Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Mwalimu wa shule ya Sekondari Jijini Mbeya, Julieth Kabuja (32) ameieleza Mahakama ya mwanzo Mkoani hapo kuwa ni bora ndoa yake ivunjike kuliko kumkabidhi mumewe kadi yake ya benki.

Ameyazungumza hayo mbele ya Mahakama ya mwanzo jijini hapo baada ya mumewe Charles Meshack (31) kufungua shauri la madai ya talaka akitaka kuachana na mkewe kwa kuhama dhehebu la katoliki na kuhamia la kilokole.

Aidha Meshack ambaye ni Askari Magereza amedai mkewe baada ya kuhamia katika ulokole fedha zake amekuwa akizipeleka kanisani kitendo kinachosababisha yeye kuzidiwa na majukumu ya familia.

“Naumia sana na majukumu, kodi ya nyumba nilipe mimi, ada za Watoto na chakula vyote mimi, halafu yeye mshahara wake apeleke kanisani, bora tuachane” alisema Meshack.
Hata hivyo Julieth aliiambia Mahakama kuwa yeye na mume wake wote ni wafanyakazi, lakini anashangaa anataka kumiliki kadi zote.

“Siku moja aliniamsha usiku na kuniambia nisipokubali kumkabidhi kadi yangu ya benki bora tuachane kwa kisingizio yeye alinilipia mahari hivyo mimi na kila kitu changu kipo chini yake, yaani kazi nifanye mimi halafu mshahara nimuachie huyu bwana, nipo tayari kuachika lakini siyo kuacha kadi yangu” alidai Julieth

Baada ya Hakimu Hafsa Shelimo kusikiliza pande zote mbili, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu kwaajili ya hukumu.

Chanzo: Swahili Times
 
Wanaume tafuteni pesa, pesa ya mwanamke ni yake, ila ya mume ni yenu.
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
No kwenye ndoa hakuna mambo ya mume kupeleka mke mahakamani ndani ya ndoa kidume unakomaa kiume akibana upaja acha ataenda yeye mahakamani wewe mpige tukio tu akili itamkaa sawa
 
Hata kama mwanaume ni kichwa cha familia ila namsapoti huyo mwamba kutaka ndoa ivunjike huo ni upimbi. Unafanya kazi kwa bidii mnaishi kwa tabu ila hela ya mwenzio ingekua hata anajenga kwao au anajinunulia nguo ni sawa ila anampa fala mmoja tu huko anayejiita mtume huo ni ufala wa hali ya juu.

Huyo mwanamke kudai mume anataka Kadi ya benki ni uongo asilimia 900. Ampe talaka tu akalitumikie kanisa vyema.
 
Mama abakie hapo hapo.
Anaitaka ATM aisee

Mwanamke kweli umkabidhi mume ATM? That is too much

Wanawake vizuri kuomba Mungu kutopata kidume kilofa kama hicho hopeless kabisa kiofisa magereza

Kinadhalilisha jeshi la magereza wanawake wenye kazi zao watakatakaa kuolewa na Askari magereza kuwa watawapokonya ATM
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Ila inauma zaidi. Yaani uoe wewe, umlishe, uvalishe, alale kwako alafu mshahara ampe mchungaji tena akiwa mchungaji mwanaume ndio inachoma hadi miguu
 
Hata kama mwanaume ni kichwa cha familia ila namsapoti huyo mwamba kutaka ndoa ivunjike huo ni upimbi. Unafanya kazi kwa bidii mnaishi kwa tabu ila hela ya mwenzio ingekua hata anajenga kwao au anajinunulia nguo ni sawa ila anampa fala mmoja tu huko anayejiita mtume huo ni ufala wa hali ya juu.

Huyo mwanamke kudai mume anataka Kadi ya benki ni uongo asilimia 900. Ampe talaka tu akalitumikie kanisa vyema.
Huyo mwanaume anataka pesa ya mwanamke tu

Uanaume sio kuvaa suruali na dude kama bunduki katikati ya suruali

Ni uwezo wa kuhudumia familia bila kuelekea ku force ohh nipe kadi ya benki na ATM na namba ya Siri

Watetezi wanasheria wa haki za wanawake na NGo tetea haki za wanawake siku hiyo kesi iliyotajwa jazaneni hasa kuonyesha solidarity na huyo mama. Maafisa balozi wa nje pia wawepo wa dawati la balozi wa jinsia.

Mfumo dume unahitaji kusomeshwa.

Hakimu na wewe kakamaa mwanamke mwenzio huyo. Toa hukumu ya kihistoria ambayo ita trend dunia nzima ili mwanaume yeyote Mwenye tabia kama hiyo asije tokea.
 
Huyo bwana hazimtoshi
Hakimu hii kesi yaweza kumpaisha kimataifa na kuipaisha nchi kimataifa kuwa Tanzania ina mahakimu mahiri
Ashirikishe mahakimu nguli, mawakili nguli wa hataki za wanawake na NGO ku draft hiyo hukumu

Hiyo kesi ni mfumo dume versus mfumo jike kwe rights za mwanamke

Handle carefully hiyo kesi imebeba image ya nchi kwenye haki za mwanamke awe wa kanisani au nyumbani au mfanyabiara nk
 
Back
Top Bottom