Mume anapokea 1M salary kwa mwezi na mke anapokea 3M, kutakuwa na heshima kweli hapa?

Mke analetwa home na gari la kazini mume anapanda dala dala, ukitela fyoko unaambiwa kaa pembeni.


View attachment 2940731

Vijana wa siku hizi kwa uoga hamjambo.

Muhamad mkewe Khadija alikuwa amemzidi Umri na pesa na bado alikuwa anamheshimu.

Mwanaume lazima ujitambue. Kuwa kwako na pesa hakukufanyi uitwe mwanaume au mkeo akuheshimu. Shauri yenu
 
Japo ni wachache sana wanawake wa design hii lakini wapo
 
Hii ni script inafaa sana kwenye jua kali mpe Lamatah😂😂😂😂😂
 
Moja kwa moja bila kupepesa macho hapo hakuna heshima, labda huyo mwanamke awe anamuabudu Mungu wa kweli au awe ana maadili ya ndoa. Kwanza ndugu wakishajua dada yao kakuzidi kipato utaonekana nyanya puza, hakuna dharau wataacha kukuonesha wakiwemo wakwe. Ndio ilivyo. Kwanza ndugu wa mke watajazana home kila mara watakuja kufaidi vinono anavyopata ndugu yao na hutawaambia kitu. Mwanaume utaonekana ni kibaraka tu na itabidi uvumilie vitimbi na visa atakavyokufanyia mkeo ili ndoa isivunjike na kusambaratika kutokana na mke kujaa kiburi na kutokuwa na heshima kwa mume wake kwa kuwa anamzidi mshahara.
 
Wee haya umeyajuajee? Alikuambia huyo mwanaume au?
Maana mwanamke inaonesha ni msiri mnoo.
 
Huyo ni mwanamke wa nguvu hawa wa siku hizi siku 2 tu akilipa bill mtaa mzima utajua
Halafu unadhani basi watu wazima sana, wote wako kwenye 37 sema mke amemzidi mme miezi kadhaa. And by the way jamaa alifukuzwa kazi mwanzoni mwa 2015 so si miaka kumi ana kama miaka 8 kuelekea 9.
 
NDOA ni mpango wa Mungu kwa wanadamu. Mwanamke aliumbwa AMSAIDIE mwanamume. ukiona kuna mke flani hawezi kumsaidia mume wake ujue hiyo ndoa sio mpango wa Mungu. walilazimisha tu. "wawili watakuwa mwili mmoja". NDOA ni jambo la rohoni (ndani sana) ni zaidi ya vitu vya kuonekana kama pesa, mali, ...


NDOA iliyo katika mpango na mapenzi ya Mungu ni raha sana!!!!!
 
“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
— Mwanzo 2:18 (Biblia Takatifu)

ukiona mke anapata shida kumsaidia mumewe, jua hiyo ndoa ina walakini
 
Tuwapate wapi wanawake kama hao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…