Hii kesi kila mmoja anavutia kwake.
Lakini kama mwanamke anafanya kazi na hachangii chochote hata kama mwanaume ndio jukumu lake, mwanamke amekosea sana.
Wanaume wanaoa ili wapate utulivu lakini pia wapate msaidizi, usaidizi ni pamoja na Hili pia, mke una kipato ila hata kuchangia kidogo hakuna inaleta ukakasi.
Japo pia wanaume baadhi husababisha hiyo hali wanawake kugoma kutoa chochote, unakuta mwanaume ana mke ila huduma zina sua sua lakini nje ana michepuko kibao na lazima ihudumiwe. Mwanamke anaamua bora amkomeshe mwanaume amuachie majukumu apambane nayo na michepuko apambane nayo.
Kwa hiyo hatuwezi kusemea lolote kwa sababu ukweli halisi wa hali kufikia hapo wanaujua hao wawili.