,na kama nisingefanya hivyo huenda tungebadilishana majengo ya serikali
Uko sahihi kabisa mkuu, wengine tumeamua kufa na tazi shingoni, tushakuwa watu wazima sasa.
 
Tena inaonekana jamaa alipata pesa nying kipind fulan labda za madin au sato akaoa huyo dada slay queen.. na sabab dada alipendea pesa.. sasa mwana inaonekana uchumi ukashuka gafla ndo dharau zilipoaanza.. na inaonekana ni dharau za muda mref.. na inaonekaa wameshazaa watoto so jamaa alikua anateseka sana.. akaona liwalo na liwe this time lazima ajimalize na ammalize

Nasemaga kila siku.. maisha ni meng sana zaid ya kuendekeza mapenz.. yaan unaua kisa penzi?. Daah
Samaki mkunje angali mbichi hizi pisi kali hizi yani hizi zinatakiwa zikunjue ukiwa umefulia na ukiwa una hela
 
Sasa ndugu yangu hata kama unachelewa kurudi home ni wajibu wako kumuambia mkeo mapema tu leo nitachelewa kurudi sababu moja mbili huwezi kuishi na mtu bila kuwa na mawasiliano unajifanyia unayo yataka simu zipo lazima kuambiana. Mimi nashangaa ndoa zingine mimi siwezi nje ya routine zangu ni lazima nimjulishe mwenzangu niko wapi nafanya nini unajenda kitu baina yako na yeye. Nadhani kuna kitu hakiko sawa katika ndo nyingi. Mwanammke wakati mwingine sio pesa anahitaji zaidi kuthaminiwa wanapenda ukimthamini kumuheshimu vitu vidogo lakini vinawapa faraja, kumpigia simu nitachelewa kwa sababu moja napita sehemu hii ni heshima kwake. Tujifunze kuishi na wake zetu, wanawake kama watoto wavumilivu sana lakini pia ni hatari sana ukiwavunjia heshima.
Ukimjua make wako vizuri,yale ya sirini mwake,ambayo ni bayana kwa majirani zako,bodaboda na waendesha bajaji...,hakika yawezekana ukamuuliza mkeo kwa hasira,kwanini anafanya hivyo wakati kilakitu unamfanyia.Wanawake hawa,baadhi yao ni siri tu ndo zinawabeba.
 
Na ndio shida ya kua na mwanamke mmoja. Ukishakua na mwanamke mmoja tu, akili yako na focus yako yote unaielekeza kwake. Unaanza kumuona kama mama yako vile na mda wote unamfatafata kujua yuko wapi, anafanya nini nk. Ukiwa nao watano you dont give a shit.

Na hakuna kitu cha hatari duniani, kama mwanamke ajue kwamba yuko peke yake!
Hayo ni mtazamo wako pia ambao siafikiani nao, unaweza ukawa na mwanamke mmoja tu mkaheshimiana vizuri. Na ikitoke mmeachana wanawake wapo wengi free.
Wanawake wazuri wapo, nimewaona na nimeishi nao, wanaume wabaya wapo pia, so ni kila upande kujielewa tu na ku move on inaoohitajika
 
Yy hakuwa na ratiba ya kwenda huko
Ni kweli lakini kumbuka binti alienda kwa mama yake, shida ni mwanaume kujenga wazo mke wangu sasa analiwa, namemlaumu sana yule mwanamke pisi kali marehemu kuacha kupokea simu calls 42 mhmhh siajabu angepokea yasingofika huko
 
Back
Top Bottom